Kuhani,
..kwani Julie Manning alipotoka kuwa AG moja kwa moja aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu?
..binafsi sifahamu Mama Manning alikuwa akifanya shughuli gani baada ya kuondoka wizara ya sheria, mpaka Raisi Mwinyi alipomteua kuwa mjumbe wa Tume ya Uchaguzi.
..vilevile sifahamu ni sababu zipi zilizopelekea Mama Manning akaondolewa toka kuwa Waziri wa Sheria na Mwanansheria Mkuu wa Serikali, na nafasi yake kuchukuliwa na Joseph Sinde Warioba.
..hivi kutoka kuwa AG na kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu siyo DEMOTION? vipi kuhusu AG[lubuva] kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa? au DPP[shaidi] kuwa Jaji wa Mahakama Kuu?
NB:
..kama madai ya Jaji Munuo ni kweli, kwamba yeye ndiye mwanamke wa kwanza kuteuliwa Jaji wa Mahakama Kuu, basi inawezekana Mama Julie Manning alikuwa mtaani kwa kipindi fulani kabla naye hajateuliwa kuwa Jaji.
Kuwa jaji wa mahakama kuu kutoka AG ni promotion, na mara nyingi AGs huwa wanateuliwa kuwa majaji na ndicho kitakachotokea kwa Johnson Mwanyika (kama JK akiamua kumwondoa). Lubuva pia alikuwa AG kabla ya kuteuliwa kuwa jaji wa mahakama kuu na baadaye mahakama ya rufaa. Kumbuka uteuzi wa majaji hapo mwanzoni kabla ya sheria haijabadilishwa, ilikuwa kwamba, Rais akimteua jaji hawezi kumfukuza kazi. Kufukuzwa kazi ilikuwa mpaka jopo la majaji kutoka jumuia ya madola wafanye uchunguzi kuhusiana na makosa anayotuhumiwa kwayo, na tume ya jopo hilo ndo lipendekeze kwa rais hatua za kuchukua kama ni kufukuzwa au vinginevyo.
Sheria hii ilifanyiwa mabadiliko miaka ya mwishoni mwa utawala wa Mzee Mkapa. Na kwa sasa rais ana uwezo wa kumfuta kazi jaji yeyote anayemteua.
Ngeleja, naomba usome Katiba kama ilivyorekebishwa kwani hayo maneno yenye wino wa Simba siyo sahihi. Kwa kukusaidia, soma Ibara ya 109 (5) na ibara ya 110A. Ibara ya 110A ndiyo inashughulikia nidhamu ya Majaji. Rais anaweza kumsimamisha Jaji baada ya kushauriana na Jaji Mkuu lakini hawezi kumfuta kazi kabla ya kuunda tume huru ya majaji wa Commonwealth of nations.
Kuhusu Manning kuteuliwa kuwa Jaji baada ya AG, siyo sahihi, kwani yeye alikuwa Jaji kwanza ndo akateuliwa kuwa AG. AG akiteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ni demotion kwani wadhifa wa AG unalingana na Majaji wa Rufani na siyo wa Mahakama Kuu. Ndiyo maana Lubuva aliteuliwa kwenda mahakama ya rufani. DPP kuteuliwa kuwa Jaji ni kwa ajili ya maslahi ya kustaafu lakini siyo promotion na ndiyo maana hata aliyekuwa Naibu Mwanasheria Mkuu aliteuliwa kuwa jaji ili akistaafu apate pension nzuri.

Tujikumbushe kutoka kwa wanafiki kama hawa wanaolaani udini leo kwenye uchaguzi wa Mwanasheria mkuu. Double standards za JF.Huyu jamaa ni dini gani vile....!! Maana teuzi za Muungwana bwana hufanyikia Jamatini ...
Ukweli wa mambo, na kama watu tunasoma na kufuatilia historia ni kwamba Julie Manning ndiye mwanamke wa kwanza kuwa jaji wa mahakama kuu nchini Tanzania, na kimsing alikuwa mwanamke wa kwanza kuwa jaji wa mahakama kuu katika Afrika Mashariki na kati.Hii imerekodiwa kwenye kitabu kinaitwa "Chronology of Womens History" kilichoandikwa na Kirstin Olsen. Na hii ilikuwa mwaka 1973. Na kisha mwaka 1975 Julie Manning alikuwa waziri wa sheria hadi mwaka 1979. Baadaye amekuwa kamishna kwa muda mrefu kwenye Law Reform Commission, na pia kamishna kwenye tume ya uchaguzi ya Tanzania.
Huyu jamaa ni dini gani vile....!! Maana teuzi za Muungwana bwana hufanyikia Jamatini ...
Hii taarifa ina makosa, angalia hayo maandishi mekundu hapo juu. Jaji jandu aliteuliwa kuwa kuwa Jaji wa mahakama kuu zaidi ya miaka miwili (naweza kusahihishwa)
Nashukuru mkuu! It seems like it was yesterday!Sijasema Ujaji Mkuu bali alitoka uwakili na kupelekwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
exactly! as far as I know
I would not dare to speculate the motives naamini JK anatimiza wajibu wake wa Kikatiba.