JK...Arusha Mjini kunani?

Mbwiga_Plus

Senior Member
Jan 5, 2011
163
42
JK alishuka KIA juzi jioni, mara baada ya kushiriki uchangiaji wa hospitali ya ccbrt huko Dar.

Alipitiliza kwenda Ngurdoto, akalala huko...Ngurdoto iko Maji-ya-Chai, eneo la nje kabisa ya Mji wa Arusha.

Asubuhi aliondoka hapo na Msafara, akapita eneo la Mianzini(Arusha Mjini) kwa kasi kubwa mno, moja kwa moja hadi Wilaya ya Longido, ambako alitoa takrima kwa Wafugaji wa huko.

Mida ya saa 9 aliondoka huko na kukata kona pale Tripple A, na kushuka Ngarenaro Msikitini, akarudi Kiwanja cha Ndege kISONGO akapanda ndege na kusepa zake Dar!

Swali:..JK ana nini na Arusha Mjini?...kwanini anawapita wapiga kura wake bila salamu kiasi hicho tokea alipochaguliwa, wakati kuna miradi mingi inahitaji kuzinduliwa?


JK, TUNAKUOMBA TEMBELEA Arusha...wewe ndiye rais wa nchi yetu yote, tunasikitika kuona unatupitiliza kama vile tumekuwa raia wa nchi nyingine!
 
tatizo lenu nyie watu wa Arusha hampendi Ubwabwa.
Si mnaona mambo haya?
6.%2BNape%2Bakila%2Bchakula%2Bkatika%2Bkambi%2Bhiyo%2Bkwenye%2Buwanja%2Bwa%2BCCM%2BKirumba.jpg
 
Sioni Mantiki ya thread yako, haiwezekani afanye kazi ya kusalimia watu bila kuwa na ratiba nao, sio Arusha tu hata Chalinze haiwezekani. Ungeniambia huko alipokuwa anagawa fidia yalitokea hayo ningekuelewa. Ebu Tuache ushabiki wa kisiasa kutufanya kuandika vitu bila kufikiria.
 
Kwa kweli this is news kwangu.... Kwa misafara yake yoote, sikuweza fikiri hajawahi fika A town.... Maybe kama you are pulling my leg.
 
JK ana kinyongo cha ajabu sana! Au ni aibu? Sasa anapita kama mwizi ilhali yeye ni raisi!inabidi akubaliane na ukweli maisha yaendelee
 
Kwa kweli this is news kwangu.... Kwa misafara yake yoote, sikuweza fikiri hajawahi fika A town.... Maybe kama you are pulling my leg.
hajawahi dadangu ni kama tu abiria wa hood anayetokea dsm kwenda mbeya inambidi aipite iringa akiwa kwenye basi ...
 
Kama ulikuwa hujui, angalia na hii..........Chezeya Ubwabwa wewe!!!
d52.jpg

Huyo mwenye mvi na masharubu kama ni Marmo, basi inadhihirisha kabisa kwamba Arusha hawapendi bwabwa. Tazama sahani yake alivyojaza viazi..!!!:lol::lol:
 
Back
Top Bottom