Uchaguzi 2020 Jipatie nakala yako ya Ilani ya CHADEMA na ACT-Wazalendo utagundua wasomi wapo

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Ilani ya Chama cha Mapinduzi naamini imeandikwa kwa maelekezo ya mtu au kikundi cha mtu akareflect kile anachokiwaza na siyo kile Watanzania wanataka.

Ilani ya CCM haina muda na maisha ya Watanzania, inazungumzia majadaraja na ndege unajiuliza biashara ya ndege ni wapi imewahi kuinua uchumi kwa manunuzi ya cash? Ndege ukopwa zikafanya biashara zikalipa deni na siyo kutumia fedha za wastaafu na wafanyakazi kununua ndege alafu ukawaacha wananchi wakishindwa kueleza familia zao.

Sera ya nchi yoyote lazima ianze na watu ifuate watu siyo ianze na vitu ifuate watu. Ukichelewesha maisha ya mtu kwa mwaka mmoja hautorudi Tena ila ndege ikinnunuliwa baada ya mwaka utapata nzuri zaidi.

Walioandika ilani za ACT-Wazalendo ambayo soon itakuwa mtaani na ya CHADEMA wameelewa utu na haki vinavyostawisha watu ambao wakistawi watafanya kazi na wakifanya kazi wataingiza Kodi na mapato yatakayotumika kununua ndege.

Corona imebeep tu shirika la ndege lipo hoi tukubali kushauriwa kuhusu viapaombele vya nchi tuna rasilimali nyingi tusijilinganishe na mfumo wa Rwanda na Ethiopia rasilimali zao ndo zinawafanya ndege ziwe kipaumbele.
 
Back
Top Bottom