bulama
JF-Expert Member
- Dec 13, 2012
- 561
- 135
Bukoba. Rais Jakaya Kikwete amewaagiza Mbunge wa Bukoba Mjini (CCM), Balozi Khamis Kagasheki na Meya wa Manispaa hiyo, Anatory Aman kumaliza mara moja mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu kwenye manispaa hiyo ukiwahusisha.
Rais Kikwete alitoa agizo hilo alipokuwa akihitimisha ziara yake ya siku sita mkoani Kagera kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba.
Akihutubia mkutano huo, Rais Kikwete alimtaka Balozi Kagasheki ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii kuzungumza mgogoro huo na alipopanda jukwaani alisema miradi iliyopangwa kutekelezwa na Manispaa ya Bukoba chini ya meya huyo haiko wazi, inawaumiza wananchi na ina harufu ya ufisadi.
Alisema kulikuwa na mgawo wa viwanja vilivyokuwa vitolewe kwa wananchi na walikuwa wamelipia fedha kwa ajili hiyo, lakini havikuwahi kutolewa. Alisema kuna viwanja 5,000 lakini havijatolewa mpaka sasa.
Hata hivyo, Rais Kikwete alisema haoni sababu ya wawili hao kuendelea kulumbana na kusema kinachotakiwa ni kukaa pamoja kupima viwanja vilivyopo na utaratibu wa kugawa uendelee.
Ugawaji viwanja uendelee, kila mwenye kustahili apewe na ambaye hakuridhika ana nafasi ya kukata rufani... hakuna sababu ya kuendelea kulumbana, alisema Rais.
Mgogoro kati ya Meya Amani na Balozi Kagasheki, ulianza baada ya Manispaa ya Bukoba kuanza kutekeleza miradi mbalimbali ikiwamo ya ujenzi wa soko la kisasa, kituo cha mabasi na upimaji wa viwanja 5,000.
Mapema Machi mwaka huu, CCM, kupitia kwa Katibu wake wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kilitolea tamko mgogoro huo na kusema hauna tija na badala yake, unarudisha nyuma jitihada za kuimarisha chama.
Nnauye, aliwataka wakazi wa Manispaa ya Bukoba kuendelea na shughuli zao zikiwamo za miradi ya maendeleo.'Mwananchi' Kwa jinsi tulivyoteseka na upuuzi wa hawa akina kagasheki alitakiwa kutoka na suluhu. Kwani alichisema hakina tofauti na aliyosema nape sasa yupi ni bisi na ninani anachukua amri?CCM ni majanga.