Hapana bwana hili kosa ni dogo mno wala sio la kubebea bango. Wakati mwingine watz tunazidi kujishusha; mbona miafrika mienzetu huwa inapuyanga tu kiingereza tena inakosea sana tu lakini sisi tunakuwa too keen ndio maana matokeo yake tunakosa confidence ya kuongea kiingereza mbele za watu. Waangalieni wenzetu wa Nigeria wanakosea sana tu kiingereza tena pronounciation ni zero, lakni hawababaiki wanakwenda tu. Vilevile mbona tukikosea kuongea kiswahili hatu-mind vile lakini ikija kiingereza inakuwa issue, lugha ambayo to some of us ni ya tatu hata ya nne? Hapa napo tunahitaji ukombozi, uzuri wa hili tatizo kulitatua hatuhitaji dola za Bush, ni kubadilika kichwani tu basi!
I know
Kiongozi anatakiwa kuweza ku contain slips kama hizo, mwisho wake atatoa siri za serikali kwa Freudian slips kama hizo.
Kwa taarifa yenu, niliwahi kumsikia hata Nyerere akichapia; Mkapa, Mbeki, Obasanjo, Moi, Museveni na wengine wengi tu!!!!!
Mkuu hapo nakuunga mkono. Mimi mara nyingi tu niki-youtube "bush idiot" naona mara kibao anachapia Kiingereza, na inaonekana kuwa ni kiongozi wa US ambaye kwenye hotuba zake nyingi anazotoa bila kusoma kiingereza (grammar)kinapimpiga chenga. Mkuu wa kaya kweli alichapia aliposema "let [him] be a friend of Tanzania", hapa kwa maana fulani alikuwa na maana Obama, kwa sababu yeye ndiye him, sio her. Lakini kwa walioelewa hii inatoka na influence ya mfumo dume, na kuona kuwa maa nyingi wanaogombea ni [him] na sio [her], kwa hiyo mimi binafsi naona muungwana alichosema kilikuwa na maana yoyote atakayekuwa rais.
Tanzania tuna maajabu sana ya kupima uwezo wa kiingereza wa mtu kuliko hata waingereza wenyewe, ajabu sana!
Lugha ni chombo cha mawasiliano si chombo cha taaluma,inatosha mtu akiwasilisha ujumbe unaoeleweka kwa hadhira kusudiwa
Exactly.There's no room for broken English kwa wale wanaofahamu fika kwamba KAMA HUWEZI USIONGEE.Bush akikutana na Angela Markel,mwanamama huyo anaongea Kijerumani,akikutana na Putin,Mrusi huyo anaongea Kirusi,akikutana na Sarkozy,Mfaransa huyo anaongea Kifaransa,na hata huko Benini presidaa wao aliongea kifaransa.Kulikuwa na ugumu gani wa kutoa speech kwa Kiswahili?Pundit,
..nimechanganyikiwa kidogo na hiyo sehemu niliyo-bold. may be i am reading too much? but, why is JK excited that Bush's tenure is winding up?
Nyani Ngabu,
..JK served as a Min' of Foreign Affairs for 10 good years. English, not swahili, is the official language of our government. He should have no excuse for not speaking good english.
Unakumbuka akina KARL PETERS walikaa Afrika miaka mingapi kabla hawajaleta Ukoloni?Endelea kuwa na furaha ya Bush kukaa siku tatu hadi hapo utapoelewa kwanini HASA alikaa siku zote hizo.Dont believe the hype brodha.Mwafrika wa Kike,
Kweli hili la rais Bush, mpeni JK sifa zake. Hata huku Europe sikumbuki kuona rais wa USA kakaa siku tatu kwenye nchi moja.
Nafikiri kuna Watanzania wenzetu wengi ambao wamefaidika na hiyo ziara yake.
Pamoja na kutokumpenda Bush, lakini hili la kukaa Tanzania siku tatu, mimi namshukuru na kuwapongeza wote waliofanikisha hilo.
Again,hakukuwa na ulazima wa yeye kuongea Kiingereza kama hakipandi sawasawa.Hatuishi katika dunia ya kusifia nusu glasi ilhali kuna uwezekano wa kuwa na full glass.Sijakuelewa mkuu, english ni lugha ya 3 kwa wengi wetu na kujibu swali vizuri haijalishi kama lugha unayotumia umepatia au laaa ila tu kama umeweza kueleweka...
Hii ya kuanza kucheck hata spellings za jinsi JK alivyojibu kwa kiingereza sioni kama ina mantiki....
Kwa vile Kiingereza sio lugha yetu,then why not speak Swahili,which JK has repeatedly vowed to promote?Just imagine,the world watching a leader of a nation they would like to embrace in the promotion of Swahili,only,to their disappointment,to see him speaking in some Broken English....Promosheni ya Kiswahili haiwezi kufanikiwa iwapo hata wachovu wa Kiingereza wataendelea kuking'ang'ania.Nyani Ngabu ,
I couldn't agree with you more , kiingereza sio lugha yetu kwa hiyo makosa aliyoyafanya Kikwete ni ya kawaida kabisa kwa mtu ambaye kiingereza sio lugha yake ya kwanza . Mbona Bush anaadmit ya kuwa hana matatizo ya lugha na mwenyewe analikubali hilo ! Kitu kimoja ninachoweza kusema ni kuwa Kikwete alikuwa na confidence ya khali ya juu this time , nadhani ni muhimu kuanza kutoa credit pale panapostahili .
Zaidi ya hayo nahisi watu hapa wana muda mwingi sana ndio maana wanaangalia kila sentence aliyosema Muungwana
1.Kweli,muhimu ni mawasiliano na ndio maana wengine wanalalamika.Alivyochapia JK ametengeneza tafsiri kwamba anafurahi Bush kumaliza muda wake madarakani.Asante sana nyani ngabu kwa hoja yako murua
Ifike wakati tuelewe kuwa lugha ya kuongea ni tofauti na lugha ya kuandika,hata wewe ukizungumza kiswahili leo wakati unahutubia bila kusoma popote tutakapoenda kuandika kazima tutaki-hariri ili kinyoke,isitoshe bush mwenyewe kiingereza anachoongea si kizuri sana,muhimu pale ni mawasiliano,je unaeleweka?hii kasumba ya kiingereza sahili inatufanya watanzania wengi tulio huku nje ya nchi tuogope kuonesha vipaji vyetu kisa tu kuogopwa kuchekwa eti hujui kiingereza.Hivi naomba niulize watu gani wanaongea kiingereza vizuri afrika,Nigeria,kenya,uganda,south africa au Egypt.Mwenzenu nikiangalia sana mfano wanageria naona wanaongea a language similar to english but they are very confident about it.
Haya wachina,warusi,wajapan je?hapa ulaya waafrika wabongo tunaonekana bora kuliko hao.Mfano mdogo tu,kwenye chuo nilichopo kuna kasumba ya kuwasubject international students whose first language isnt english wapigwe paper,hata kama una toefl ukishindwa unaingizwa darasani six month sambamba na masomo yako.
Wabongo wote tuliopiga hilo pepa tulitoka na A tukiwaacha wazungu na jamii zao.Je,hatujui english?tena wao native speakers wanaongea kibaya,kuliko sisi waambie waandike utacheka,yaani ni kama sisi kile kiswahili cha manzese na kariakoo,ndicho wao wanaongea na kuandika.They never speak formal english.
Kwa mantiki hiyo kikwete big up,watanzania tujiamini hasa huku ughaibuni,tusijishushe.Ok,wakuu tuendelee na hoja.
EXACTLYKama hujiu Kiingereza ongea Kiswahili watu watakuwekea interpreters. Ukishaongea Kiingereza maana yake unajua Kiingereza na ukikosea tunakulima kama kawaida.
Ukiona unaanza kusifiwa na vyombo vya marekani basi ujue kuna something wrong kati yako na raia wa nchi yako........
Icadon,
Katika suala zima la Kikwete kuwa "excited" juu ya Bush kuondoka White House, message iliyofika ni ipi?
"Of course, people talk with excitement of Obama well, our excitement is that President Bush is at the end of his term, and the U.S. is going to get a new President, whoever that one is. For us, the most important thing is, let him be as good [a] friend of Africa as President Bush has been."
Swali lilihusu Obama, yeye katika kujiuma uma kajikanganya akaanza kusema
Sasa hapa ni kama mgeni kaja nyumbani halafu siku ya kuondoka unasema I am so excited you are leaving, mgeni anaanza kujiuliza huyu jamaa alikuwa ananiona mzigo nini? Maana kwa kawaida watu marafiki husema "I am so sad to see you go"
Sasa Kiwete mnaosema message ilifika ni message gani? Kwamba the Kikwete administration could not stand Bush and could not wait to see him go?
Yaani Kikwete alishindwa kusema "We are saddenned to see a friend concluding his presidential term and getting ready to leave office".Au hata ku mute tu?
Swali lilihusu Obama, yeye katika kujiuma uma kajikanganya akaanza kusema
Sasa hapa ni kama mgeni kaja nyumbani halafu siku ya kuondoka unasema I am so excited you are leaving, mgeni anaanza kujiuliza huyu jamaa alikuwa ananiona mzigo nini? Maana kwa kawaida watu marafiki husema "I am so sad to see you go"
Sasa Kiwete mnaosema message ilifika ni message gani? Kwamba the Kikwete administration could not stand Bush and could not wait to see him go?
Yaani Kikwete alishindwa kusema "We are saddenned to see a friend concluding his presidential term and getting ready to leave office".Au hata ku mute tu?