Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 617
Ufisadi wa 255m/-Bodi ya Tumbaku.
Ni kwamba,
Tanzania Tobacco Board TTB, yenye makao makuu yake Morogoro, iko chini ya Wizara ya Kilimo. Kwa kawaida, TTB ina utaratibu wa kuweka Bank kama Ficed Deposit 200m/- ili faida inayopatikana kila mwaka iwe inatumika kulipia viinua mgongo vya wafanyakazi wanaostaafu.
Hiyo imekuwa ni desturi ya miaka yote. Wakurugenzi wote waliokuja na kuondoka waliuacha utaratibu huo ukiendelea kutumika.Lakini Mkurugenzi wa sasa Bw Wilfred P.Mushi amekuwa ni jipu tangu alipoingia TTB mwaka 2012.
Mpaka wakati huu amefanikiwa kuzitafuna pesa hizo ambazo endapo zisingeguswa, zingekuwa zimefikia 255m/-.Wakati huo huo, kufikia January mwaka huu jumla ya wastaafu 7 wanaidai bodi hiyo jumla ya 86m/-.
Amezitumiaje? Huko tutafika. Ngoja tuanze na ujio wake pale TTB.
Mkurugenzi huyu aliingia TTB pasipo sifa stahiki kulingana na scheme of Service ya Mwaka 2012, inayomtaka Mkurugenzi Mkuu awe na uzoefu wa miaka 12 kwenye nafasi ya maamuzi, 6 kati ya hiyo iwe kwenye sekta ndogo ya tumbaku.
"He must have 12 years of senior position, six of which should be in tobacco sub-sector" inasomeka sehemu ya scheme hiyo.
Hata hivyo, yeye aliletwa TTB na Waziri wa Kilimo wakati huo Christopher Chiza ambaye wameoa nyumba moja.
Mpaka wakati huu haijulikani amesomea nini na bado Bodi haijamthibitisha. Lakini uwepo wake TTB umekuwa na madhara madhara makubwa siyo tu kwa Bodi hiyo, bali na wadau mbalimbali wa tumbaku nchini.
Ubadhilifu/namna alivyozifuja 255m/-
1. Mishahara
Kwa mujibu wa Waraka wa Msajili wa Hazina, Mkurugenzi wa Tumbaku alipaswa kuanza na Mashahara wa 3.5m/-.Lakini yeye aliuona mdogo na akawa anajiongezea chajuu yaani 1.5m/- ili uweze kufikia 5m/- tangu wakati huo.
Madhara
Madhara ya uamuzi huo ni kwamba shughuli za maendeleo ya Bodi hiyo,yaani zao la tumbaku zimekuwa zikiathirika mfano usajili wa wakulima, upangaji madaraja za zao pamoja na mafunzo. Kwa kawaida, kila msimu wa kilimo, wataalam wa tumbaku hutakuwa kwenda vijijini na kusajili wakulima watakaolima zao kwa msimu huo.
Hao ndio husimamiwa na taratibu na kanuni zilizopo ili waweze kuzalisha zao bora. Halafu wakati wa ununuzi wa zao, maafisa wa bodi wanakuwepo kwenye masoko/minada ili kupanga madaraja ya zao ili wanunuzi wanunue.
Lakini kwa kukosekana fedha huko,wanunuzi wamejikuta wakishindwa kununua zao kwa wakati,huku Mkurugenzi akitafuna fedha zote,mpaka za O.C yaani Other charges.
2. Masurufu
Kulingana na maelekezo ya Msajili wa Hazina wakati huo, Mkurugenzi wa TTB alipaswa awe analipwa masurufu ya kiasi cha 80,000/- pale anapokuwa kwenye Miji na Majiji. Lakini pasipo kuomba kibali cha Msajili huyo, yeye alijipandishia masurufu hayo hadi kufikia 150,000/-.
Mpaka hapa unaweza kujua alikuwa anapata wapi pesa nyingine ya kujazia masurufu hayo. Na kwa mujibu wa logbook ya Kampuni hiyo, amekuwa ni mtu wa kusafiri sana hapa nchini. Kimsingi amekuwa anaishi zaidi Jijini Dar es Salaam akijilipa masurufu manono hayo.
3. Nyumba
Kulingana na taratibu za Msajili wa Hazina, Mkurugenzi wa TTB alipaswa kuwa analipwa 800,000/- kama kodi ya nyumba. Hata hivyo, TTB ina nyumba ya Mkurugenzi iliyopo Mkoani humo, ambamo ndipo wamekuwa wakiishi watangulizi wake na hivyo hawakuwa wanalipwa stahiki hiyo ya pesa.
Lakini cha ajabu, yeye alipoingia mabarakani alisema nyumba hiyo siyo ya viwango vyake na asingeweza kuishi humo. Hivyo aliamua kupanga nyumba ya thamani ya 25m/- kwa mwaka, akilipa kwa USD.
Lakini kama ilivyosemwa hapo awali, Mkurugenzi huyo wala haishi muda mwingi kwenye nyumba hiyo,maana muda mwingi yuko nyumbani kwake Dar es Salaam,huku akijilipa masurufu ya safari.
4. Ukabila/Upendeleo
Si tu kwamba anaendekeza ukabila, lakini ni dhahiri kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na Mwanasheria wa TTB anayeitwa Philmina Hubert. Ndiyo maana alimuajiri na kumpa kazi hapo. Lakini pia, alimteua aingie kwenye Bodi ya Kituo cha Utafiti wa Tumbaku, huku yeye siyo mwanataaluma ya Kilimo, hivyo kushindwa kuiwakilisha vyema bodi hiyo kwenyemijadala husika.
Hata uteuzi hui huo ulipopigwa Bodi hiyo, yeye aliwaandikia akiwataka wamkubali tu kwakuwa walipoomba jina hilo, hawakumpa vigezo ambatishi.
Hata kwenye Mikutano ya Kimataifa amekuwa akiwateua Wachagga wenzake ili wakaiwakilishe bodi, hata kama hawana ujuzi wa zao hilo. Wadau wa Tumbaku kusini mwa Afrika wana umoja wao wa kujadili maendeleo ya zao uitwao T5.Walipofanya mkutano wao kwanza Cape Town, yeye alihudhuria.
Huko pamoja na mambo mbalimbali ikiwemo kuongeza ubora wa zao, kuzingatia mazingira yanatunzwa,serikali husika zinasimamia uwazi na usimamizi wa kwenye vyama vya ushirika etc.
Cha ajabu kwenye mkutano uliofuata nchini Malawi, yeye hakuenda,badala yake akamtuma Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Mrs Mary Assey. Jambo hilo liliwashangaza sana wadau wa sekta nchini na huko mkutanoni Malawi.
5. Wajumbe wa Bodi
Mkurugenzi wa TTB ndiye mshauri wa Waziri wa Kilimo kuhusu namna ya kuwapata wajumbe wa Bodi. Kwa muundo wa bodi ulivyo, kunapaswa kuwa na wawakilishi kutoka kwenye makundi mbalimbali wakiwemo wanunuzi, wenye viwanda n.k
Tanzania ina viwanda vitatu vya tumbaku,viwili viko Morogoro na vinafanyakazi. Kimoja kiko Songea lakini hakifanyi kazi kwa zaidi ya miaka 15 sasa. Na nchini kuna makampuni ya tumbaku manne.
Mawili makubwa yana viwanda vyao ambavyo ni Alliance One na TLTC. Mengine Mawili ambayo ni madogo ni Premium Active Tanzania na na Japanese Tobacco International.
Lakini tangu aingie madarakani huyu, uwakilishi wenye viwanda kwenye bodi umekuwa ukitoka kwenye Kiwanda cha kilichokufa kule Songea! Halafu uwakilizi wa wanunuzi na Halmashauri ya Tumbaku umekuwa ikipewa kampuni moja tu ya Premium Active Tanzania! Ikitoa wajumbe wa Bodi wawili,yaani Mkurugenzi Mkuu wake Phillip Mainet na Mkurugenzi wake mwingine aitwaye Nick Louzos.
6. Uhusiano mbaya kati yake na Wadau
Wanamuita mtu wa suti muda wote. Haendi mashambani.Halijui zao na sijui kama yupo kwa ajili ya zao hilo kama ifuatavyo:-
· Hayupo karibu na wadau kama wakulima kupitia ushirika,wanunuzi wa tumbaku na hata watendaji wizarani
· Haelewi mipaka ya kazi yake ya kazi na hiyo hupelekea kufanya maamuzi yanayoshusha hadhi ya Bodi mbele ya wadau(barua imeambatanishwa inayovunja Halmashauri ya Tumbaku kinyume cha sheria namna alivyojibiwa na wizara.
· Sasa hivi anataka makampuni yaende kufanya kampeni vijijini ili kusajili wakulima, utaratibu ambao ulishapigwa marufuku miaka mingi iliyopita kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuongeza uhasimu baina ya wakulima pamoja na kumuongezea mkulima mzigo wa gharama
· Ameandika barua kwenda kwa Serikali ya China akitoa taarifa zisizo kweli kuwa nchi yetu itaweza kuzalisha kilo 250m kwa muda wa miaka 3 ijayo ikiwa ni sababu ya kuwavutia wachina,wakati si kweli.Hii inaonesha uwezo wake ni mdogo na hafahamu mwendendo wa uzalishaji na ukuaji wa tumbaku na soko la zao hilo duniani. Kwani hata nchi ya Zimbabwe inayoongoza Africa kwa uzalishaji wa zao hilo,haiwezi kufikia kiwango hicho cha uzalishaji kwa kipindi cha miaka 3 ijayo.
Madhara uwepo wake
· Ukuaji wa zao umedorora
· Wadau hawana imani naye
· Wawekezaji na wanunuzi wamenza kuondoka kwenye baadhi ya maeneo ikiwemo Songea
· Kwa miaka 3 sasa TTB imeshindwa kuwalipa kifuta jasho/kiinua mgongo wastaafu wanaoidai jumla ya 86m/- kwani zile pesa hazipo tena.Kulingana na Mkataba wao wa hiari, kila Mfanyakazi wa TTB anapaswa kulipwa kiwango cha 396,396/- kwa kila mwaka aliokuwa kazini mpaka kustaafu kwake.
Kulingana na hili, mmoja wa wastaafu wa TTB alienda kortini kudai haki yake ambapo alishinda kesi na iliamriwa alipwe 10m/- au mali za TTB zikamatwe. Kutokana na hilo gari aina la Landcruiser lenye namba za usajiri SU 36092 mali ya TTB lilikamatwa. Mstaafu huyo Aloyce Newa aliyekuwa dereva kabla ya kustaafu kwake alilipwa stahiki zake haraka ili kunusuru gari hilo kuzwa.