Jinsi ya kutoka nje ya mwili (Astral Projection)

Rakims

JF-Expert Member
Jun 4, 2014
3,808
2,000
ASTRAL PROJECTION/Mental Projection.

Ni Ule Uwezo Wa Mtu Kutengana Na Mwili Wake Ki Fikra Katika Imani Husemwa Kiroho.
au pale ambapo mwili unakuwa umetengana na fahamu zako.
Utokaji huu wa nje ya mwili upo wa aina mbili au tatu na wenyewe ni wa roughly watu wanafundisha kwa maelezo marefu na mapana hali ya kuwa ni kitu kifupi tu watu wanatakiwa kujua jinsi ya kutoka na mengine kujifunza huko huko.
images (2).jpg

FAIDA ZAKE:
1. Kujitambua kuwa wewe hufi na kuondoka moja kwa moja: Hili ni tukio litakalo kubadilishia maisha. Mamilioni ya watu wamekua wakithibitisha kuwa mtu akifa hapotei moja kwa moja bali kuna maisha mengine ambayo ataishi wale wasioamini life after dealth.

2. Kuongeza uwezo mzuri wa kulala:
Hii husaidia mtu kulala katika hali ya usalama na kupata nguvu inayozungumziwa baada ya kulala na kujua ni ipi sababu kubwa ya kulala tunalala ili miili yetu ipumzike roho zetu zianze kuishi.

3. Kuongeza nguvu ya majariwa:
Hii inaongeza kipawa cha unabii na uwezo mkubwa wa kumsoma mtu akili hufahamika kama kama mind reading au telepathy, kasimama hapo wewe unaongea na roho yake.

4. Kujiendeleza Kimaisha:
Ukiwa nje ya mwili inakuthibitishia kuwa wewe ni zaidi ya binadamu wa kawaida hivyo hukuongezea akili ya utendaji zaidi kwa kutumia maajabu na si nguvu tena.

5. Inakuongezea kukomaa kiroho:
Watu wengi wamekuwa na roho nzuri baada ya kuishi na kiumbe zaidi ya asiekuwa mwanadamu.

6. Inaongeza heshima ya maisha:
Hii hukufanya umuheshimu kila kiumbe na umuhurumie hata paka maana kule una uwezo wa kuongea hata na wanyama pia.

7. Inaongeza akili kumbukumbu na ubunifu:
kupitia ufahamu utakao kuwa nao kwa zoezi hili inaeleweka kwamba utakuwa umefungua sehemu za ubongo wako za fahamu zinazodeal na akili pamoja na kumbukumbu.

8. Kukuwezesha kupata majibu yako mwenyewe kwa spiritual guide:
kutoka nje ya mwili kutakujibia maswali mengi ambayo ulikua huwezi kuyajibu katika ulimwengu wako wa kiroho.

9. Kuondoa woga wa kufa:
kuhofia kifo ni kuhofia jambo usilolijua.utakapotoka utaona kwamba kumbe nina uwezo wa kuishi maisha ya pili hata nikifa.

10. Kutambua na kuelewa mambo ya kale yaliyopita:
utajifunza jinsi ya kupanua ubongo wako haya kuzungumza na historia za kale ingawa unaweza kuona pia tukio lijalo ila hii ni kwa wenye power ya precognition na retrocognitions.

11. Kupaa na kufurahi:
Ulimwengu wa roho hata anga sio mpaka. unaweza kupaa nyuma ya mawingu. na ukapaa kama puto. unataka kuwa na macho ya ndege mjini? la shaka! au unataka kupaa na kuogelea kama samaki dolphin na hata kuruka kama ndege, au kudumbukia ndani na kuogelea kama samaki!

ukitaka unaweza hata kufika kwenye sayari za juu na zile ambazo bado hazijawa discovered wazungu walifanya zamani sana hii na kwenda huko kabla hata ya kurusha ndege, unaweza kwenda popote duniani na nje ya dunia hata kuwatembelea marafiki kila corner ya ulikmwengu

12. Kuthibitisha kwamba mwili wako utakufa ila akili au nafsi yako itabaki tu

13. utayaona mengi maisha yako yaliopita na kuyachezea na utakuwa na nafasi ya kuona kila kitu ambacho unatakiwa kufanya ufanikiwe:
Pia hii yaweza kuwa tiba kubwa kwa magonjwa yasiyotibika kwa maana unaingia hata sehemu ambazo zimefichwa hasa na waweza kula dawa yeyote.

14. Kukutana Na Malaika wako wawili
Utawaona hawa hatua ya kwanza kutoka na kukuongoza kwa mengi ukitaka kuwaona.
japokuwa hawaonekani moja kwa moja ila kama vivuli

15. Kuongeza Nguvu ya miujiza
Kutoka huku kutakufanya uongeze nguvu zako za miujiza kama vile
kuona vitu visivyoonekana kwenye real world, kuskia sauti za mawazo ya mtu, kujua kinachotokea dk kadhaa zijazo, kumlazimisha mtu kufanya utakacho (mind control), kuhisi jambo fulani linatokea, nguvu ya unabii,

16. Kuona aura ya kila kitu na nguvu zingine nyingi tu. haya yote yatakutokea kwa maana umezidi mpaka wa ubongo wako hapa ndio tunaanza kuona more than a normal brain function(waweza kuwa genius pia ukitumia vizuri, anyway usitumie manguvu yote hovyo utaanza kuhisi kuchanganyikiwa fuata hatua kwa hatua.

17. kujaza busara akilini.
hii hukufanya uzidishe busara katika akili yako na amani kuu katika roho yako

18. Kuongeza tamaa ya kupata majibu
Kutoka nje ya mwili kutakufanya kujibu maswali na kujua zaidi kwamba wewe ni nani? upo wapi? na unafanya nini? na unaenda wapi? ukijua hayo hutabadilika mfumo wako wa maisha?

19. Kuwaona waliokufa
Hapa utakutana na ndugu zako uliokuwa ukiwapenda waliotangulia mbele za haki. Kukutana nao huku kutakusaidia sana kuwasaidia kama kuwalipia madeni na kukuonyesha mali walizoficha kama walikua wanakupenda.

20. Kujiongezea maajabu ya maisha
hapa utajifunza mengi kuona kila kiumbe kisichoonekana kupajua sehemu watu na nyumba kabla hujaenda

21. Kupona
Ukitoka nje ya mwili unakuwa umejitibu hapa utaweza kujitibu mwenyewe na wengine na wanyama pia.

Na Hizo bado ni baadhi tu:
astral-travel-compressed.jpg

Ni Aina Ya Nguvu Ambayo Huwa Nayo Watu Wote Isipokuwa Katika 100%

65% Ni Watu Wasioijua

25% Ni Watu Wanaoijua

10% Ni Watu Wanaoitumia

Hatua za kufuata ili uweze kutoka nje ya mwili

Kuna Njia Mbili Za Kutoka Nje Ya Mwili Hapa Nitaielezea Moja.

Njia Hizo Ni:

1; Kutoka nje wewe binafsi

2: Kutoka nje ya mwili kwa msaada wa mlio(Binaural beats)
astral-projection.jpg

HATUA ZA KUFUATA KWA NJIA YA KWANZA:

NI RAHISI TU.!
Ukiwa katika hali ya utulivu na utayari na amani na pia kujiamini kuwa leo nitaweza kutoka kwa mara ya kwanza,

HATUA ZA KUFUATA:
1; Oga Na Vaa Nguo Safi Zisizo Bana yaweza kuwa hata night dress ambayo ni laini au nguo yoyote itakayokufanya uwe vema na huru katika kufanya jambo hili,

2: Lala Chali Mgongo Ukiwa Umenyooka Vema huku umefumba macho, hakikisha hukazi mwili wala kufanya focus yoyote katika mwili wako ili uweze kufanya vema na kwa usawa na utulivu,
images (4).jpg

3: wakati ukiendelea kuutafuta utulivu utapata vishawishi vya kujigeuza au kujitingisha usiweke mawazo yako huko usiweke wazo moja wala usilenge wazo sehemu moja wala usitengeneze picha yoyote akilini wewe tulia tu. Kumbuka ili kufanikisha zoezi lolote la kiroho UTULIVU,UTULIVU,UTULIVU pekee ndio jambo au kitendo au maamuzi pekee ya kukufanikishia jambo la kiroho, usijishike wala kujitingisha wewe tulia tu UTULIVU ndio kitu kiwe kinachozunguka kwenye akili yako na mwili wako na pumzi yako TULIA. utaanza kuhisi uzito kwenye viungo mbali mbali vya mwili wako hasa kichwa.

4: Usitingishe Macho Wala Kuchezesha Mwili Wako. tulizana usiogope wala usihofu kwa maana hakuna cha kukuogopesha kwa wakati huo zaidi ya mwili wako ni sawa na mtu aliyelala usingizi.

5: Subiri Na utulizane Kwenye Pumzi yako ( Hapa unakuwa unaupa taarifa ubongo wako kuwa mwili wote umeshalala au upo kwenye state ya ndoto)

6: ukiweza kujizuia Kujigeuza Geuza Au Kujikuna Ubongo Utajua Umelala Na Utaruhusu Mwili Kuachia Kinga Ya Paralysis Au Ganzi Salama Ya Mwili Mzima.
Ambayo Huwa Inakinga Miili Yetu Kutokujiumiza Wakati wa Kuota Mfano: sleep walking(unaota huku unatembea) au wakati unapigana ndotoni usiweze kupiga au kujiumiza.

7: Wakati Hali Hii Inatokea Hapo Ndipo Unaweza Kujitenga na mwili wako ambao umepata ganzi.
tatizo hapa huwa lipo katika kujua ni upi mwili sahihi maana bado miili miwili inakuwa imeshikana
ukiamka na mwili wako wa ganzi kila kitu utakuwa umevuruga na utaamka kwenye mwili wenye ganzi (hii mimi ninauzoefu nayo pia unajiona upo macho lakini mwili hauamki wala kucheza unaganda ni kawaida ila huwa ni inashtusha kidogo. haichukui muda ni kama sekunde 10 ukianza kujishtua au kujitingisha ila inashangaza kidogo na kukutisha kama ni mwoga kwa maana unaweza hisi utakuwa hivyo moja kwa moja.

Sasa Je Utajua Vipi Kati Ya Miili Hii Upi Ni Sahihi?

Mbinu Rahisi Ipo Hivi Ukifikia Kwenye Hatua Hiyo Ya Kutoka. tengeneza picha Kwamba Una Mikono Mipya Na Miguu Mipya..
na ukishaingia kwenye hali hiyo hutokea set ya mingine na ndio unaweza kutumia kwa kutoka.

Lakini kwa wengine hii huwa ngumu sasa hapo unatakiwa uangalie dali na kuhisi ikiwa ni pamoja na mbinu kuwa kamba inashuka na kukukuta unaishika kisha unahisi inakuvuta na kukufanya uelee

9: Baada Ya Hapo Inuka Katika Mwili Wako huo na Sogea Mbele Hatua Tano Geuka Nyuma na Uangalie Mwili Wako Uliouacha.

10: Hongera Umeweza Fanya Chochote Unachojiskia Hakina Madhara Kwenye Real World....
lakini vipo ambavyo vinaonekana in real world play safe there.
Lakini pia kwa wanaoanza ni bora asiende mbali aishie karibu na nyumbani kisha azunguke zunguke ili azoee mazingira ya mwili huo na hali hiyo.

ANGALIZO:
3638238241_527c68904b_z.jpg

Wakati Unautizama Mwili Wako Uliouacha Kuna Kitu Kina Kuwa Kimekuunga Na Ule Mwili Kama Silver cold Hivi Nyeupe Ya Kama Wingu Hiyo Ndio Hukusaidia Kurudi Hata Kama Umepotea Njia.....
download.jpg

kama una swali ambalo ni personal na upo nje ya forum:

Wasiliana nami kupitia email hii:

Rakimsspiritual@gmail.com

Kwa haya na mengineyo pia tembelea
Rakims Spiritual

Rakims
 
Attachments

Last edited by a moderator:
Jun 18, 2020
84
125
Mkuu faida zake ni kuwa unaweza kujitabiria nini ufanye ili utoboe kimaisha?na mambo mengi yajayo waweza jitabiria?
Ni hayo na zaidi ya hayo mkuu, hata uponyaji pia nilivyofuatilia hii kitu kwenye website mbalimbali na kwenye youtube. Lakini Mimi ninachoogopa nasikia kutoka sio shida kurudi sasa, jasho la ulimi litakutoka
 
Jun 18, 2020
84
125
ndio mana tunaambiwa tulinde silver chird zetu kwa gharama yoyote, japo chances za wao kuingia ni ndogo sana ila wanaweza ukiwaruhusu...by the way ni nice experience...nimeshafika hadi egypy kwenye pyramids..kifupi unaweza fika mahali popote pale, nimefika sehemu nyingi sana, ila siku moja nitakuja kuweka thread yaliyonikuta nilienda sehem ambayo sikutakiwa niende as a soul ..hii dunia ina mambo mengi sana..

HAIL LUCIFER !!!
Umenipa attention nyingine ya kuogapa zaidi. Hebu lete mkuu na sisi tujifunze, Nimepania kuifanya lakini nataka nije niifanye nimeshajua tahadhari zake
 
Jun 18, 2020
84
125
ndio mana tunaambiwa tulinde silver chird zetu kwa gharama yoyote, japo chances za wao kuingia ni ndogo sana ila wanaweza ukiwaruhusu...by the way ni nice experience...nimeshafika hadi egypy kwenye pyramids..kifupi unaweza fika mahali popote pale, nimefika sehemu nyingi sana, ila siku moja nitakuja kuweka thread yaliyonikuta nilienda sehem ambayo sikutakiwa niende as a soul ..hii dunia ina mambo mengi sana..

HAIL LUCIFER !!!
Hiyo silver cord tunailindaje mkuu tusaidie,
 
Waterbender

JF-Expert Member
Oct 2, 2018
1,243
2,000
ndio mana tunaambiwa tulinde silver chird zetu kwa gharama yoyote, japo chances za wao kuingia ni ndogo sana ila wanaweza ukiwaruhusu...by the way ni nice experience...nimeshafika hadi egypy kwenye pyramids..kifupi unaweza fika mahali popote pale, nimefika sehemu nyingi sana, ila siku moja nitakuja kuweka thread yaliyonikuta nilienda sehem ambayo sikutakiwa niende as a soul ..hii dunia ina mambo mengi sana..

HAIL LUCIFER !!!
Sio lucifer tu ni michael big brother
 
ebu naomba mode ya namna unavyo meditate maaan mm naishiaga kupaa paa tu
 
Jan 16, 2018
62
125
ndio mana tunaambiwa tulinde silver chird zetu kwa gharama yoyote, japo chances za wao kuingia ni ndogo sana ila wanaweza ukiwaruhusu...by the way ni nice experience...nimeshafika hadi egypy kwenye pyramids..kifupi unaweza fika mahali popote pale, nimefika sehemu nyingi sana, ila siku moja nitakuja kuweka thread yaliyonikuta nilienda sehem ambayo sikutakiwa niende as a soul ..hii dunia ina mambo mengi sana..

HAIL LUCIFER !!!
Nyinyi ndio majini sasa
 
Jun 18, 2020
84
125
tumia beats kwa ajiri la jicho la tatu kwanza obe ni stage kubwa sana
Sawa, mkuu naomba unisaidie hapa-, Mimi huwa nikilala chali ndio nakuwa comfortable Sana kwa kumeditate, Sasa ninachoogopa nitawezaje kutofautisha kuwa hii inayotaka kunitokea ni Open The Third Eye niifate na hii ni Astra Projection niikwepe wakati nimelala chali?, yaani nilishajaribu kwa kutumia beats nikaanza ku_vibrate nikajiona naanza kuelea elea hivi kwenda juu Nikajikurupua nilijuwa kuwa nilitaka kuingia kwenye Astra na wakati Mimi lengo langu ni Third Eye kwanza na sio Astral.
Nitumie mbinu ipi mkuu Waterbender ili niweze ku open third eye nikiwa nimelala chali kwa kutumia beats? Maana nikikaa nakuwa sipo comfortable
Nisaidieni jamani
 
Jan 16, 2018
62
125
Ahsante Kwa Kuchangia Mkuu Jibu Langu Litoe Hapa Kwenye Haya Maswali!!

1: je, kipindi hicho ulikuwa unajua kusoma?

2: kipindi hicho ulikuwa unawaza upate wapi mwanamke?

3: kipindi hicho ulikuwa unamaskitiko moyoni ya kukosa pesa?

mengi na zaidi ya hayo hukuwa nayo kipindi hicho msongo wa mawazo....

mawazo ndio hupelekea kudumaza subconscious mind na kushindwa kukupa utambuzi Sahihi fanya zoezi hili mkuu hali hiyo itarudi na kwa haraka maana una experience nayo...

umesema unacheza na mbwa sie wengine huwa tunawatisha paka na kuwakimbiza just kama mchezo vile....

"Rakims"
Hivi hii elimu yako inaweza ikawa na majibu ya kwanini mbwa huwa wanabweka "wuuuuuuuuuuuu" wakati wa usiku?
 
Waterbender

JF-Expert Member
Oct 2, 2018
1,243
2,000
Sawa, mkuu naomba unisaidie hapa-, Mimi huwa nikilala chali ndio nakuwa comfortable Sana kwa kumeditate, Sasa ninachoogopa nitawezaje kutofautisha kuwa hii inayotaka kunitokea ni Open The Third Eye niifate na hii ni Astra Projection niikwepe wakati nimelala chali?, yaani nilishajaribu kwa kutumia beats nikaanza ku_vibrate nikajiona naanza kuelea elea hivi kwenda juu Nikajikurupua nilijuwa kuwa nilitaka kuingia kwenye Astra na wakati Mimi lengo langu ni Third Eye kwanza na sio Astral.
Nitumie mbinu ipi mkuu Waterbender ili niweze ku open third eye nikiwa nimelala chali kwa kutumia beats? Maana nikikaa nakuwa sipo comfortable
Nisaidieni jamani
endelea ivo ivo. na watu tupo tofauti we fanya meditaion tu watu hua wanakutana na hali tofauti tofauti kama kupaa ni kaaaida
 
Waterbender

JF-Expert Member
Oct 2, 2018
1,243
2,000
Hivi hii elimu yako inaweza ikawa na majibu ya kwanini mbwa huwa wanabweka "wuuuuuuuuuuuu" wakati wa usiku?
[/QUOT
Hivi hii elimu yako inaweza ikawa na majibu ya kwanini mbwa huwa wanabweka "wuuuuuuuuuuuu" wakati wa usiku?
wanyama wengi wanauwezo mkubwa wa kiona na kusense spirits majin na wanga.sasa moja ya faida ya jicho la tatu iyo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom