Jizuieni kupiga simu hovyo hovyo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jizuieni kupiga simu hovyo hovyo

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Lukolo, Nov 25, 2010.

 1. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #1
  Nov 25, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Nawakumbusha vijana mkumbuke kujilinda ili muendelee kuishi. Nimewahi kuwaeleza vijana wajizuie kupiga, wakijifanya gonga gonga watakuzika, wanakusahau.

  Hata kama una salio la kutosha jizuie kupiga, usione noma kutuma SMS, acha sifa za kijinga kujifanya kijogoo wakati unajimaliza, acha kujiangamiza.

  Zitunzeni simu zenu , ni muhimu kwa maisha yenu na Tanzania kwa ujumla, msipende kupiga piga, gharama yake ni kubwa kwenu na kwa taifa hili.

  Kama ikibidi upige hakikisha simu yako iko kwenye kipochi, jifanye dereva wa pikipiki anayeheshimu sheria za usalama barabarani, haendeshi pikipiki bila helmeti ili hata akipata ajali asiumie kichwani.

  Ikibidi kupiga kumbuka usalama wa maisha yako, usipige nanihii kwenda nanihii, ni hatari, unashauriwa kutopiga ule mtandao unaoaminika kuwa ni wa gharama nafuu, inaweza kuharibu kabisa mfumo wa mawasiliano ya simu yako.

  Naamini simu yako inafanya kazi vizuri na una hamu angalau ya kubeep, hii nayo ni hatari, wengine ukibeep tu wanapokea, hawana longolongo, wanasema wapo kibiashara zaidi.

  Kutokupiga si ujinga, jambo la msingi si kupiga ila unachokiongea, na kumbuka kwamba, jambo la msingi ni mawasiliano, ukijali ufahari hiyo ni juu yako, simu ni simu tu, madhumuni yake yanafanana.

  Usidanganyike na simu kuwa eti ina kamera au double-skrini. Hizo ni mbwembwe tu. Kuna simu nyingi sana feki siku hizi zinauzwa zimevishwa vifuniko vipya, usidanganyike mwanangu, usikimbilie samaki wabichi bila kuuliza wamevuliwa wapi, bila shaka ‘umenisoma', nawasilisha.

  Makala: Habarileo
   
 2. GFM

  GFM JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Very educational................. asante................ haya masikia sasa nayasikie!
   
 3. T

  Tunga Member

  #3
  Nov 25, 2010
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  imetulia nadhani ujumbe umefika bila mawimbi..............
   
 4. Iteitei Lya Kitee

  Iteitei Lya Kitee JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2010
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 589
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Very creative
   
 5. Iteitei Lya Kitee

  Iteitei Lya Kitee JF-Expert Member

  #5
  Nov 26, 2010
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 589
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Does it have second meaning or just one meaning?
   
 6. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #6
  Nov 26, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Wengine kupiga mpaka chaji inaisha ndo hobby zao...
   
 7. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #7
  Nov 26, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Duh...! Nilijua ni taarifa kutoka TCRA....! Anyway, ujumbe umefika....!
   
 8. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #8
  Nov 26, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Mimi nikikupigia kuna tatizo?
   
 9. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #9
  Nov 26, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  tULOKULA fASIHI...MAUDHUI TUSHAZOA!!
   
 10. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #10
  Nov 26, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  I guess there is only one meaning. The only one you know. Just take and implement it.
   
 11. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #11
  Nov 26, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Duh, hiyo inakuwaje tena? Sijawahi kusikia kama chaji huwa inaisha
   
 12. Gobegobe

  Gobegobe JF-Expert Member

  #12
  Nov 26, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 245
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Asantle Lukolo, umesomeka. Hii ndo lugha ya picha ee?
   
 13. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #13
  Nov 26, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  A wonderful msg to all, ahsante kwa reminder...
   
Loading...