Mkuu, ina kubidi kwanza uamue ni kampuni aina gani unayo taka kuanzisha.
Una weza kufanya biashara hiyo kwa kutumia jina lako binafsi, yaani bila ku-register jina la biashara. Hii utahitajika upate barua kutoka kwa mjumbe wa pale ofisi yako ilipo uipeleke pamoja na kitambulisho chako kwa mtendaji atakaye andika barua ya utambulisho kwa watoa leseni wilayani kwako. Baada ya kupata leseni utaenda ofisi za TRA husika kati ka eneo lako ili kupata TIN certificate. Hapo tayari unaweza kuanza kufanya biashara yako.
Unaweza pia kuanza kwa kusajili jina la biashara (Business name)
Business name una weza kusajili kama sole proprietor (una endesha biashara mwenyewe)
au partnership (ya watu wawili au zaidi). Unaweza pia kusajili Limited Company.
Usajili huu wa business name, partnership au Ltd Company utafanyika kwenye ofisi za BRELA zilizopo jengo la Ushirika, mnazi moja, Dsm. Utaandika barua ya kuomba usajili wa kampuni alafu watakujulisha kama hilo jina limesha sajiliwa tayari. Kama bado watakupa fomu za kujaza ili wakutengenezee vyeti vya usajili. Kwenye partnership na Ltd Company utahitaji usaidizi wa wakili ili kutengeneza Partnership deed au Memorandum and articles of Association ya Limited Company.
Kwenye bajeti ya juzi waziri alisema mtu binafsi ata ruhusiwa kusajili na kuanzisha Limited company hata akiwa mwenyewe. Sijui kama hili limesha pitishwa lakini limited company ilikuwa inahitaji watu wawili na zaidi.
BRELA watakupatia vyeti viwili, certificate of registration itakayo onyesha tarehe, jina na namba ya usajili ya kampuni yako na extract from register itakayo onyesha majina ya wenye kampuni. Watapiga mihuri yao pia kwenye partnership deed au Memorandum and articles of association kutegemea kama kampuni ni partnership au Ltd company.
Kama uliamua kutumia business name kwenye leseni hapo juu basi utaambatanisha certificate of registration na extract from register unapofuatilia kwa mtendaji, wilayani na TRA. Katika kila hatua kuna hela utalipia kwenye ofisi husika (Sina hakika sasa hivi ni kiasi gani- lakini sio hela nyingi), TRA ndio nadhani bado hawalipishi chochote kutoa TIN certificate.
Mkuu, usiogope kwenda ofisi yeyote kwa ajili ya kufuatilia usajili wa biashara yako. Kuna watu ambao wameajiriwa na serekali ili wakusikilize na wakuhudumie wewe. Maendeleo ya nchi hii pia inaanza na watu wenye uamuzi kama wako. Kuwa mjasiri na ujiamini kwa kila jambo na utafanikiwa. Nakutakia vyema.