Jinsi Ya Kuyahimili Mambo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi Ya Kuyahimili Mambo

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by X-PASTER, Mar 27, 2010.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Mar 27, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Jinsi Ya Kuyahimili Mambo Yasiyotarajiwa Katika Maisha Ya Ndoa

  Huwa unapata shida kuota ndoto za kumpata mwandani mwenye sifa unazozitaka. Lakini kinyume na ndoto zako yawezekana ukajikuta unaishi na mwenza ambaye halingani na ile picha iliyokuwa akilini mwako ambayo ulidumu nayo kwa miaka mingi.

  Ikiwa mwanandowa mwenzio ana upungufu kinyume na matarajio yako, si vizuri kumfanyia ukatili na kumfanya akose raha ya maisha ya ndoa au aone kuwa maisha ya ndoa ni machungu.

  Jaribu kurekebisha mambo kwa upole, uungwana na ucheshi kama ambavyo wewe ungependa wengine wakutendee pale unapokosea.

  Ni jambo jema zaidi kumpa majibu yako bila jazba. Jaribu kumuelimisha polepole, mueleze kwa utulivu na mpe heko pale mambo yanapokwenda sawa.

  Mara zote ukumbuke kuwa ni MwenyeziMungu Pekee Atakayekupa malipo unayostahiki kwa subira yako. Vyovyote mume atakavyostahamilia tabia mbaya ya mkewe atapewa malipo kama yale atakayoyapata Yaaqub (‘Alayhi salaam) na vyovyote mke atakavyovumilia tabia mbaya ya mumewe atapewa malipo sawa na yale ya Asia (mke mwema) wa Firauni.” (al-Ghazal)

  Kuna stratejia kadhaa zinazoweza kukusaidia kupunguza pengo la tofauti kati yako na mwandani wako. Nazo ni:

   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Mar 27, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kuweka Malengo na Mambo ya kipaumbele


  Isome vizuri aina ya tabia ya mwandani wako, huenda ukabaini labda yale matarajio uliyokuwa nayo wewe ni ya juu mno kiasi kwamba hakuna mwanamke wa kibinadamu anayeweza kuyafikiya.

  Hebu sasa wewe mwenyewe jitahidi kuwa mkweli katika kuyatathmini malengo yako na kuangalia yale mambo yenye umuhimu miongoni mwa yale unayoyataka.

  Kujenga tu matarajio kwa njozi zisizoweza kutekelezeka kwaweza kukuletea mfadhaiko. Mke kwa upande wake, anaweza kuishi bila kumtarajia mumewe kuwa tajiri au mtu wa mafanikio lakini bado akafurahi na familia yake.
  Wakati mwingine ni vigumu kufanikiwa kufanya jambo bila kujitowa muhanga ambao huigharimu familia. Kwa kutaka mke msomi au kwa ajili ya kuongeza kipato, mume huenda akamuhimiza mkewe atafute elimu au akafanye kazi nje ya nyumba yake.

  Lakini bado mume huyu anamtarajia mkewe afanye kazi kama mama wa nyumbani anayetumia muda wake wote na nguvu zake kwa ajili ya kazi za ndani ya nyumba.

  Changamoto halisi ni kuelewa mahitaji yako halisi na kuangalia mambo muhimu. Lazima utambuwe mambo ya kujitowa muhanga na mambo unayohitaji kuyafanyia marekebisho.

  Katika kuweka malengo na mambo ya kipaumbele, wandani lazima watafakari na kujali mahitaji ya kila mmoja wao. Katika kufanya maamuzi ili kufikia malengo yao lazima watambuwe upungufu unaoweza kuwepo katika kipengele kimoja kwa ajili ya tija katika kipengele.

  Tufuwate ile kanuni ya uhifadhi wa nishati ambayo inasema kuwa tunatumia kiasi cha nishati katika shamba jipya kwa kuchukua kiasi sawa na hicho cha nishati kutoka shamba jingine.

  Unapoziendea shughuli zako lazima ukumbuke kuwa familia yako ndiyo kipaumbele nambari moja katika orodha ya mambo muhimu kwani wajibu wako kama baba au mzazi ni wako peke yako. Hakuna mtu yeyote duniani atakayekaa badala yako.
   
 3. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #3
  Mar 27, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Stahamala na Ukarimu


  Pale hali fulani inapokuudhi, yumkini lawama na shutuma zisizo za haki huanza kukutoka, lazima uoneshe uvumilivu na ukarimu. Kumbuka usemi huu: “Muislamu wa kweli yuko kama ardhi: kila dhambi inatendwa juu yake lakini kile kilicho kizuri tu ndicho kinachotoka ardhini

  Mapenzi ya kweli sio kukasirika, sio kuona wivu, kutiliana shaka au kupagawa. Mambo haya ni ishara ya kutokuwepo kwa utulivu unaosababishwa na hali ya kudhaniana vibaya ambayo lazima ichukuliwe tahadhari.

  Huwa ni rahisi sana kuona makosa ya watu wengine lakini ni vigumu kuyakubali yale ya kwetu. Lakini tukiwa Waislamu wakweli lazima tujitahidi kujikosoa.

  Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam ) kasema; “Amebarikiwa yule anayejiangalia zaidi kasoro zake kiasi cha kutoona kasoro za wengine.
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Mar 27, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Pongezi na shukurani


  Ndivyo silika yetu ya kibinadamu ilivyo kushutumu mno udhaifu wa wandani wetu pale tunapopata fazaa, hasira au tunapochanganyikiwa, kwa sababu ya kutotimia kwa yale matarajio yetu.

  Unaposumbuliwa na hisia hizi mbaya, mkumbuke (Mdhukuru Allaah) na muombe Akukinge na Shaytwan ambaye hulifanya jambo duchu sana liwe kubwa na kuleta mlipuko mkubwa kupita kiasi na kukufutia mema yako ambayo ulifaidika nayo hapo kabla.

  Kumbuka kuwa huyo mwenza wako ni neema kutoka kwa Allaah ambayo lazima ushukuru kwayo. Kumbuka nasaha hizi za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa waumini wakati wanapokuwa na hisia za kufadhaishwa na wandani wao.
  “Mwanamume aliyeamini asimchukie kabisa mwanamke aliyeamini; Iwapo anachukizwa na tabia moja ya mkewe basi ataona sifa nyingine ya kumfurahisha.” (Muslim).
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Mar 27, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kuoneshana upendo na kuishi kwa mapenzi


  Hata kama utakuwa unampenda mwandani wako kiasi gani, iwapo hutalionesha pendo lako, mwenzio hatahisi kama unampenda. Hata kama unafurahishwa vipi na mwandani wako, kama huoneshi kufurahishwa, yeye hatahisi kama anafurahiwa.

  Hakuna mume wala mke mkamilifu lakini wandani wanapooneshana mapenzi na furaha na kuishi kwa kufuata misingi ya Uislamu, siyo tu watapendana kwa mapenzi na heshima bali pia watapendwa na Allaah.

  Magusano ya ziada huongeza zaidi uhusiano wenu wa ndoa na kukoleza huba ya kumfanya mwenza aongeze jitihada za kukuridhisha.

  Aidha zawadi ndogo ndogo ambazo zinaonesha jinsi unavyomjali hizi ni chachu za pendo, na zinasambaza mawimbi ya mapenzi mwilini mwa kila mmoja.

  Vilevile kula na kusali pamoja kwaimarisha mahusiano ya wanandoa. Usipuuze umuhimu wa chakula cha pamoja cha familia. Sufiyan ath-Thawri kasema; “Nimesikia kuwa MwenyeziMungu na Malaika Wake huipa baraka familia inayokula pamoja

  Ni jambo la kupendeza kusali nyuma ya kiongozi wa familia na kufanya naye ‘ibada pamoja. Hata hivyo mume-Imamu lazima azingatie mafundisho ya Mtume mwenyewe ambaye aliifanya swala ikidhi mahitaji na shida za jamaa iliyokuwa nyuma yake.

  “Mimi husimama kuswali kwa kisimamo kirefu lakini punde ninaposikia kilio cha mtoto naifupisha swala kwa kuchelea kuwa mama yake anaweza kudhikika”. (Bukhari na Muslim).
  Mbali na hayo, mambo mengine madogo sana kama haya yanaweza kukuleteeni kheri. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kasema, “hata kumlisha mkeo tonge la chakula mdomoni ni swadaka” (Bukhari na Muslim).

  Hii inaonesha aina ya ukarimu unaotakiwa kuwepo katika ndoa ya Muislam
   
 6. Sydney

  Sydney Senior Member

  #6
  Mar 27, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante sana kwa shule nzuri na jinsi ya kuhimili mambo katika maisha hasa maisha ya ndoa, nimesoma na kuelewa ingawa kuna baadhi ya majina na maelekezo mengine mimi yaliniacha pembeni maana iko zaidi katika "dini fulani" lakini haina neno ujumbe umeeleweka! Asante sana mimi nitayafanyia kazi niliyoona yatanifaa!
   
 7. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #7
  Mar 27, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  thread zako shwari ila tatizo lako ni font size kuwa ndogo mkuu!
   
 8. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #8
  Mar 27, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Inaweza ikatokea kuwa mwenzi wako kakosea na ukadhirisha kosa lake; mara nyingi tumekuwa wa kwanza kulaumu na kufikiria kutoa adhabu hili huwa ni kosa lako kubwa!

  Hata kama kosa limedhihirika na ni kubwa kiasi gani Binadamu na tunakumbushwa na Baba yetu Muumba kusamehe ....kama Baba yangu alivyowasameheni ninyi nanyi vivyo hivyo watendeeni wadeni wenu!

  Jitahidi sana huku ukimtanguliza Mungu wako kumsamehe mwenzi wako akikosa; tena pasipo kumhesabia makosa kwani si mahala pako wewe kutoa hukumu; hukumu inatolewa na yule aliyemuumba tu!
   
 9. Fisherscom

  Fisherscom JF-Expert Member

  #9
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,423
  Likes Received: 239
  Trophy Points: 160
  Ahsante sana mkuu kwa darasa,tumekuelewa na tutayafanyia kazi. Hakika Qur-an ni muongozo thabit kwa wamchao Mwenyezi Mungu. Maisha ya ndoa kwa ukamilifu wake yameelezwa ndani ya Qur-an na hakika tukiyatekeleza pamoja na kuzingatia hadith na sunna za Mtume Muhammad(S.A.W) tutaongoka na maisha yetu yatakuwa safi.
   
 10. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #10
  Mar 27, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Sawa ndugu yangu pale ambambo unaona kuwa hujaelewa unaweza kuniuliza na kukufafanulia Insha'Allah. Wewe chukuwa kile ambacho unaona ni mwafaka kwako, yale mengine tuwachie sisi.
   
 11. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #11
  Mar 27, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mkuu nitajitahidi kuongeza font size, ila kama unatumia Mozilla Firefox unaweza kuongeza font size kwa kubonyeza Alt pamoja na alama ya kujumlisha Alt plus (+).
   
 12. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #12
  Mar 27, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Masikini _Jeuri nashukuru kwa nyongeza yako muruwa.
   
 13. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #13
  Mar 27, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Well said mkuu.
   
Loading...