Jinsi ya kushawishi watu

Mcqueenen

JF-Expert Member
Nov 2, 2019
6,817
11,542
Hello ,
Leo tuongelee mbinu za kushawishi watu.
Hizi nlizisomaga kwny kitabu fulan miaka imepita..Lakini zimenisaidia sana kwa kujua au kutokujua.
Nakuomba nishee na wewe pia.
Ushawishi huu unaweza kuutumia popote iwe ni mahusiano ya kawaida, mapenzi, kazini, biashara, urafiki nk. Yani itakusaidia katika nyanja zote za maisha
Nataka tuongelee Mbinu 5 tu lakini za uhakika, bila kupoteza muda tuanze

1.Nipe nikupe
Binadamu sisi ndivyo tumeumbwa hivyo kama social creatures, dhana ya nipe nikupe ni kitu asilia tunazaliwa nacho kabisa.
Ndio maana mtoto ukimchekea anacheka, ukimnunia analia.
Yani moyo wa binadamu ni kama kioo, ukikisonta kinakusonta, ukikitukana kinakutukana..
Sasa Hii mbinu inafanyaje kazi?
ukitaka kumshawishi mtu akupe kitu au afanye kitu unachotaka inabidi utumie asili yake ya nipe nikupe kumshawishi.
Kwa mfano unataka mtu ahudhurie sherehe yako? Basi Hudhuria za kwake, unataka rafiki yako akupe hela? Basi anza kumpa wewe.
Unataka mpenzi wako akununulie zawadi? Anza kumnunulia wewe
Unataka jirani awe anakusalimia? Anza kuwa unamsalimia.

Hii mbinu ni rahisi, na uzuri wa hii mbinu ni kwamba unaweza ukatoa kidogo halafu ukaja kupata kikubwa.
Unaweza kumpa mteja ofa ya pipi dukani ila ikamfanya awe anakuja kununua hapo kila siku.
Unaweza kumpa mtu hela ndogo ila baadaye wewe akakupa zaidi.
Chamsingi umpe mtu kitu pale ambapo hakutegemea na pia kwenye kumpa uoneshe kujali sio unampa kama basi tu. Mfano "Chukua hii nguo maana imenibana sina pa kuipeleka''❌
" Hii nguo naipenda, ila nmeona itakupendeza zaidi"✅
Kwahyo ukitaka mfanyakazi mwenzako akufanyie favour kubwa hapo kazini, wewe anza kwa kumfanyia favour ndogo.

2.Kuwa adimu
Kwa kifupi, "binadamu tunapenda kupata kwa wingi vile vitu ambavyo vinapatikana kwa uchache."
Ndio sababu madini yana thamani kuliko mchanga unaopatikana kirahisi.
Ndiomaana wasanii mastar ni ngumu kuonana nao kirahisi

Vitu adimu ndio vinapendwa.
Kwahyo kama unataka kushawishi watu, kuwa adimu, kama unataka mpenzi akuwaze kuwa adimu mda mwingine, sio kila akikutaka anakupata (unless amekuoa/umemuoa)
Kama unafanya biashara jaribu kuibrand bidhaa yako kuwa ni adimu
Mfano unataka kumuuzia mtu friji "Hizi friji tunazitoa South Africa na kwa hapa Tz tunaoziuza ni wachache..Na dukani zimebaki mbili tu mpaka nije nifuate mzigo mwezi ujao"(Hata kama unazo 20 stock na jirani anaziuza😁)
Ndiomaana wafanyabiashara wanatumia maneno kama " hii ni ya mwisho njoo uimalizie"

Popote ulipo jaribu kuwa adimu...usiwe mrahisi rahisi tu kupatikana. Utazoeleka na kuonekana wa kawaida tu.
Hata kazini jaribu kuonesha kuwa mchango wako ni adimu na sio rahisi kupata mtu kama wewe hata wakiamua kukufukuza na kuajiri mwingine.

nawaacha na Law of scarcity kwa watu wa uchumi inasema "If what we desire “appears” to be in limited supply, the perception of its value increases significantly"
the key word hapo ni 'appear'...ndiomaana wataalamu wanasema almasi ni rahisi kutengenzwa hata maabara lakini wanazuia sana ili zisishuke thamani

3.Mamlaka
In short, binadamu tunaamini sana mamlaka.
Kwahyo ili ushawishi watu inabidi kwanza waamini una mamlaka juu ya hiko kitu unachowashawishi.
Mamlaka simaanishi serikalini au cheo, namaanisha ile nafasi ya kuwa na utaalamu, credibility, uzoefu juu ya kitu.

Mfano Mtu akivaa kidaktari anakuwa na mamlaka ya kushawishi watu juu ya maswala ya kiafya.
IT ana ushawishi juu ya maswala ya ki'IT kuliko Nesi
Tajiri ana ushawishi wa biashara kuliko masikini (Ndiomaana wazee wa goodmorning walikuwa wanakutania Mlimani city wamevaa suti😁)

Hii ndio sababu pia maduka huweka vyeti vya Brela, TRA ili wateja waone na kujua kuwa hapa ni biashara ya uhakika sio matapeli.

Unaweza kuitumiaje hii mbinu sasa?
Tuseme wewe ni fundi gereji halafu amekuja mteja na gari pale anajiuliza uliza..unaweza kumtuma mfanyakazi wako awe anapokea wageni na akitaka kuwaelezea anasema "Ngoja nikamuite fundi mkuu maana yeye ndio ana uzoefu wa muda mrefu na hizi kazi za AC"
Unauza TV? "Ngoja nkamuite kaka maana yeye ndio anajua TV nzuri kwasababu ameanza kuziuza tokea miaka ya 2006"
Trust me ukija pale, wateja wanakuwa wanakusikiliza kama mang'ombe maana wanakuwa tayari wameshakuamini chochote unachosema.

4.Social proof
"Binadamu tunapenda vitu ambavyo vinapendwa na watu wengi"
Tena pale tusipokuwa na uhakika na kitu, huwa tunapenda kuiga watu wengi wanafanya nini.

Kwahyo ili ushawishi watu inabidi waone kuwa watu wengi wanapenda hiyo bidhaa
Ndiomaana utasikia "Mimi ni charismatic napendwa na mtaa mzima"
"Hii bidhaa inapendwa na watu sana, nimenunua juzi tu ila mzigo umekaribia kuisha"
"Ukichelewa hautoikuta, maana watu huwa wanaipigania"

Ndiyo sababu ya matangazo mbalimbali kutumia wasanii na watu maarufu ili hiyo bidhaa ionekane kama inapendwa sana na watu maarufu wanaitumia.
Utasikia "Kalynda ni ya ukweli, Hata waziri fulani amejiunga...Mtoto wa Mengi amejiunga, mshauri wa serikali amejiunga"
Zote hizo ni mbinu za ushawishi.

Kwahyo ili ushawishi watu, inabidi uwaaminishe kuwa wewe au hiyo bidhaa yako inapendwa na watu wengi.

5. Kupenda
"Binadamu tunakubali tunavyovipenda na kukataa tusivyovipenda"

Sasa ili ushawishi watu inabidi kwanza wawe wanapenda hiko kitu, ili uwashawishi watu wakusikilize inabidi wakupende kwanza.
Na binadamu huwa tunapenda watu tunaofanana nao, wanaotusifia, au wanaoshirikiana na sisi kufiikia lengo fulani.
a)Kufanana nao: hapa namaanisha either kufanana interests, kufanana uwezo, kufanana haiba, kufanana tabia.
ili uwashawishi watu inabidi kwanza uwaaminishe kuwa mnafana kwa kitu fulani ndio maana utasikia "Raisi wa wanyonge, mnyonge mwenzetu" au "mlevi mwenzetu" nk.
Unauza pembejeo? Amekuja mteja mkulima "mimi pia ni mkulima nalima mahindi, hizi dawa zimesaidia sana wadudu"

b)kusifia: Tusiwasingizie wahaya tu, binadamu wote tunapenda sifa. Tunatofautiana viwango tu.

Kwahyo ili uwashawishi watu inabidi uwafanye wakupende kwa kuwasifia.
Mfano "Umependeza" "Una akili nyingi mzee" "Una moyo sana" "Upo vizuri kaka"

Wakishakupenda ni rahisi kuwashawishi kufata jambo unalotaka.
Hata mteja pia unaweza kumsifia mfano we mdada unauza duka la nguo anakuja mteja "Kaka unajua kuvaa, umependeza sana...kuna Tsheti hii hapa inaendana na wewe kabisa"
Trust me unapomsifia tayari unakuwa umeshamteka.
Hata kazini msifie bosi, kwenye mahusiano msifie mpenzi wako.

c)Kutoa ushirikiano: Mtu unatakiwa umuoneshe ushirikiano ili umshawishi.
Sio dukani kwako wewe umekaa unachati yeye anahangaika kutafuta bidhaa...unapoonesha ushirikiano anakupenda, na akikupenda utakuwa una ushawishi mkubwa juu yake atanunua bidhaa.

Kwa leo naishia hapo.
 
Safi saana mkuu. Nimekuelewa vema sana kuna vitu vichache nilikuwa nafahamu ila umeniongezea vitu zaidi.
 
Bado sana soma kitabu kinaitwa how to win friends and influence people
 
madini matupu mzee
 
Asante Uzi mzuri,Kuna kitu nimejifunza..... paragraph ya mwisho Ni Mimi kabisa Nike kwenye biashara yako halafu ujifanye uko busy huwa najiondokea tu kiroho safi
Hahah kweli, wafanyabisashara wengi wanafeli hapa na kwenye lugha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom