marveljt
JF-Expert Member
- Jan 11, 2017
- 1,503
- 1,479
Mahitaji ya uji kwa watu 2-4
1. ngano ambayo haijakobolewa kikombe kimoja kikubwa cha chai(mug)
2. Maji vikombe viwili vikubwa vya chai
3. Maziwa ya chai kikombe kimoja kikubwa cha chai
4. Sukari vijiko vitatu vya chakula.
Maandalizi
1. Chambua ngano zako kisha uzisahe kwa kupitia blender. Saga hadi upate unga ingawaje kutabakia na vipande vidogo vidogo vya ngano.
2. Weka sufuria jikoni pamoja na kiasi cha maji yaliyotajwa hapo juu na uache kwa dakika moja.
3. Weka unga wako na anza kukoroga hadi ulainike.
4. Uji ukishaanza kutokota weka maziwa yako pamoja na sukari ili viendelee kuiva pamoja.
5 . epua uji wako baada ya dakika 10-15 na uko tayari kwa kunywewa.
N.b
1.unaweza kuweka siagi au jibini.
2. Unaweza kutumia maziwa katika upishi wako bila kutumia maji.
3. Kiasi cha unga unaweza kuongezeka kulingana na idadi ya familia.
4. Unaweza kukaanga kidogo ngano kabla hujazisaga.