jinsi ya kuwadhibiti watu tuliowajiri ktk biashara zetu wasituibie. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

jinsi ya kuwadhibiti watu tuliowajiri ktk biashara zetu wasituibie.

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by queenkami, Mar 30, 2012.

 1. queenkami

  queenkami JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Wakuu wa jukwaa la uchumi nawasalimu.

  JUkwaa hili la uchumi ndilo jukwaa ambalo kila siku lazima nilichungulie kwanza,katika pitapita zangu humu nimegundua kwamba wafanyabiashara wengi tumekua tukiumizwa na wafanyakazi tuliowaajiri katika biashara zetu kutokana na wao kutuibia jambo ambalo limesababisha wengine wafunge biashara zao au wengine wapate faida wasiyo stahili.

  Mim ni mmoja wa waathirika wa hili tatizo,nina biashara sehemu mbali mbali ambako siwezi kusimamia sehemu zote peke yangu.

  Kama kuna ambao mmeweza kudhibiti msiibiwe naomba mtuambie mmetumia mbinu gani kufanikisha hilo.Tusaidiane jamani wenzenu tunaibiwa sana.

  Natanguliza shukrani.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  tumia teknoloji
  wewe una biashara gani labda?
   
 3. S

  Stoudemire JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 840
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kuna biashara nyingine huwezi ku account for kila kitu. Biashara kama hizo unaweza kupunguza wizi huwezi kumaliza kabisa.
   
 4. S

  Silicon Valley JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 554
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 60
  Asante sana kwa hoja yako muhimu sana na nzuri sana hasa kwa wajasiriamali waliofikia hiyo level, nadhani pana haja ya kufafanua aina ya biashara, ukubwa wake kimtaji, geographically, number of employees, level of management as knowledge, experience, technology applied lingine la muhimu kuliko yote RETURN ya hiyo biashara na mengine mengi,
  natamani nikae na wewe kitako tubadilishane mawazo lazima hata wewe una ulilo lifanya hadi kufikia hatua hii....
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  hebu twende na mfano wa guest house ya vyumba 21
  una chaji kila chumba sh 10000......

  na umeajili watu wa tatu wasimamizi na wasafishaji

  na imetokea umesafiri wiki mbili

  utawezaje kuzuia wasikuibie?
   
 6. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #6
  Mar 30, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  TATIZO LA WATANZANIA BIASHARA ZETU NI PROFIT ORIENTEDSANA, TUNAANGALIA FAIDA TU NA SI KITU KINGINE,

  UAMINIFU MDOGO KWA WAFANYA KAZI HUSABABISHWA NA

  1. Elimu- kutowapa elimu ya jinsi ya kusimamia vyema biashara

  2. Malipo duni- Wafanya kazi wengi sana wanapunjwa, mwajiri yeyeanaangali faida pekee haangalii wafanya kazi wake wanaishi vipi

  3. Marupurup/ motivation

  MOJA YA NJIA ZA KUFANYA

  1. Elimu- Wafundishe kwanza jinsi ya kusimamia mradi wako, wape elimuya wiki moja kama huwezi kutoa elimu ajiri watalaamu watoe elimu hiyo,wafundishe kwamba hiyo biashara ndo itakayo walisha wao so kadri wanavyosimamia vyema na kupata faida ndo na wao watakavyo nufaika

  2. Malipo- Jitahidi sana kuwalipa vizuri wafanya kazi wako- usiangaliefaida tu na kuwalipa wafanya kazi wako elifu 60 wakati maisha yenyewe ndo haya,jitahidi kuwalipa vyema, usiangalie tu kwenye kumake super profiti wakatiwafanya kazi wako wakiwa na maisha magumu sana hapo ni lazima wakuibie sana

  3. Motivation/ malupulupu- Jitahidi sana kuwapa vitu vingine vya ziadamfano
  - Kuwatoa wakaenda hata kutembelea kambuga fulani
  - Tenga pesa ya matibabu yao na familia zao
  - Kila mwaka uwe unatoa zawadi kwa mfanya kazi bora, zawadi iwe yamaana lakini si zawadi uchwara
  - Sometime Biashara yako ikiruhusu wasaide hata katika kusomesha watotowao kwa kuwaambia utatoa kiwango fulani cha pesa
  - Uwe unawasiliza mara kwa mara shida zao na kuwasaidia kutatua hizoshida zao
  UKIFANYA HAYO WATAKUWA NA MOYO NA KAZI KWA SABABU WANAJUA JINSI GANIUNAVYO WAJALI SANA

   
 7. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Ukiwajali hawakuibi, ukiwatumia kama majembe lazima wakulize kwa sana!!!
   
 8. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  theoretically yes, kiuhalisia mkuu umepotea vibaya sana. Njia pekee ya kuzuia wizi ni wewe mwenyewe kuwa karibu sana na kazi zako, hakikisha unakula nao sahani moja kwa kila step within your business area and you must be very sensitive to detect possible frauds. Weka sheria kali kwa wafanyakazi wako wote na hakikisha kila mfanyakazi anazifuata hapa swala la kuchekacheka ondoa kabisa and you must be cruel inapobidi.
  Weka records nzuri ya stock uliyonayo na uwe unafanya inspection daily/twice a week ili kudetect kama kuna loss.

  indirect theft: huu wizi unawaliza wengi sana siku hizi bila kujijua na zaidi wenye maduka/suppliers utakuta mfanyakazi wako anaingiza bidhaa zake sawa na zakwako zilizopo stock na kuziuza kupitia biashara yako, matokeo yake unaona wateja wengi lakini quantity yako inatoka kidogo. Hii kitu unaweza ukaidetect kwa kufanya ka intelijesia kako utakachoona katakufaa kutokana na nature ya biashara yako. Mimi nilimshauri ndugu yangu afanye inspection ya kushitukiza na nikamwambia akikuta bidhaa zisizo za kwake achukue uamuzi mgumu wa kujibinafsishia zile bidhaa na kweli alifanya nilichomwambia na alikuta mzigo usio wake wa sh 4.2m.. alimfukuza yule mfanyakazi haraka na tangu siku hiyo haka katabia kalikoma

  Njia nyingine ninayoipenda ni mind games, katika wafanyakazi wako 10 weka watatu wawe kama informers wako kukuletea taarifa za ubadhilifu wa baadhi ya wenzao, make sure hawatambuani (muaminishe kila mtu hiyo ni kazi yake pekee)na wape bonus of around 40%, akikuletea taarifa nyingi zaidi muongezee tena bonus ili awe encouraged zaidi.. this should be repeated and reviewed..

  NOTE: ITAKUSAIDIA KUPUNGUZA
   
 9. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #9
  Mar 31, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Narubungo nimependa maelezo yako hapa... Ila tu umekua too Strict. Ukiwa na hii attitude kwa Wafanyi kazi wako ndio wale ambao at the end of the day huchora mission zako zote na kukabidhi wezi... Mnakua wote mko wote hapo mnavamiwa kiintelligensia na kuibiwa papo hapo. Bila wewe kujua kua nao wamehusika.... Tokana na kuwabana kwako mno. Kubana ni nzuri but there is a line not to cross hasa katika biashara zetu za Kiswahili hizi.
   
 10. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #10
  Mar 31, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Queen kumthibiti moja kwa moja asikuibie kabisa ni kazi saana lazima utaibiwa tu kwa kiwango fulani, na hii hutegemea na Biashara. Kwa mtu ambae ana biashara nyingi ambazo hawezi manage mwenyewe mara nyingi ni nzuri sana kua makini sana katika wafanya kazi.... Lets say Una wafanya kazi 10. Katika maeneo matano tofauti, ni lazima uwe na mtu ambae ni Msaidizi. Na tokana na kwamba wafanyakazi wengi twaajiri ambao sio proffessionals inatakiwa huyo mtu umjenge kuweza kusaidia kuendesha hizo biashara zako.

  Katika hao kumi lazima atakuepo mtu ambae yupo trust worthty, ana bidii, yupo sharp, ana nidhamu na aijua kazi kuliko wenzie.... If at any means unaona hakuna katika hilo kundi mtu wa namna hio; then Nakushauri unaajiri mara moja. Ukisha mpata wa sampuri hio... Invest kwake kumkosha Psychologically and physically. Hakikisha wampa mshahara wa kutosha, marupu rupu, na wamtreat kama rafiki mwenye mipaka (asikuzoee kuvuka mpaka heshima iwe pale pale!) hakikisha wamfundisha kazi hasa upande wa Management ya biashara zako vizuri na muoneshe kua Unamuamini saana (Hakikisha unamuamini kwa % 50 tu!); Huyu mtu atakusaidia kuweza endesha biashara na wewe huku aki pointi penye matatizoa na madhaifu.... na mwaweza work as partners hali ni mfanya kazi wako. Mara nyiingi hii technique ni nzuri for from experience na observation watu wa namna hii huwa hadi wachungu kwa wafanya kazi wenzao. Hapo tayari yeye anakusaidia kuthibiti wenzie wa chini yake (Maadamu tu asiwanyanyase).

  Kuweza kumdhibiti anaekusaidia kuendeha biashara na wale chini yake ni kujua vema Biashara yako.... Ukijua Biashara yako fika hata kama utaibiwa ni katika kiwango cha chini sana. Which can not be escaped. Hii itakusaidia hata unapo pata dharula ya kusafiri nje kidogo ya mji ama matatizo kama misiba ikitokea....
   
 11. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #11
  Mar 31, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,808
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Narubongo ameelezea vizuri. Nitafanya extension wa kutoa mifano. Mji wa amsterdam ni bandari kwa miaka mingi sana. Bidhaa nyingi kutoka pembe zote za dunia zilikuwa zinapitia katika bandari hii kabla ya kwenda kwenye nchi zingine za Ulaya.

  Na wafanya biashara walioleta bidhaa hizo walihamua kuuza bidhaa zao hapo hapo. Lakini kama wangehamua kuchukua bidhaa hizo na kuzipeleka katika miji mingine ya Ulaya wangepata faida kubwa. Swali linakuja kwanini hawakufanya hivyo?

  Kusambaza bidhaa inabidi kuajiri watu ambao watakusaidia kusambaza bidhaa hizo. Tatizo lilikokuwepo ni kuwa waajiriwa wengi walikuwa wanawaibia wafanyabiashara hao na kupunguza faida. Hivyo waleta wa bidhaa wakaamua kuwa wanauza vitu vyao kwa jumla huku wakisimamiwa wenyewe kuliko kutafuta mawakala.

  Biashara ni usimamizi. Kama biashara inakupa faida ndogo lakini ukaweza kuisimamia ni bora zaidi kuliko kuwa na biashara mia moja usizoweza kusimamia.
   
 12. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #12
  Mar 31, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280

  Mkuu usimamie vipi?
  - Mfano unamagari ya Biashara mabasi uwe unayaendesha mwenyewe? au uwe kondact wa mabasi yote? utasimamia biashara yako lakini huwezi simamia katika operation zote,

  - Hakuna biashara ambayo utakua nayo wasikuibie wakiamua,

  - Labuda uwe na TAX NA WEWE NDO DREVA NA WEWE NDO KONDACTA NA WEWE NDO UNAJAZA MAFUTA NA WEWE NDO UNAPELEKA GARI GEREJI

  - Wahindi huwa wanasimamia maduka yao asubuhi hadi jioni lakini wanaibiwa wakiwa hapo hapo, sasa wewe unaongelea usimamizi wa aina gani?

  - Wafanyakazi wako hata sekunde 50 zinatosha kukuibia na wala hawahitaji saa nzima, kitendo hata cha kwenda chooni kinatosha wao kukuibia,


  - NA WIZI UKO KATIKA VITU VINGI SANA MKUU NA SI KWENYE PESA TU
  - wanaweza kukuibia pesa sawa
  - Watakuibia bidhaa zako
  - Watakuibia katika manunuzi
  - Watakuibia katika matengenezo
  - Watakuibia muda

  NILAZIMA UWAJENGEE UWEZO WAFANYAKAZI WAKO NA UWAPE ELIMU YA KUTOSHA NA UWALIPE VIZURI NA KUWAPA STAHIKI ZINGINE,

   
 13. c

  collezione JF-Expert Member

  #13
  Mar 31, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Mimi naona ni culture ya wa_afrika kuibiana. Mimi nimefanya biashara wa wajapan na wahindi. Hawa watu mkiwekeana mikakati ya ukweli hamuibiani. Hata kama anapata kipato kidogo, huwa wanaridhika...

  Kwetu sisi wabongo, mtu anataka atajirike kirahisi kwa kupitia mgongo wako... Yani afanye kazi kidogo tu, kesho watu wamwone tajiri

  Mfanyakazi ukimweka kwenye duka kubwa, baada tu ya miezi mitatu anataka kununu gari....yani ni shida sana ku_control hii kitu. nahic uaminifu kwa wa_Africa ni zero.

  Na ku_control wizi kwa wa_Africa hamna formula...ni jinsi tu utavyojipangilia. Kwasababu wewe njia flani inaweza kukusaidia. Mwenzako akitumia njia hiyo hiyo kwa wafanykazi wake, ina_prove failure.

  Na sio mfanyakazi tu, hata mtoto wako anaweza akakuibia dukani... Hapo ndo utapochoka...
   
 14. Kuku wa Kabanga

  Kuku wa Kabanga JF-Expert Member

  #14
  Mar 31, 2012
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 804
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 80
  kukomesha wizi haiwezekani,lakini tunaweza kupunguza,mimi nashauri tuanze kufanya biashara kisasa,kadri biashara yako inapokua na kuwa kubwa unahitaji management yenye skills,hire professional manager,na kazi zingine kama za kutunza mahesabu na kumbukumbu unaweza kuoutsource,itakusaidia.
   
 15. m

  majogajo JF-Expert Member

  #15
  Mar 31, 2012
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 321
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  kikubwa ni motivation kwa employees, hii itaambatana na perfomance na pia unatakiwa uwe nao karibu ili na ww ugundue system wanayotumia kukuibia na uwe makini kila unapogundua namna wanavyotumia kkuibia....zen wapige bit.
   
 16. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #16
  Mar 31, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Inabidi utumie computerized system na ujitahidi kuwalipa wafanyakazi mishahara mizuri + incentives.
   
 17. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #17
  Mar 31, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  kwa mfano huo unaweza fanya hivi, hao watatu wote umekosea kuwafanya wawe wasimamizi. Hata kama wote ni wasimamizi ni lazima kuwe na msimamizi mkuu ambao wengine watareport kwake.
  Pili, katika kugawa majukumu angalia usije ukampa mtu majukumu ya yeye kuwa na control ya kila kitu. Kwa mfano, unaweza kuta katika biashara mtu huyo huyo anaetunza fedha na kuidhinisha malipo ndio huyo huyo anaehusika na kwenda kupurchase vitu na pengine hata yeye ndio anavikeep hivyo vitu. Hapo lazima uibiwe maana kwenye kutenga fungu la manunuzi atajipangia mwenyewe, kwenye manunuzi anaweza foji risiti na kwenye store anaweza kufoji records. Jaribu kuweka mgawanyo mzuri wa majukumu katika namna ambayo haileti mkanganyiko wa kimaslahi.
  Tengeneza mbinu za kuwamotivate, mfano. Kama unajua guest house yako inaingiza maximum laki 2 kwa siku, unaweza waambia siku watakayoingiza zaidi ya laki 2 watapata bonus ya % fulani kwa wale ambao wapo incharge siku hiyo. Au kama watu watakuwa wanakula hapo hapo then wakataka wapelekewe vyakula vyumbani... Unaweza kuwacharge amount ya hiyo huduma ya mpaka mchumbani then hizo hela zikawa ni marupu rupu ya watu wa jikoni.
  Unaweza kubuni mbinu nyingi za kuwafanya wafanyakazi wako wakawapunguza kuiba au kuacha kabisa.
   
 18. Kuku wa Kabanga

  Kuku wa Kabanga JF-Expert Member

  #18
  Mar 31, 2012
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 804
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 80
  kumlipa mtu vizuri sio suluhisho hata siku moja,ni kawaida ya waajiriwa kutotosheka na mishahara,kwa hiyo mshahara mdogo sio chanzo cha wizi hata siku moja,mfano mzuri ni mishahara ya viongozi wa Afrika,ni mikubwa kushinda ya viongozi wa mataifa yaliyoendelea,ya ulaya lakini bado wanatupeleka pabaya kwa tamaa zao za kupata mali zaidi.

  Option ni kuwabana tu employees wako.
   
 19. Lenana

  Lenana JF-Expert Member

  #19
  Mar 31, 2012
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 422
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  cctv camera may solve this!
   
 20. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #20
  Mar 31, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  wewe unaiba?
   
Loading...