Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ingia kwenye tovuti ya BRELA wametoa maelezo ya kina juu ya usajili wa kampuni. Pia kuna fomu za usajili.
Mkuu,unaweza kufanya biashara kwa jina lako binafsi bila kwenda BRELA kwa kutumia kitambulisho chako kupata leseni na TIN. Unaweza pia kusajili jina hilo lako kuwa jina la biashara kupitia usajili wa BRELA. Kama unatumia jina lako binafsi sheria inakuruhusu kuto kwenda BRELA. Lakini kama utataka kutumia majina mfano. Mjamaica enterprises, Mjamaica general suppliers, mjamaica industries, Mjamaica ltd nk itabidi uanzie BRELA kusudi ijulikane kama kuna kampuni nyingine lenye jina hilo. Kama unatumia jina lako binafsi na unaona labda kampuni inaweza kuwa kubwa au kuwa inaweka matangazo kwenye vyombo vya habari ni vizuri usajili jina lako BRELA hata kama ni la binafsi. Hii ni kwa sababu mtu mwingine akiwahi kusajili jina hilo (labda anaitwa hivyo pia) hautaweza kuweka matangazo yako kwa sababu anaweza kukushtaki. BRELA ina hakikisha kwamba hakuna kampuni mbili zitakuwa na jina linalo fanana na la kampuni nyingine. Anaye wahi kusajili jina la biashara BRELA basi haitakubalika kamwe kampuni nyingine kuitwa jina hilo hilo. Inakuwa ni jina la kipekee na inasaidia sana kwa sababu mfano ukilipwa kwa cheki inamaanisha mtu yeyote mwenye jina kama lako anaweza kuchukuwa ile cheki na kuingiza kwenye akaunti yake na kulipwa hela yako. Ndio sababu benki wanaitisha vyeti vya BRELA wakati wanafungua akaunti za biashara na wanaenda kufanya search huko huko BRELA kuakikisha ni vyeti vya kweli.
Unaends kwa mwanasheria anakuiandalia memorandum and article of association,kuna gharama unalipia kutokana na maelewano na mwanasheria kwa mimi alinifanyia kilo moja,then zikiwa tayari anaweza kukusaidia kuzipeleka brela kwa malipo kuhusiana na brela visit web yao,ila ktk kuregister kampuni minimum capital inatakiwa uwe na tsh laki 3 by the time naregister 2009.brela watasajili jina kama halitakuwepo ktk orodha yao,fee ni ndogo tu,then watakupa certificate of incorporation then ndo utaitumia kuacquire licence ktk jiji na tin tra