Galadudu
JF-Expert Member
- Jun 23, 2014
- 2,304
- 780
Jirani yangu mmoja ambae tunafahamiana lakini sio marafiki, kanivamia tu jioni hii na kuanzakuniporomoshea mvua ya matusi makali huku akiwa na tuhuma nzito za kwamba natembea na mke wake.
Kisa kilianzia siku ya valentine katoka kwenye starehe zake alikuwa kamuacha mkewe nyumbani, na mi ndio nilikuwa narudi home mida hiyo ya saa 6 usiku na mimi wife hakuwepo alikuwa kaenda kumuuguza bibi yake jamaa akamkuta mkewe anaongea na mtu kwenye simu kusema ule ukweli ckuwa mimi.
Jamaa akaanza kumsakama kwa maneno makali yaliyoishia kutoa kipigo kwa mwanadada, ktk harakati za kujiokoa akapata upenyo akakwapua khanga akatimua mbio, hakufika mbali mbele tu ya nyumbani jamaa likamkamata tena kipigo kikaendelea huku linasema 'kwa hiyo ndio umekimbilia huku kwa hawara yako.
Sasa nakupiga mbele yake tuone atafanya nini'jamaa alikuwa haongopi na kweli kipigo kikaendelea hapo mi sikushtukia kuwa hawara yake ni nani sasa maana mi sijawahi kuwa na mazowea yeyote na huyo dada zaidi ya salamu uswahilini hakuna dogo watu wakajaa na wengine wakitumia busara kutoa suluhu ya ule ugomvi.
Nakumbuka jumapili moja baada ya lile songombingo ndio nikakutana na yule Dada (nae ni mzuri kwa kweli, hana haya mambo ya kujichubua uso kwa madawa ya kuusaka weupe wala kuweka marangi rangi ya mdomoni, kwenye nywele wala nini ndio akanimwagia mzigo wote kwamba kumbe mtuhumiwa wa ile kesi na nyinginezo nyingi zinazotokea ndani na kumalizwa kimyakimya ni mimi.
Nikabaki nashangaa, lakini akanipa angalizo lililoniacha na viulizo eti 'kwa hiyo kazi ni kwako'.Leo ndio ivo jamaa kajitoa ufahamu akanivaa mzima mzima kuja kunipa makavu live tena akiwa na mke wake amesimama pembeni dada wa watu huku uso umemsinyaa kwa aibu.