JK aliulizwa maswali haya na wazee wa Serengeti,na majibu yake kuhusu BILILA

MJASIRIMALI WETU ANAMILIKI HII KITU,
006980-02-bedroom-savannah-view.jpg
 
Hii kitu acha Tu ni
006980-04-presidential-dining-room.jpg
Balaa, kwa Bongo nzima hii inaweza shika namba Mbili baada ya ile ya kule Singita nako Serengeti
Singita ndo VIP, JK huwa anapumzika pale.P ale ndo kwa mara ya kwanza nilisika Human Resources Manager analipwa milioni 17 kwa mwezi.amazing!
 
Mkuu Mwita Maranya hapo juu waeza dokeza ni makabila/mikoa gani ambayo huzawadiwa sana hivi vyeo visivyo na tija kwa maendeleo ya taifa? (DCs na RCs)

Watu wa ukanda wa Pwani Pwani ya Bahari ya Hindi na watu wenye asili ya kiswahiliswahili ndo wananeemeka na hivi vyeo
 
Hili suala mimi nililiweka wazi katika uzi mmoja wa Lokissa, Mdau mwenzetu unaohusu Bilila...Hata hivi sasa ilivyo chini ya Four Seasons bado ni mali ya JK..Mkuu Lokissa utakubaliana na mimi hapa kuwa ni ya JK.
Mwaka 2009 JK alifika Mugumu Serengeti,ilikuwa ufunguzi wa Hotel ya Bilila.Kituko cha kwanza kufanya ilikuwa kumfukuza mkuu wa mkoa ambae alihudhuria hafla hiyo as if ilikuwa dhifa ya kitaifa.Akatolewa balu,kwamba akaendelee na majukumu ya kitaifa.

Wangoreme ni kabila dogo mkoani Mara,ila ni kati ya makabila giant wilayani serengeti ukiacha wakurya.Waliposikia kuwa jk anakuja Mugumu wakateua wazee wanane wakaonane nae ili wamweleze matatizo ya mwangoreme.Baada ya kumweleza wakawa na maswali yafuatayo:

1.Katika uteuzi wako wa wakuu wa mikoa na wilaya na nafasi nyingine kitaifa,wangoreme umeamua kututupa(kwa maana ya kwamba hakuna mongoreme hata mmoja aliyeteuliwa),je ni kwasababu hatufai?

2.Tulikuwa na mtu mmoja kutoka Ngoreme aliyekuwa mkuu wa wilaya(ni Dr. Deogratius Mwita-alikuwa mkuu wa wilaya ya Kilombelo enzi za Mkapa),ndiye peke yake katika kabila letu aliyekuwa na wadhifa wa juu.Ulipoingia madarakani badala ya kumpandisha,ukamvua ukuu wa wilaya bila kutupatia mwingine,ni kwanini?

2.Tulikusikia ukikemea habari ya kuchanganya biashara na siasa,je Hotel ya Bilila sio biashara?

Majibu yake kufuatia mpagilo wa maswali ni kama ifuatavyo:

1.Hakuna kabila lisilofaa,isipokuwa nafasi ni chache.

2.Mnishukuru saana kwa kumwondoa mtu yule katika nafasi ya ukuu wa wilaya,ningemuacha wananchi wangemmaliza.Nilipokea malalamiko mengi sana ya kwamba anatembea na wanafunzi wa Sekondari,hivyo kumwondoa ilikuwa ni heshima kwake,kwa serikali na hata kwenu ninyi Wangoreme.

3.Nadhani mngenishukuru kwa kuwekeza Tanzania na hasa Serengeti,kwani vijana wetu watapata ajira.Hii ni bora sana kuliko wale wanaokwenda kuwekeza nje,maana wanajenga uchumi wa mataifa mengine.

Kwakua hoja yangu ilihusu Bilila,je hayo ni majibu sahihi ya swali aliloulizwa?
Na je anaekataa kuwa BILILA si ya JK anaona hayo majibu? na unasemaje?
 
wanyancha alikuwa anahonga wapiga kura
Sana,hata mimi alitaka kunipa elfu 80,nikakataa kwa sababu zifuatazo, kwanza sihongeki mimi,maana najua nani anafaa.Pili hata kama ningekuwa nahongeka, I could not be cheap as such. Nikamkatalia,mtu mmoja anaitwa Shaweshi,ni mtendaji kata ya Mbalibali akaniambia niondoke maeneo yale kwakuwa jamaa ni mtu wa visasi anaweza kuni-ulimboka.
 
Mungeendelea na Dr Wanyancha saa hii jimbo la Serengeti lingekuwa na waziri kamili. JK alishamkubali huyu jamaa. Sasa huyu Kebhwee....Ah, sijui. Wangoreme punguzeni ukabila, fitna na visasi. Mkoa ule una makabila matatu tu, Wakurya, Wajita na Wajaluo. Dr Wanyancha alipita wakati ule kwa sababu ya kupambana Mongoreme dhaifu sana wakati ule.
Naomba nikusahihishe kidogo, mkoa wa Mara ndo mkoa unaoongoza kwa kuwa na makabila mengi sana kuliko mkoa wowote wa Tanzania, mkoa una makabila yafuatayo ambayo ninayakumbuka, kuna Wakurya, Wangoreme, Waikizu, Wanatta, Waisenye, Waikoma, Wajita, Wajaluo. Mbali na hilo kusema ukweli mpaka sasa mimi sijui kitu gani kiliwaroga mpaka wakampa ubunge Dr Kebwe yaani huyu jamaaaa anyway ya Mungu ni mengi sana na riziki hupangwa na Mungu sie wanadamu tutapambana we but at the end of the day Mungu ndo mtoaji wa yote
 
Singita ndo VIP, JK huwa anapumzika pale.P ale ndo kwa mara ya kwanza nilisika Human Resources Manager analipwa milioni 17 kwa mwezi.amazing!

Kitu SINGITA
Sasakwa9.jpg

Sasakwa2.jpg

Mkuu Hii kitu ni Balaa kweli, inatisha sana na sisi Wabongo wa Kawaida tunaweza Kufa bila kukanyaga Pale
 
Mungeendelea na Dr Wanyancha saa hii jimbo la Serengeti lingekuwa na waziri kamili. JK alishamkubali huyu jamaa. Sasa huyu Kebhwee....Ah, sijui. Wangoreme punguzeni ukabila, fitna na visasi. Mkoa ule una makabila matatu tu, Wakurya, Wajita na Wajaluo. Dr Wanyancha alipita wakati ule kwa sababu ya kupambana Mongoreme dhaifu sana wakati ule.

Humjui Mosena Nyambabe wewe, utakuwa umesimuliwa. Muulize hata James Mbatia wa NCCR Mageuzi waliyekuwa naye UDSM na kufukuzwa chuo miaka ile ya early 90s wakati wa vuguvugu la mageuzi nchini.
Baada ya hapo utafute japo speech zake akiwa kwenye majukwaa utaipata vizuri habari yake.
 
Mkuu ni kweli Ile ni Mwisho wa Matatizo nazani kwa Africa inaweza kuwa No 1

Acha chumvi hizo wewe ndugu yangu kwenye lile pori na yule mama HR na ile timu yake ya wanawake wa HR Walivofrustrated ndo kweli analipwa 17 sasa na MD wao atakuwa analipwa sh ngapi.Usiwapeleke mbali hivo, mishahara mizuri wanalipwa makaburu ambao ndo mameneja wa lodges na camp zote waafrica wa pale ni mburula tu hawana lolote ni wa kawaida sana
 
Mkuu ni kweli Ile ni Mwisho wa Matatizo nazani kwa Africa inaweza kuwa No 1
Bwana shacha,pale wanafanya booking ya vyumba mwezi january tu,hadi tena january.Ukimwona jk anakwenda pale ujue booking alifanyiwa january.Mwaka 2008,kulala pale siku moja ilikuwa 1.5 mil.Sijajua kwa sasa.Cheza weye na jk.
 
Acha chumvi hizo wewe ndugu yangu kwenye lile pori na yule mama HR na ile timu yake ya wanawake wa HR Walivofrustrated ndo kweli analipwa 17 sasa na MD wao atakuwa analipwa sh ngapi.Usiwapeleke mbali hivo, mishahara mizuri wanalipwa makaburu ambao ndo mameneja wa lodges na camp zote waafrica wa pale ni mburula tu hawana lolote ni wa kawaida sana

Mkuu hebu Rudi Nyuma, mimi sijaongea hiyo ya Milioni 17 Ila ni mesapoti kwamba ni Hoteli ya Ukweli, hayo ya milioni 17 mimi siyajui kabisa
 
Acha chumvi hizo wewe ndugu yangu kwenye lile pori na yule mama HR na ile timu yake ya wanawake wa HR Walivofrustrated ndo kweli analipwa 17 sasa na MD wao atakuwa analipwa sh ngapi.Usiwapeleke mbali hivo, mishahara mizuri wanalipwa makaburu ambao ndo mameneja wa lodges na camp zote waafrica wa pale ni mburula tu hawana lolote ni wa kawaida sana
Nimefanyia research pale Mugumu,miongoni mwa maswli yangu kwa watumishi wa serikali na makampuni lilikuwa"unalipwa kiasi gani kama mshahara "Hilo la milioni 17 ndo nilipata kutoka kwa yule mama. Lakini pia wale watu wanaonekana wako njema,wafanyakazi hawajachoka kama kwenye kampuni nyingine.
 
Back
Top Bottom