Jinsi ya kupika maharage kwa njia rahisi bila kutumia gharama kubwa

Wadau napenda sana maharage lakini sasa yananimalizia sana gesi yangu na muda pia

Kuna utundu wowote naweza kufanya angalau kupunguza makali maharage yaive mapema zaidi?
 
Kuna maharage jina maarufu "maharage tyr" yanakuwa yashaiva unanunua super market.
Au kama vp unachemsha ndondo la kutosha kisha unaweka kwenye vibakuli vidogo unatunza kwenye friji,kisha unakamua mdogomdogo.
 
MAUJANJA JIKONI

copy & paste

1.Nimekosa majani ya chai,nitaunguza sukari ,KISHA NITAWEKA MAJI,TAYARI NIMEPATA CHAI.

2.NITAITUNZA STEEL WIRE NDANI YA MAJI,NIKAWEZA ITUMIA KWA KIPINDI KIREFU

3.HUDUMA YA KWANZA KWA MTU ALIEKUNYWA MAFUTA YATAA,SAGA MKAA KISHA KOROGA KATIKA KIKOMBE MPE ANYWE

4.Mfereji Au kitu chochote kilo fanya kutu loweka Au sugulia na Coca-Cola kitang’aa kama kipya.

5.ILI PILAU LAKO LIWE NA TEST HAKIKISHA HUWEKI VITUNGUU SAUM KWENYE MAFUTA,VITIE BAADA YA VITUNGUU MAJI KIWA BROWN KISHA WEKA SUPU NA VIUNGO VYA UNGA THEN VITUNGUU SAUM,PILAU LITANUKIA NA KUWA NA TEST NZURI.

6.Kama upo safarini au upo maeneo ambayo umezidiwa na haja kubwa hamna haja ya kumsumbua dereva!!!.Unachukua mate unapaka kwenye kitovu kwisha habari yake ngoma mpaka ufike sehemu usikaaaa!!!

8.tumia bicarbonate of soda na limao kuondoa weusi kwapani

9.Karai/sufuria yako ina kutu na hata kwa steelwire haitoki….. bandika sufuria/karai lako jikoni likianza kushika moto sugua na kipande cha limao likiwa hapo hapo jikoni.Kutu yote inatoka linakua safi,then unaosha na dodoki

10.Kama upo safarini na ukapata tumbo la kuhara kunywa Maji baridi sana kiasi tu na tumbo litaacha koz utagandisha tena mafuta yanayovuruga tumbo na utakua salama ila ukifika kunywa chai moto kayatoe tu.

11.Vikombe vya udongo vilivyoweka rangi ya chai hadi unaona aibu kumkaribisha mumeo chai,vioshe kwa tumia majivu au stilwaya utavipenda vitakavyong’aa/Vim na still wire ndivyo natumiaga.

12.Chungu ama sufuria jaza majivu unakuwa unafukia moto mle kwenye majivu,huji Kuomba moto kwa jirani au kuwasha kwa mafuta ya taa utayasikia tuu kwa watu.

13.Ukichemsha maziwa ili yasimwagike weka kisosa cha chai ndani ya sufuria /kijiko au uma pia

14.Ukipika wali ama mboga mfano wa maharage kwa bahati mbaya ukaunguza,usimwage badili sufuria na kimenye kitunguu then kitie bila kukikata,harufu haitoi na wala radha ya kuungua hutoisikia.

15.Ukitaka Kufua taulo yako ing”ae vizuri,fulia maji ya moto sana itakua supa

16.Ukipika mchuzi wa nyama ukawa mwepesi sagaa kiazi mviringo juu yake utapata rojo zito.Au koroga ngano kidogo weka,ukikosa ngano tumia sembe kidogoo korogo chuzi zitoooooo.

17.Ukikaangia mafuta samaki ukimaliza kuwatoa samaki kamulia ndimu au limao shombo na harufu yote utatoka,mafuta yatafaa kwa matumizi mengine

18.Ukikosa mkaa na una hamu ya maharage! Chemsha maji yachemke vizuri weka maharagwe kwenye themos tia Yale maji yaliyochemka funika vizuri! Usiku asubui yamekwiva vizuri kabisa yamoto!

19.Ukichemsha mayai na hutaki yapasuke weka chumvi ichemkie.

20.Friji ikitoa harufu weka kaa ndani ama pangusa na bicarbonate soda.

21.Pasi kama imeshika nguo na kuungua paka dawa ya meno upanguse itaondosha ule weusi

22.Maharage kuiva fasta yachambue safi chukua sufuri yako weka jikoni yakaange kama karanga hadi yawe kama yanabadilika then yaoshe bandika jikoni yani mapema sanaa!!

23.Ukiwa na ukoko Sugu nyweleni Au mba jisugulie Limau acha nusu saa osha
Au tangawizi,Limau,na mtindi changanya upake kichwani.

24.Mikono migumu Chukua olive oil na sukari jisugulie Kila Siku Ukimaliza pirika zako baada hapo nawa kwa maji ya uvuguvugu na paka Vaseline.

25.Ukizidisha chumvi kwenye wali menya kiazi mbatata tumbukiza kati kati ya sufuria ya wali chumvi itapungua.

26.Ukiunguza wali kata kitunguu maji weka kwenye wali harufu ya kuungua itapotea.

27.Ukizidisha maji kwenye mchuzi kwangua kiazi mbatata na chuzi litakuwa shatashata

28.Kama una fungus sugu miguu chukua hina ya majani ikoroge na chai kidogo iwe nzito pakaa palipo athirika vaa soksi hata siku nzima fungus itakuwa historia.

29.Sink Chafu lilofubaa jikoni Chukua baking soda na siki ya apple(apple cider vinegar) roweka Hadi asubuhi sugua linakua kama jipya.

30.Sisimizi Sugu wanao kaa jikoni weka pilipili ya unga watahama.

31.Kikohozi kikavuu tafuna majani Ya mbaazi na magadi.Ili mbaazi zisigongwe na wadudu chemsha MAJI yakichemka zitose zitoe anika hagusi miaka.

32.Kiatu kikibana chonga kiazi mbatata tumbuliza kilale humo humo kikaushe kiatu kivae kinatanuka.

33.Jikoni kukifanya vile vidudu vinavyo letwa na matunda weka vinegar kwenye sahani uweke karibu na ulipo weka matunda ama mboga.

34.Ukitaka kitunguu kibadilike rangi fasta unapokaanga tia chumvi.

36.Ukikaanga vitunguu vya biriani mwagia chumvi vitakuwa crunch.
 
Tumia pressure cooker to cut the story short
Unachemsha say kilo 1.,unatia kwny fridge unaunga as needed
 
Back
Top Bottom