Jiwe la Tawi la Kingstone CDM lavunjwa-Morogoro

Jiwe la Tawi la Kingstone CDM lavunjwa-Morogoro

Shembago

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2011
Posts
332
Reaction score
50
Lile jiwe la Tawi la Kingstone ambalo lilifunguliwa na Mheshimiwa mchungaji Msigwa na kwa maandamano zaidi ya vijana 700 katika kata ya Boma -Morogoro usiku wa kuamkia leo limevunjwa.

Ikumbukwe tangu wakati kamanda mhandisi Samwel Msagati agombee udiwani wa Kata hii nyeti katika manispaa hii ambapo alipambana na naibu meya kwa wakati ule ambapo sasa ndiye Meya wa manispaa ya Morogoro kumekuwa na mwamko mkubwa katika kata hiyo ambapo Vijana kwa wazee wanaendelea kusema bye bye kwa Magamba. Mambo hayo yamekuwa yakimtisha sana Meya amabye ndiye Diwani wa kata hii ya Boma,ambapo alishatishia kuvunja jiwe hili la utambulisho wa Tawi na pia hata Viongozi wa kata ya Boma mnamo mapema mwaka huu waliitwa na ofisa Mtendaji wa kata na kuambiwa walitoe lile jiwe pale eti CDM hawakufuata utaratibu wakati wanajenga,alipoulizwa alete huo utaratibu ambao CCM wanaufuata ili wao pia wafate Mtendaji alishindwa kutoa na kukiri kwamba yeye anafata maagizo ya Diwani ambaye ndiye huyu Meya.

Ikumbukwe pia huyu huyu Meya kwa kumtumia mkurugenzi alishawahi kutoa Tangazo ambalo lilihusu kutopeperusha Bendera katika maeneo ya wazi na makzi ya watu eti kwakuwa kuna watu ambao hawana itikadi!!! tangazo hilo lilijibiwa na CDM wilaya na Kupuuzwa.

Inashangaza kuona Kiongozi huyu anashindwa hata kutii katiba, maana katiba ibara 146(2)(C) inaelekeza kwamba mamlaka ya serikali ya mitaa itaimarisha demokrasia katika eneo lake na kuitumia demokrasia kuharakisha maendeleo ya wananchi.Kiongozi huyu ambaye anashindwa kusimamia katiba tumfanyaje?

Asante,
 
ni kutokumpa nafasi tena ya yeye kuwa kiongozi kwa sababu hata hyo nafasi aliyo nayo anayo kwa mapenzi ya watu wachache siyo walio wengi na kikubwa zaidi ni rushwa ndiyo iliyomuweka madarakani
 
Hawajaskia kuna moto wa ajabu Znz?? Shauri yao wavunjaji.
 
Mkoloni Mweusi (ccm) ni hatari kuliko mkoloni mzungu aliyepambana baba yetu (Mwalim Nyerere). Mkoloni ccm akiua anaunda tume yake kujichunguza!lol.
 
Kiongozi dhaifu utumia udhaifu wake akifikiri utadhaifisha wasio dhaifu. "bye bye shishiem''
 
ccm hamnazo kwelikweli.

awajajuwa tu kama hivyo vitendo ndo vinaongeza chuki ya wananchi dhidi ya chama chao.

we're stronger than ever.
 
Kuna haja ya CHADEMA sasa kuzindua operation ya kupeperusha bendera nchi nzima, maana CCM wanachukia na kuziogopa bendera za CHADEMA kama moto.

Nashauri viongozi wa CHADEMA kuhakikisha bendera zinapatikana kwa wingi na kuhamasisha ili kila mpenda mageuzi aweze kuzipeperusha juu ya mali yake iwe Ukuta, paa, kibanda, nyumba, miti, biashara, Gari, Ofisi, Baiskeli, Pikipiki nk.
 
Wameshikwa pabaya pale moro sasa wanaanza kutapatapa.

Chezea peoples power weye.............................................!
 
Mfa maji haishi kutapatapa. So huyo meya kona ugali unaenda ukingoni so lazima ajitetee.
KWA PAMOJA TUNAONDOA CCM MADARAKANI.
 
Mfa maji haishi kutapatapa. So huyo meya kona ugali unaenda ukingoni so lazima ajitetee.
KWA PAMOJA TUNAONDOA CCM MADARAKANI.

Mkuu bachani, mimi moyoni mwangu nilishaiondoa madarakani siku nyingi! sana sana ninachokiona hapa tz. ni ukoloni wa ccm ambao watanzania woote shime tungane kuuondoa, reja kurithishana uongozi kwa watoto wa vigogo UVCCM.
 
Morogoro inasadikiwa kuwa ni ngome kuu ya CCM, sasa kama inatetereka basi huko kwingine kutakuwa kumeshateketea.
 
Watavunja jiwe la tawi 2, let them try kuitoa mioyoni
 
Kama ni vijiwe watavunja sana, lakini hawatofanikiwa kuvunja mioyo ya wananchi.
Huku ukonga kata ya majohe walivunja kijiwe, wakachukua bendera na kumshitaki aliyetoa eneo la kujenga kijiwe lakini the next day wajumbe wa mashina kiasi cha 15 wakahamia Chadema.
 
Duh! Mbinu zao chafu kama hizo hazitakwamisha mabadiliko,wamefunga uwanja wa NMC Arusha lakini CCM wajue kuwa Ukimpiga chura teke unampunguzia urefu wa Safari. Na mkuki haupigwi ngumi pia Shimo la panya halizibwi kwa mkate.
 
Kuna haja ya CHADEMA sasa kuzindua operation ya kupeperusha bendera nchi nzima, maana CCM wanachukia na kuziogopa bendera za CHADEMA kama moto.

Nashauri viongozi wa CHADEMA kuhakikisha bendera zinapatikana kwa wingi na kuhamasisha ili kila mpenda mageuzi aweze kuzipeperusha juu ya mali yake iwe Ukuta, paa, kibanda, nyumba, miti, biashara, Gari, Ofisi, Baiskeli, Pikipiki nk.

Kuna kitu kinanifurahisha hapo mji kasoro bahari. Pale stendi ya daladala mjini kuna bango lina tangazo la benki fulani. Lakini juu kabisa ya bango hilo kuna bendera ya CDM.
 
Huyo anajaribu na hotoweza kushindana nasaut yaweng inshot ata aibika na atashindwa yetu macho namuhurumia sanaa
 
Back
Top Bottom