Asante sana kwa hoja yako muhimu sana na nzuri sana hasa kwa wajasiriamali waliofikia hiyo level, nadhani pana haja ya kufafanua aina ya biashara, ukubwa wake kimtaji, geographically, number of employees, level of management as knowledge, experience, technology applied lingine la muhimu kuliko yote RETURN ya hiyo biashara na mengine mengi,
natamani nikae na wewe kitako tubadilishane mawazo lazima hata wewe una ulilo lifanya hadi kufikia hatua hii....
TATIZO LA WATANZANIA BIASHARA ZETU NI PROFIT ORIENTEDSANA, TUNAANGALIA FAIDA TU NA SI KITU KINGINE,
UAMINIFU MDOGO KWA WAFANYA KAZI HUSABABISHWA NA
1. Elimu- kutowapa elimu ya jinsi ya kusimamia vyema biashara
2. Malipo duni- Wafanya kazi wengi sana wanapunjwa, mwajiri yeyeanaangali faida pekee haangalii wafanya kazi wake wanaishi vipi
3. Marupurup/ motivation
MOJA YA NJIA ZA KUFANYA
1. Elimu- Wafundishe kwanza jinsi ya kusimamia mradi wako, wape elimuya wiki moja kama huwezi kutoa elimu ajiri watalaamu watoe elimu hiyo,wafundishe kwamba hiyo biashara ndo itakayo walisha wao so kadri wanavyosimamia vyema na kupata faida ndo na wao watakavyo nufaika
2. Malipo- Jitahidi sana kuwalipa vizuri wafanya kazi wako- usiangaliefaida tu na kuwalipa wafanya kazi wako elifu 60 wakati maisha yenyewe ndo haya,jitahidi kuwalipa vyema, usiangalie tu kwenye kumake super profiti wakatiwafanya kazi wako wakiwa na maisha magumu sana hapo ni lazima wakuibie sana
3. Motivation/ malupulupu- Jitahidi sana kuwapa vitu vingine vya ziadamfano
- Kuwatoa wakaenda hata kutembelea kambuga fulani
- Tenga pesa ya matibabu yao na familia zao
- Kila mwaka uwe unatoa zawadi kwa mfanya kazi bora, zawadi iwe yamaana lakini si zawadi uchwara
- Sometime Biashara yako ikiruhusu wasaide hata katika kusomesha watotowao kwa kuwaambia utatoa kiwango fulani cha pesa
- Uwe unawasiliza mara kwa mara shida zao na kuwasaidia kutatua hizoshida zao
UKIFANYA HAYO WATAKUWA NA MOYO NA KAZI KWA SABABU WANAJUA JINSI GANIUNAVYO WAJALI SANA
theoretically yes, kiuhalisia mkuu umepotea vibaya sana. Njia pekee ya kuzuia wizi ni wewe mwenyewe kuwa karibu sana na kazi zako, hakikisha unakula nao sahani moja kwa kila step within your business area and you must be very sensitive to detect possible frauds. Weka sheria kali kwa wafanyakazi wako wote na hakikisha kila mfanyakazi anazifuata hapa swala la kuchekacheka ondoa kabisa and you must be cruel inapobidi.
Weka records nzuri ya stock uliyonayo na uwe unafanya inspection daily/twice a week ili kudetect kama kuna loss.
Wakuu wa jukwaa la uchumi nawasalimu.
JUkwaa hili la uchumi ndilo jukwaa ambalo kila siku lazima nilichungulie kwanza,katika pitapita zangu humu nimegundua kwamba wafanyabiashara wengi tumekua tukiumizwa na wafanyakazi tuliowaajiri katika biashara zetu kutokana na wao kutuibia jambo ambalo limesababisha wengine wafunge biashara zao au wengine wapate faida wasiyo stahili.
Mim ni mmoja wa waathirika wa hili tatizo,nina biashara sehemu mbali mbali ambako siwezi kusimamia sehemu zote peke yangu.
Kama kuna ambao mmeweza kudhibiti msiibiwe naomba mtuambie mmetumia mbinu gani kufanikisha hilo.Tusaidiane jamani wenzenu tunaibiwa sana.
Natanguliza shukrani.
Narubongo ameelezea vizuri. Nitafanya extension wa kutoa mifano. Mji wa amsterdam ni bandari kwa miaka mingi sana. Bidhaa nyingi kutoka pembe zote za dunia zilikuwa zinapitia katika bandari hii kabla ya kwenda kwenye nchi zingine za Ulaya.
Na wafanya biashara walioleta bidhaa hizo walihamua kuuza bidhaa zao hapo hapo. Lakini kama wangehamua kuchukua bidhaa hizo na kuzipeleka katika miji mingine ya Ulaya wangepata faida kubwa. Swali linakuja kwanini hawakufanya hivyo?
Kusambaza bidhaa inabidi kuajiri watu ambao watakusaidia kusambaza bidhaa hizo. Tatizo lilikokuwepo ni kuwa waajiriwa wengi walikuwa wanawaibia wafanyabiashara hao na kupunguza faida. Hivyo waleta wa bidhaa wakaamua kuwa wanauza vitu vyao kwa jumla huku wakisimamiwa wenyewe kuliko kutafuta mawakala.
Biashara ni usimamizi. Kama biashara inakupa faida ndogo lakini ukaweza kuisimamia ni bora zaidi kuliko kuwa na biashara mia moja usizoweza kusimamia.
hebu twende na mfano wa guest house ya vyumba 21
una chaji kila chumba sh 10000......
na umeajili watu wa tatu wasimamizi na wasafishaji
na imetokea umesafiri wiki mbili
utawezaje kuzuia wasikuibie?
hebu twende na mfano wa guest house ya vyumba 21
una chaji kila chumba sh 10000......
Na umeajili watu wa tatu wasimamizi na wasafishaji
na imetokea umesafiri wiki mbili
utawezaje kuzuia wasikuibie?
kumlipa mtu vizuri sio suluhisho hata siku moja,ni kawaida ya waajiriwa kutotosheka na mishahara,kwa hiyo mshahara mdogo sio chanzo cha wizi hata siku moja,mfano mzuri ni mishahara ya viongozi wa Afrika,ni mikubwa kushinda ya viongozi wa mataifa yaliyoendelea,ya ulaya lakini bado wanatupeleka pabaya kwa tamaa zao za kupata mali zaidi.
Option ni kuwabana tu employees wako.