Peter Mwaihola
JF-Expert Member
- Jun 23, 2022
- 289
- 489
Usiwe mtu wa kuishi maisha na ndoto za wengine, vaa uhalisia wa maisha yako, vaa kiatu cha ndoto yako na uipambanie itakupunguzia msukumo wa mawazo ya kuwaza mambo yasiyokuhusu na yaliyo nje ya uwezo wako.
Ishi vizuri na kila mtu, wenye kukusema vibaya usipambane nao endelea kufanya mazuri ambayo yatawashawishi wakuone mtu bora zaidi ya jana. Usisahau kuwa Mungu hawezi kuruhusu jaribu ambalo hauwezi kulishinda.
Heshimu muda, panga mambo yako vizuri itakusaidia usichelewe kutekeleza malengo yako na kuepuka hofu ya kuwa nyuma ya wakati, hivyo kila jambo liwe na wakati wake.
Usiwe na matarajio makubwa kuliko juhudi zako, jibidishe kisha umuombe Mungu ndipo mafanikio yatakuja hata hivyo baada ya hayo usikose subira na uvumilivu.
Kila siku tambua kuwa baada ya Mungu na wazazi wako mtetezi na mpigania haki yako anayefuata ni wewe mwenyewe, hivyo jipe kipaumbele katika kujipambania wengine wafuate baadae kukupa msaada.
"Huenda wewe sio mkubwa kwa macho lakini ukubwa wako upo kwenye ndoto yako ukisimama imara utang'ara mbeleni"
[emoji2398] Peter Mwaihola