JK amuweka kitanzini Profesa Kapuya

JK amuweka kitanzini Profesa Kapuya

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,087
Reaction score
34,884


1.png

RAIS Jakaya Kikwete ameviagiza vyombo vya dola kuhakikisha vinamkamata mtu yeyote bila kujali cheo, atakayebainika kumbaka au kumuoa mwanafunzi wa shule.


Ametoa kauli hiyo huku aliyekuwa waziri wa wizara tofauti katika awamu mbalimbali za uongozi, Profesa Juma Kapuya, akiandamwa na tuhuma za kumbaka na kutishia kumuua binti, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16.


Ingawa Rais Kikwete hakutaja jina, lakini ni dhahiri kuwa kauli hiyo inamgusa pia Profesa Kapuya, Mbunge wa Urambo Magharibi (CCM).


Akizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya hadhara kwenye wilaya za Itilima, Meatu na Maswa mkoani Simiyu, Rais Kikwete alisema mtu anayefanya mapenzi na wanafunzi lazima akamatwe, ahojiwe na kufunguliwa mashitaka ya ubakaji na si vinginevyo.


“Kuna watu wanafanya mapenzi hadi na wanafunzi wakati sote tunajua ukimwi upo na hauna dawa na unaua. Kwa hiyo kila mmoja wetu awe makini kujikinga nao na tuepuke kuwaambukiza wengine,” alisisitiza Rais Kikwete.


Wakati Rais Kikwete akisisitiza wahalifu wa makosa ya kubaka na kuoa wanafunzi wachukuliwe hatua, polisi jijini Dar es Salaam wamekuwa wakisuasua kumchukulia hatua Profesa Kapuya licha ya binti anayedaiwa kumbaka, kufungua jalada namba OB/RB/21124/13 katika kituo cha Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam, akidai kutishiwa kuuawa na mbunge huyo.


Kauli ya Rais Kikwete imeonyesha dhahiri kukerwa na moja ya ujumbe mfupi wa maneno wa simu ya mkononi kutoka kwenye simu inayodaiwa kumilikiwa na Profesa Kapuya kwenda kwa binti aliyebakwa, ambapo mbunge huyo alijigamba kwamba serikali haiwezi kumfanya chochote.


Ujumbe huo unasomeka hivi: “Mkiuawa itakuwa vizuri…itawapunguzia gharama za kuishi, usitake kugombana na serikali mtoto mdogo kama wewe, sisi ndiyo wenye nchi yetu, mwenye hilo gazeti ni Mbowe, sasa mwambieni nyumba ya kuishi si mmemuingizia hela leo?

Mnatumika tu bure watu wanaingiza hela nyingi, ila mmenitibua lazima niwaue, wiki hii haitaisha, nitapiga kambi kote, jana si wamekuficha, tuone utalindwa milele, maana washatengeneza hela, lazima mvae sanda tu, hilo sio ombi ni wajibu wenu, mnajitia na nyie mafia watoto siyo, watoto wetu wanauza unga nani anawakamata? Nani atapingana nasi.”



Habari kutoka Ikulu ya Rais Kikwete zinaeleza kuwa kiongozi huyo wa nchi amekerwa na kauli ya mbunge huyo wa Urambo Magharibi kwamba serikali haiwezi kumfanya jambo lolote.



Ni kutokana na kauli hiyo, mtoa taarifa wetu alisema rais aliagiza vyombo vya dola kufuatilia kwa karibu sakata hilo na kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake.



Pamoja na msimamo wa Rais Kikwete na binti anayedaiwa kubakwa kuripoti polisi, Profesa Kapuya alifanikiwa kusafiri nje ya nchi huku polisi wakimshuhudia bila kumtia mbaroni.


Akiwa nje ya nchi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alikaririwa mara kadhaa akijigamba kuwa polisi inamsaka mbunge huyo na itamtia mbaroni mahala popote alipo.


Hata hivyo, Profesa Kapuya alirejea nchini juzi huku polisi wakimshuhudia bila kuchufkua hatua zozote.



Mwanafunzi huyo anadai kubakwa na Profesa Kapuya kwenye moja ya hoteli ya kitalii iliyoko jijini Dar es Salaam mwaka 2011, na kurudia tena kitendo hicho ndani ya ofisi yake katika Jengo la Biashara Complex lililoko Mwananyamala Juni 3, 2012 alipomuita kwenda kuchukua ada.

Source: Tanzania Daima

 
Inatia matumaini jamani ngoja tusubirie uenda udhaifu wa mr fastjet ukaanza kupungua kutokana na hili suala.
 
Kama ni wakukamatwa angeshakamatwa lakini hii ni kiini macho,mbona kuna taarifa alirejea j2 saa 5 akaelekea buibui hotel m'nyamala akiwa amevaa kofia pana?
 
Ni porojo tu. CCM ni chama cha vibaka wanaolindana na wala hakuna atakayemkamata Kapuya!
 
Maajabu Hivi Polisi Oster Bay Nao Si Watuhumiwa? Inakuweje Afungue Kesi Pale Dogo Hayupo Serious Na Hili Swala. Emirate Degree Nae Waajabu Sana, Siku Ngapi Sasa Hajamshika Kapuya, Au Kale Kakauli Ka Watoto Wetu Wanauza Madawa........ Napendaga Kusema NYERERE WENGI HATUKUFANANA NAE!
 
Maajabu Hivi Polisi Oster Bay Nao Si Watuhumiwa? Inakuweje Afungue Kesi Pale Dogo Hayupo Serious Na Hili Swala. Emirate Degree Nae Waajabu Sana, Siku Ngapi Sasa Hajamshika Kapuya, Au Kale Kakauli Ka Watoto Wetu Wanauza Madawa........ Napendaga Kusema NYERERE WENGI HATUKUFANANA NAE!
Mkuu Hakutatokea Kiongozi Shujaa,shupavu na mpenda nchi yake kama Mwalimu Nyerere Mungu amuweke pema peponi. Waliobakia karibu wote ni Viongozi wasanii tu kaka.
 
hivi mambo ya EAC,hayaruhusu kwenda kufungua kesi mahakama ya nchi nyingine,kama kenya au Rwanda??
 
Ivi mwalimu nyerere mnamfanya kama malaika wakati yeye ndio ametutengenezea katiba hii ambayo inafanya majambazi, ufisadi, ubakaji.... na itaendelea kutunyanyasa hii katiba mpaka vita itokeee..
 
Prof Kapuya ni kam nani asiweze kukamatwa Mkuu? Umemsikia Mkuu wa nchi Rais J.Kikwete anavyosema katika Thread hapo juu?





Hivi mkuu unaelewa maana ya danganya toto wewe? Kwani kuna vingapi JK anavikemea na mpaka leo hii havijatekelezwa. Jiulize ile list ya wauza unga kaifanyia nini mpaka sasa na wakati anakemea utumizi na uuzaji wa dawa hizo? Anataka rushwa ikomeshwe na wakati sie wote tunajua kuwa TAKUKURU ndiyo iliyokithiri kwa rushwa, anafanya nini? Kapuya ni profesa na si mpumabvu kusema aliyoyasema kwani anajuwa JK ni dhaifu na hana ubavu wa kumfanya chochote.
 
Hii ishu ya kapuyakapuyaka ndo ishaisha ivo..!
 
ckuzote hizo ajakamatwa walikuwa wanasumbiri .changa la macho hilo
 
Changa la macho hiloooooo!
Pembeni 'Usiniangushe nyingi'.
 
Back
Top Bottom