Jinsi ya kuwa 'anonymous' kwenye mtandao

Jinsi ya kuwa 'anonymous' kwenye mtandao

Wakuu, katika pitapita zangu niliamua kulitazama hili suala la kuwa anonymous hasa unapotumia internet.

Kuna sababu nyingi za mtu kutaka kuwa anonymous mtandaoni, mfano kujilinda na kutaka kujihakikishia kuwa hakuna atakayeweza kufuatilia mienendo yake binafsi. Hapa ninaongelea the right to privacy, au kutaka kujifunza tu. Na hicho ndicho kilichonisukuma mimi kushare nanyi jambo hili.

Kuwa anonymous mtandaoni kuna maana kubwa ya kuwa na identity ambayo haihusiani na wewe na hivyo mambo yote utakayofanya mtandaoni yasiweze kufuatiliwa na mtu yoyote au kuwa traced kwako. Hapa naongelea kutumia mtandao kama 'mtu' mwingine wa kufikirika, kwa njia salama zaidi.

Kwa maana hiyo, unakuwa na personalities mbili tofauti ambazo hazilandani kwa lolote na hazijuani kabisa. Moja ikiwa ni wewe hasa, huku ukiendelea na maisha yako na matumizi yako ya mtandao kama kawaida na nyingine ikiwa ni 'anonymous' - wa kufikirika, ambaye hayupo na hajulikani. Watu hawa wawili hawatakiwi kufanana au kushahibiana kwa lolote (mfano email, namba ya simu, mahala pa kuishi, tarehe ya kuzaliwa, JamiiForums ID) wala kuwa na mawasiliano ya aina yeyote....kila personality inatakiwa kuwa na characteristics zake kama mfano tajwa hapo juu. Hili ni muhimu sana.

Kitu kingine kwako utakayeamua kuwa na anonymous online identity: USIMWAMBIE MTU YOYOTE hiyo identity. Simple.

Maelezo yote yapo kwenye hii PDF document iliyo attached. Itakuelezea A to Z za hii concept. Good luck and take care!

ONYO: Hili ni somo tu. MATUMIZI YA HIYO ONLINE IDENTITY YAKO NI JUU YAKO. ZINGATIA SHERIA.

https://piwik.org/wp-content/uploads/2012/01/How-to-remain-anonymous-online.pdf

Karibuni kwa mjadala na maswali kuhusu hili.

Asante kwa kutujuza
 
Kwahiyo mkuu JF wanajua kila kitu kuhusu Mimi kupitia IP address yangu? mfano kujua namba ya SIMU.... kudukua meseji zangu za kwenye SIMU (regular SMS) kudukua FB... Twt..whatsapp n.k??

Tunaanza kupata hofu Kama mambo ndo hayo maana unaweza kumsema vibaya MTU humu akaamua kuchukua taarifa hizo kwa JF kupitia mods wasio waaminifu....

Kwahiyo JF mod yeyote anaweza dukua all information za SIMU yangu? maana unakuta unatumia device moja kutumia mitandao mingi ambayo mingine ID zetu ziko disclosed.....

Msaada kwa hili please.....

Hapana hawanauwezo
informations wanazoweza kujua tu ni unatumia
-Mtandao gani
-Unatoka nchi gani
-Unatumia simu gani
-Unatumia operating system gani yaani windows/android/ios etc
-Na unatumia version gani za Operating system kama ni android 4.1.1 n.k

uwezo wakujua wewe ni nani wanao ISP ambao wanauwezo wakujua namba yako ya simu kupitia hiyo hiyo IP address, ila JF wao wakitaka kujua who are lazma wawe na sababu za msingi wanapoenda kwa ISP wako unaemtumia kwamba lusungo kafanya hiki na hiki IP address yake hii, tunahitaji ushirikiano...
Zipo service online zakujua location ya IP address flani lakini zote ni za uongo, mfano mtu yuko mbeya zinakwambia yupo Dar ila ni ndani ya TZ, wenye real location ya mtu ni ISP.

Ila wewe uki expose IP address yako mtu anaweza kukuattack, ktk computer yako nakuchukua information zako za muhimu nakujua wewe ni nani.
Mfano kuna tools kama RATs (remote accessing tools) kwakutumia tool hii advanced hacker anaweza ku control kila kitu kwenye computer yako yaani mpaka mouse akiwa mbali.
Wewe utakapokua unafanya activities zako mtu anakuchora tu, unaingia FB mtu anakuchora anajua huyu ni flani n.k

sijui kama nimeeleweka ingia hapa uweze kuangalia user agent inavyoonekana baadhi ya info What's My User Agent?
 
Last edited by a moderator:
Ila wewe uki expose IP address yako mtu anaweza kukuattack, ktk computer yako nakuchukua information zako za muhimu nakujua wewe ni nani.
Mfano kuna tools kama RATs (remote accessing tools) kwakutumia tool hii advanced hacker anaweza ku control kila kitu kwenye computer yako yaani mpaka mouse akiwa mbali.
Wewe utakapokua unafanya activities zako mtu anakuchora tu, unaingia FB mtu anakuchora anjua huyu ni flani n.k

Hapo ni noma...hawa jamaa wanapata complete access ya PC yako na wanaficha process yao ndani ya valid process kama explorer. They can do anything including stealing your site cookies and impersonating you, accessing your file system, na ukiiacha PC kwa muda wanainject NetMon and similar tools ili waweze kuaccess GUI remotely kwa Remote Desktop (hapa kuna kawindow kanatokea kwa muda kwahiyo wakifanya huku uko nayo utaiona na utashtuka).

Kibaya zaidi wanakuwa na administrator access. Ni hatari sana.

Sasa snipa, unamuadvise mtu asiye na knowledge kubwa kwenye hii field ajikinge vipi na hacking za aina hii either kwa software au security practices...

Kaspersky Antivirus, inaweza ikasaidia?
 
Yah Karspesky na Avast zinauwezo mkubwa sana wakupambana na hizi vitu ila kama unafanya regular updates..
Antivirus za miaka hii ya karibuni sio zakutumia kwasabu hazijawa tayari kupambana na Virus/malwares wazamani.

Baadhi ya Forums especially za hacking wao ukizingua tu wanakwambia "don't tell us who are you, we know you and where are you from" ndomana nyingi sana wamerestrict huwezi kutumia TOR.
 
Pia mtu asipende kudharau anachoambiwa na Antivirus.
Mfano virus imedetect kwamba site hii haiko safe, mtu anaendelea na yake tena ikiwezekana anatoa kabisa silent gaming mode.
Kuna additional softwares nnazoweza mrecomend mtu kama vile Malwarebytes, huwa inasaidia sana, na kufanya regular scanning ya device yenyewe.
 
I think everybody humu ndani anatakiwa aangalie movie ya CITIZENFOUR ile ya Edward Snowden... Tutaongeza uelewa kwenye swala zima la kwann ni muhimu na pia kujua ni nguvu gani jamaa wanazo ambazo wanaweza tumia kutafuta watu...

Usishangae hata hizo tools kama Hotspot shield nazo zikawa zina backdoor vilevile, mfano mzuri tembelea web ya Lavabit (ambayo ilikua ndo email host snowden alikua akitumia kufanya encryption ya emails zake), halafu uone how deep the guys can go, kwenye hyo website owner ametoa ushuhuda wake... lakini hiyo ni Marekani, ila the methods can apply hata huku bongo incase The police force ikawa na smart people ambao can truly think, kama yuke police wa kwenye movie ya Taken 3, then hapo kimenuka...

Nilishangaa somewhere kwenye hyo movie, snowden anasema kuwa the guys wanamashine zenye uwezo wa kufanya 1 Trillion guesses per second, kama umeshawai kujaribu password cracking, i guess unaelewa ninachomaanisha.

Hata hyo Tor browser yenyewe ambayo watu wanatumia, nimeona Dark websites kibao zikiwa zimeshushwa na FBI, its really hard to be trully anonymous... Kibongo nilishwai muuliza polisi mmoja pale sabasaba ambae yupo kwenye IT Dpt yao, akasema kuwa kama wao wakishndwa huwa wanaomba msaada kutoka nje.

Ni muhimu kuwa anonymous na kuwa conscious na how much information ya letting out kuhusu wewe unapokuwa mtandaoni, personally tayar i`ve done a terrible job and its hard to erase it, unless i create a new alter ego...
 
Sio mfumo wa computer, ni mfumo wa website yenyewe uliyotembelea, kwamfano nyingi zinatumia PHP IP grabbing scripts kuchukua IP address yako wewe, na katika server side kinachoonekana ni IP address yako pamoja na Browser uliyotumia na OS yako pia mostly.

Sio lazima sana kutumia google directly kufanya searching kwasabu kama ulivyosema huwa wanakutrace movements zako.. Ili kukupatia matokeo kiurahisi baadae utakaposearch or for security reason.
Mtu ni muhimu akatumia http://startpage.com ambayo haikeep logs zako yaani unapotumia hii service yao kusearch google huwa wanaona kama mtumiaji anaeserch ni wenyewe startpage lakini sio wewe.,, yaani ni sawa nakumpa mtu akusearchie kwenye computer yake.

Sio wote ambao huwa wanatumia plugins... Na mara nyingi huwa hawafanyi tracing unless yawe yale mambo ya Jomlaa

Sio lazima ISP ajue device unayotumia kuna vitu kama sendbox environment the place where no one is get hurted.
Umeonglea "User agent"
zamani firefox walikua wanatoa option yakutweak user agent yaani mtu anajua unatumia Linux kumbe ni windows. Mfano What's My User Agent?

Anonymous ni kitu kinachowezekana kabisa kama uko knowledgeable na una take kare concerning it.
The word IMPOSSIBLE is found on fools dictionary.
_______________________________________________
 
Yah Karspesky na Avast zinauwezo mkubwa sana wakupambana na hizi vitu ila kama unafanya regular updates..
Antivirus za miaka hii ya karibuni sio zakutumia kwasabu hazijawa tayari kupambana na Virus/malwares wazamani.

Baadhi ya Forums especially za hacking wao ukizingua tu wanakwambia "don't tell us who are you, we know you and where are you from" ndomana nyingi sana wamerestrict huwezi kutumia TOR.

Ndio maana siwezi ku access HackForum kwa TOR. hivi sababu kubwa ni nini...?
 
Hii Movie Ninaitazama Daily Huwa Nabaki Mdomo Wazi Asee... Jamaa wako mbali sana hususa Kwenye Tech.
 
Ndio maana siwezi ku access HackForum kwa TOR. hivi sababu kubwa ni nini...?

Unapotumia Tor kusurf, wengine wanatumia kufanya Attack.
Na ubaya wa Tor mpaka baadhi ya site wanazuia ni kwasabu inawapa kazi kubwa sana wale site admins kujua we ni nani, na ISP nao hawawezi kujua unafanya nini, tofauti na agents wengine.

kwahiyo kama utataka kuepukana na hizi sheria walizoweka jamaa za cyber crime, we tumia Tor ktk online activities zako.
 
Okey... thanks Nimekuelewa.
 
Me siamini hawa watu wenye mitandao si wajinga kama mnavyowachukulia,wanajua kila kitu hata kama uwe na hiyo,wakiamua kakutafuta watakupata tu,na Kwa sababu hiyo wazungu uwa kila wanasema "African people think we are crazy and we know nothing about them but they must know we are not crazy and we are watching them"kila kitu na wakiamua kwa sababu zao wanakukamata,kuna mshikaji wa ivory cost alikuwa anapiga kaz ubalozi wa nje ya nchi akawa anapiga sana deals kumbe jamaa washajua man na uyo jamaa alikuwa na mke wake mzungu na walikuwa wanafanya kaz wote ubalozi lakin mwisho wa siku walimkamata man,wazungu wapo mbali sana au hawa walioanzaisha hii mitandao wakiamua kakutafuta uwe unatumia nini au nini watakupata tu,nina mifano mingi tu nimejionea kwa macho yangu ndugu yangu
Kuna mahackers wasumbufu wamewasumbua sana FBI kwa miaka lkn hawajakamatwa issue ni namna ya kuji protect kuna jamaa mmoja wa kundi la anoynomous na lulzec huyu aliingia kwenye server na kuchukua millions of data za stratfor na kuziachia FBI walishindwa kabisa kumtrace lkn mwishoni alichomwa na sabu snitch,sabu alikuwa hacker pia na kiongozi wa lulsec na anynomous alikuwepo ila jamaa alikamatwa kizembe na hvy FBI wakamtumia wamkamate Hammond

Wapo wengi wasumbufu lkn kwa miaka ss hawajakamatwa,

NB inabidi uwe makini kwa kila step sabb former CIA anayehusika na cyber anasema watu hawa ni wajanja sana lkn tunawafuatilia kwa kila step one mistake wakifanya ndio wanakamatwa mfno huyo sabu alisahau akalog in kwa njia ya kawaida

Ukiwa mjanja na ukijua security steps na ukiwa makini huwez kamatwa na hz windows cyo za kutumia
 
Back
Top Bottom