JK ampa shavu Anna Abdallah

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,446


Rais Jakaya KIkwete amemteua Mheshimiwa Anna Margaret Abdallah (mb) kuwa mwenyekiti mpya wa bodi ya Korosho.

Source: Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
 
Bado ile kasumba mbaya ya kuwateua WABUNGE kwenye taasisi na vyombo vya DOLA inaendelea. Mh Zitto ulipambana sana hili liondolewe kwenye mashirika ya UMMA. Hakuna aliyekusikia? Kamati yako ya Kudumu ya Mashirika ya Umma Itamuwajibishaje mama huyu kiburi sana akienda ndivyo sivyo?
 
Anampa shavu shemeji yake. Ila tusitarajie mendeleo yoyote kwenye korosho katika kipind hicho huyu mama anaongoza hiyo bodi. Hata ukisikiriza hija zake huwa ni masaburi flani hivi
 
Anampa shavu shemeji yake. Ila tusitarajie mendeleo yoyote kwenye korosho katika kipind hicho huyu mama anaongoza hiyo bodi. Hata ukisikiriza hija zake huwa ni masaburi flani hivi

Hivi Korosho inalimwa haswa wapi?
Huyu mama anatokea huko kunako limwa korosho?
Je huko kunako limwa korosho hakuna mtu mzuri anae weza simamia bodi hiyo?
Je huyu mama makazi yake yapo karibu na wakulima wakorosho ili kujua vilio vya wakulima wa korosho?
Je huu uteuzi hauna harufu ya kaupendeleo flani?
 
Hii ni Bongo kaka!
Tangu lini maswali yako yakafanyiwa kazi nchini kwetu hapa?
 
Pius Msekwa mwenyekiti wa bodi NCAA, Anna Abdallah mwenyekiti wa bodi ya korosho. Ni posho za uzeeni kwa kwenda mbele!
 
Mpaka watakapo baki mifupa mitupu yeye na mumewe watabaki wenyeviti wa bodi wizi mtupu yaani Tanzania hii hakuna watu wasomi,wenye uzoefu wa kuweza kuhead hizo bodi ila hao vigagula wezi,wizi mtupu nchi hii,mtu aliingia menopause miaka hamsini iliyopita eti bado ana peta KIkwete ni jeuri wa kuzaliwa dawa nikumg"oa tuu
 
Hii ni Bongo kaka!
Tangu lini maswali yako yakafanyiwa kazi nchini kwetu hapa?

Ndo yale yale Mkulima mahiri wa mahindi una mpa uenyekiti wa bodi ya Pamba sijui vinaendana?
Au nae awepe pale anauza tu sura siku zinaenda...?
Maswali mengi majibu ya kina Salva duh
 
Mods,
Mmefanya vizuri kuziunganisha hizi threads hizi. Sikuwa nimeiona hii ya Fidel80. Kwa nini teuzi hizi ni kwa watu na majina yaleyale tangu miaka hiyo?
 
 
Yani huyu mama JK anaona bado anatakiwa kuendelea kula bata? Kati ya vijana woooote wanaomaliza hata UDOM hajaona hata moja? JK hebu kua kidogo bana..hata mimi nina kauzoefu ka kutosha..nipigie pande basi best!
 
sitegemei jipya toka kwa huyu mama!alikuepo tangu enzi za nyerere hapo creativity zero,wakulima wa korosho mlie tuu!
 
 
 
Hivi vibibi kwa nini visistaafu!! Wanawabania nafasi vijana, ambao wamemaliza vyuo vikuu kupata ajira..tangu miaka ya 50 hadi leo vipo kwenye madaraka.
 
hivi hamna watu wengine wa kulitumikia taifa hili zaidi? kila siku ni wale wale tu.. tena wale ambao ni zero kabisa upstairs
 
...Jirani zetu hapo wameamu kuachana na huu ujinga wa kumuachia mtu mmoja ndio ateue watumishi mbalimbali kukataa upuuzi wa kuletewa makapi yale yale tuliyokwishayachoka utadhani nchi haina watu wengine. Mbaya sana mtu anaweza kushikwa na kifafa ghafla ukasikia kamteua Funzadume kuwa mwenyekiti wa bodi au mkurugenzi wa taasisi fulani...si balaa hiyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…