mpya9
Member
- Aug 29, 2016
- 31
- 18
Kujiandaa kwa ujio wa mtoto ni kuna changamoto zake. Mtoto ni vema akawa na chumba chake ili kumjengea hali ya kujitegemea akiwa angali mdogo na pia kurahisisha uhifadhi wa vitu vyake bila kuchanganyika na vya wengine. Chumba cha mtoto 'Nursery' inatakiwa iwe comfortable na pia ya kisasa na yenye kuvutia.
Yafuatayo ni mambo ya kuzingatia katika kuandaa chumba cha mtoto anayetarajia kuzaliwa
Tengeneza mpango au design ya chumba
Chagua rangi kwa umakini. Rangi ziwe zenye utulivu na zinazoshabihiana na kuta nyingine za nyumba. Baada ya rangi ni muda wa kuchagua michoro utakayoiweka kwenye kuta. Ingawa michoro ukutani inapendeza, ni ngumu kubadilisha pale hitaji linapotokea. Unaweza kuweka midoli na michoro iliyo kwenye vibao vinavyohamishika au fremu za kuning'iniza.
Usijaze samani kwenye chumba cha mtoto
Sidhani kama ungependa kuingia kwenye chumba cha mtoto asubuhi ukiwa na usingizi tele ukajikwaa kwenye kiti au meza. Weka samani chache zenye ubora. Kitanda cha mtoto, kiti cha kumbembelezea mtoto, meza ya kumbadilishia mtoto na kabati dogo vinatosha. Kitanda kilichounganishwa na kabati ni bora zaidi.
Usisahau vitu vyote vya muhimu
Siku za kwanza baada ya kujifungua huwa ngumu. Kuwa na vitu muhimu vyote itakusaidia pale unapohama kutoka hospitali kwenda nyumbani ili uwe umetulia.
Hivi ni vitu muhimu ambavyo utavihitaji:-
Nepi/Pampers
Mafuta (Ya nazi ni mazuri)
Tishu za kujifutia (Baby Wipes)
Poda
Hand Sanitizer
Dawa ya vidonda (ya kusafishia kitovu)
Nguo za mtoto ( Hasa soksi, kofia na gloves)
Kuwa makini na vitu vya kuchezea mtoto (toys)
Kuwa makini unaponunua vitu vya kuchezea mwanao. Kwanza angalia material yake, size na pia maana ya toy husika( mtoto asikue anachezea bunduki)
Muhimu Zaidi:
Anza sasa. Mimba inachosha hasa katika siku za mwishoni. Usiahirishe kisha ukashindwa kufanya.
========
Leo nakuangazia namna ya kupamba chumba cha mtoto.
Ubunifu kwa namna moja ama nyingine unaokoa gharama za muda na fedha. Ni Ubunifu huu huu wenye nguvu kubwa ya kuwasilisha ujumbe kwa jamii. Wengi wetu naamini tumewahi kusikia njia zilizotumika kuwasiliana miaka ya nyuma kidogo si tu kwenye mapango ya Amboni bali hata Misri ambapo mpaka leo hii wanaakeolojia na wanasayansi wanajaribu kufichua(to decipher) kusoma zile jumbe zilizoandikwa kwenye kuta za mafaraoh kwa kutumia Ubunifu wa hali ya juu.