jirani yangu huyu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

jirani yangu huyu

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by BADILI TABIA, Apr 7, 2012.

 1. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #1
  Apr 7, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  yaani hapa nimenuna kweli kwelì!

  Baada ya kusaka usingizi muda mrefu ulipoanza kukolea jirani yangu amerudi!

  Na usingizi wangu umekata!
  Jirani huyu sijui amefunga spika za matangazo kwenye gari yake? Au ana matatizo ya kusikia? Anafungulia mziki mnene mpaka roho inadunda. Ingawa tunatenganishwa na barabara maana nyumba zetu zinatizamana lakini toka jumatatu hadi ijumaa ikifika saa saba usiku yeye ndo anarudi,weekend mwendo wa saa tisa au kumi!

  Tatizo kwa mziki wake lazima niamke. Na huchukua takriban dakika 2-5 kumfungulia geti.

  Yaani ndo mateso nipatayo. Nimeamka usingizi umekata! Sijafanikiwa kuongea nae maana daily simpati,labda nimvizie usiku wa manane.

  Mnikopeshe usingizi jamani
   
 2. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #2
  Apr 7, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Mfate sa'ivi umweleze dukuduku lako.
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Apr 7, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  naogopa kutoka nje usiku. Ingawa ni wazo zuri,
   
 4. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  BT pole sana Mazee, kuishi na watu kazi !
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  Apr 7, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  asante mkuu. Tena sio kazi ndogo. Hapa inabidi nisake upya usingizi!
   
 6. ULUMI

  ULUMI Member

  #6
  Apr 7, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hama mahali hapo mwachie starehe zake!
   
 7. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #7
  Apr 7, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  nikapange? Wakati na jiminya kutafuta hela ya kodi na nyumba si nitakuwa bado nateseka?
   
 8. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #8
  Apr 7, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  tena ya hitaji uvumilivu wa hali ya juu..
   
 9. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #9
  Apr 7, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kareport hiyo abuse kwa mjumbe wenu ili apigwe ban ya kufungulia mziki usiku ni hayo tu maushauri ya haraka..
   
 10. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #10
  Apr 7, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  good idea. Mjumbe anaweza kumsaka akampata....nitareport kwake


   
 11. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #11
  Apr 7, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Ha ha haaaaa!!! Kwa nini uteseke mkuu?? Hujui kuwa nimefungua duka la usingizi hapo mitaa ya Kariakoo??? Usisubiri hadi macho yaning'inie. Njoo ujipatie usingizi kwa bei nafuu kabisa sawa na bure. "Akwambiaye usikombe mboga, ujue anatala ushibe.
   
 12. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #12
  Apr 7, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  HAhhaaaa kilo moja ya usingizi bei gani?


   
Loading...