JK agoma kusaini sheria mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK agoma kusaini sheria mpya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ng'wanza Madaso, Apr 15, 2010.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  *NI YA KAMPUNI ZA SIMU KUJISAJILI SOKO LA HISA DAR

  Ramadhan Semtawa

  BAADA ya kusaini Sheria ya gharama za uchaguzi ambayo imegubikwa na utata, Rais Jakaya Kikwete ameshtuka na amegoma kusaini sheria inayobana makampuni ya elektroniki ikiwemo ya simu na posta kujisajili kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

  Habari za uhakikika zimelidokeza gazeti hili jana kuwa Rais Kikwete alikataa kusaini sheria hiyo akitaka Muswada wake ufanyiwe marekibisho katika kifungu cha 26 ambacho pamoja na mambo mengine, kinabana makampuni ya simu kujisajili DSE kwa lazima.

  Kifungu hicho tayari kilipingwa na kampuni za simu nchini wakati mjadala huo ukijadiliwa kwenye mkutano wa 18 wa bunge mjini Dodoma, ambako walitaka kilegezwe.


  Said Arfi ambaye ni msemaji wa kambi ya upinzani katika mambo ya mawasiliano, sayansi na teknolojia akisoma maoni ya kamati, alipinga vifungu mbalimbali vya muswada huo, kikiwemo kifungu cha 26.

  Upinzani huo wa kambi ya upinzani na kampuni za simu, unaelezwa na chanzo hicho cha habari kwamba ulikuwa na nguvu ya hoja ambazo zimemshwawishi Rais Kikwete kugoma kufanya kazi yake ya kikatiba ya kusaini sheria hiyo ili ianze kufanyakazi.

  Hata hivyo, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Peter Msolla alipoulizwa kuhusu hatua hiyo ya Rais, alijibu kwa kifupi: "Sijapata taarifa hizo, lakini pia Rais halazimishwi kusaini au kutosaini muswada wa sheria."


  Chanzo cha habari kilifafanua kwamba, Rais ameona ni vema serikali iweke mazingira mazuri ya kuvutia wawekezaji kuwekeza hisa DSE na si kulazimisha kama kifungu cha muswada huo kilivyokuwa kikisisitiza.


  "Rais amekataa kusaini sheria hiyo na itarudishwa bungeni ili ifanyiwe marekebisho. Serikali imeleta mapendekezo ya kubadili section (kifungu) ya 26, its a blow to bunge and Msolla (Ni pigo kwa Bunge na Msolla)," kiliweka bayana chanzo hicho cha kuaminika.

  “Kwa mujibu wa taarifa hizo huru, inachopaswa kufanya serikali ni kuweka mazingira mazuri ya kuvutia wawekezaji na si kuwalizimisha,” kilisema chanzo hicho.

  Chanzo hicho huru kilisisitiza kwamba: "Economically you don't force to list but you provide incentive to list (Kiuchumi, huwezi kulazimisha kusajili bali unaweka mazingira ya kuvutia watu wajisajili".


  Sheria hiyo, pamoja na mambo mengine ulikuwa ukitoa nafasi pia kwa kampuni za simu kutumia miundombinu ya pamoja katika kupitishia na kutoa huduma za mawasiliano.


  Lengo la mpango huo lilikuwa ni kupunguza athari za wingi wa minara hivyo kuweza hata kusababisha mwingiliano wa masafa na hivyo kuleta athari kwa binadamu.


  Kampuni kubwa za simu nchini ni Vodacom, TTCL, Zain, Tigo na Zantel huku kampuni nyingine zikichupuka kwa kasi kama vile, Benson Informatics (BoL), Six Telecoms. Pia kuna kampuni zingine zinahusu huduma za kiposta.


  Tangu kuingia madarakani Rais Kikwete, amesaini sheria mbalimbali nyeti ikiwemo ile ya Kudhibiti wanaoeneza virusi vya Ukimwi kwa nguvu, Sheria ya Takukuru ya mwaka 2007, Kuzuia Fedha chafu ya mwaka 2007 na Kitengo cha Kuzuia Fedha chafu (FIU).


  Hata hivyo, kati ya sheria zote hizo, Sheria ya gharama za uchaguzi imemuweka katika wakati mgumu baada ya Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa, kuibua tuhuma akisema kifungu kinachohusu idadi ya wapambe wa uchaguzi kilichomekwa nje ya bunge na Rais akasaini bila kujua.


  Source: Mwananchi
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Apr 15, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  Hawa watu wana matatizo.. Rais analazimishwa kusaini mswada unaoletwa kwake, na akikataa mara tatu.. Bunge linavunjwa na yeye mwenyewe kupoteza Urais.. hawa watu wana matatizo gani?
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Lakini ni vyema rais kuwa mwangalifu kuliko kukurupuka na sasa itakuwa vizuri kuwa kumbe maoni ya wachache kama yanamashiko ni bora kuliko ya wengi yenye ushabiki tu, si mda tena wa kudharau kila maoni ya upinzani na kuangalia uchache wao kuliko hoja za msingi kwa maslahi ya nchi, imejionyesha katika kadhia hizi kuwa wingi wa wenzetu bungeni ni kama wingi wa kunguru kwenye mti, kelele nyingi tu, pakidata kila mmoja anasalimisha ubawa wake kwa njia yake.
   
 4. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kwa uelewa wangu mdogo, naamini mchakato wa kuandaa sheria yoyote ni mrefu na unahusisha wadau wengi likiwemo bunge kabla ya kupelekwa kwa Rais kwa ajili ya kusaini. Katika nchi yenye watawala na watendaji makini ni nadra sana jambo linalotakiwa kupelekwa kwa Rais aidha kwa kusaini ama kujadiliwa kama ushauri jambo likawasilishwa likiwa na mapungufu fulani kwani linafanyiwa kazi na wataalam wa fani husika.

  Kwa jinsi hali ilivyo kwa sasa hapa Tanzania, naona hata wataalam katika fani mbalimbali wamekata tamaa na kukosa ari ya kufanya kazi kwa sababu watawala wetu wamekuwa legelege na wanajali siasa zaidi badala ya kuangalia mustakabali mzima wa Taifa letu. Mchumi anaposhauri jambo la ukweli kuhusu mwenendo wa uchumi anakemewa kwa kuambiwa ushauri wake utaleta picha mbaya kwa wananchi kuhusu serikali yao, hali kadhalika mhandisi, mwanasheria na wengineo katika fani zao. Kwa hali ilivyo kwa sasa Tanzania kila jambo linafanywa kwa kulipua na hakuna umakini. Rais anaposhauriwa vibaya tunategemea yeye kama Rais achukue hatua kali kwa wale waliomshauri lakini kwa JK ni tofauti na naamini wataendelea kumpeleka njia ya mbigiri kwa kila jambo.
   
 5. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Na imani hili litakuwa fundisho kwa Serikali na watendaji wake kwa ujumla.
   
 6. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,934
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  binafsi nilishangaa sana sheria hii kupita bungeni kama ilivyo. In a way ilikuwa ni sheria ya kibaguzi na kishabiki zaidi kuliko uhalisia wa kiuchumi. Sina hakika kama katika mchakato wa kuandaa sheria hii waliwahusisha mamlaka ya mitaji (CMSA - Capital Markets and Securities Authority), maana sioni ni vipi wangeiacha ipite na kwenda mpaka kwa Rais kama ilivyo. Sijui tumerogwa na nani!
   
Loading...