Jinsi ya Kupata furaha

Smart Technician

JF-Expert Member
Feb 22, 2015
653
824
Siku moja kundi la watu 500 walikua wamehudhuria Semina. Mara msemaji mkuu wa semina hiyo akaanza kumpa kila mtu puto (balloon), na kuwaambia kila mmoja aandike jina lake juu la puto alilopewa. Kisha maputo yote

yakakusanywa na kuwekwa kwenye chumba kimoja.Kisha watu wote wakaambiwa waingie kwenye chumba hicho na kila mmoja atafute puto lenye jina lake ndani ya dakika 5. Kila mmoja akaanza kuhangaika huku na kule akitafuta puto lake bila mafanikio, na chumba chote kikawa na fujo tupu.

Baada ya dakika 5 kwisha, hakuna hata mmoja aliyekua amefanikiwa kupata puto lake. Ndipo msemaji akawaambia basi kila mmoja achukue puto lolote tu na ampe mtu ambaye jina lake limeandikwa kwenye puto hilo. Ndani ya dakika chache kila mmoja akawa ameshapata puto lake.Ndipo msemaji mkuu akasema:

"Hii inatokea kwenye maisha yetu kila siku. Kila mtu anahangaika kutafuta furaha yake huku na kule, bila kujua ilipo. Furaha yako ipo kwenye Furaha za watu wengine. Wape furaha watu wanaokuzunguka;nawe utapata Furaha yako.Usipende kujitenga... Maisha ni watu.... Bila watu hakuna furaha....hakuna Maisha! Sambaza upendo.. 💐💐🌺🌺🌺
 
Biblia. Wagalatia 5:22-23
[22]Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
But the fruit of the Spirit is love, joy, peace, longsuffering, gentleness, goodness, faith,
[23]upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
Meekness, temperance: against such there is no law.
 
Furaha ni tunda (zao) la Roho Mtakatifu
 
Ukweli mchungu ni kwamba kamwe na milele hutoweza kumfurahisha kila mtu. no matter what you do.
Au itapelekea kuwa people pleaser na utakufa kwa disappointments sababu utakuwa unatumika na watu kukufanyia makusudi.
Huo mfano ni mdogo sana kucover uhalisia mkubwa wa maisha.

Furaha utaipata kutoka kwako tu, ndani kabisa.
 
Siku moja kundi la watu 500 walikua wamehudhuria Semina. Mara msemaji mkuu wa semina hiyo akaanza kumpa kila mtu puto (balloon), na kuwaambia kila mmoja aandike jina lake juu la puto alilopewa. Kisha maputo yote

yakakusanywa na kuwekwa kwenye chumba kimoja.Kisha watu wote wakaambiwa waingie kwenye chumba hicho na kila mmoja atafute puto lenye jina lake ndani ya dakika 5. Kila mmoja akaanza kuhangaika huku na kule akitafuta puto lake bila mafanikio, na chumba chote kikawa na fujo tupu.

Baada ya dakika 5 kwisha, hakuna hata mmoja aliyekua amefanikiwa kupata puto lake. Ndipo msemaji akawaambia basi kila mmoja achukue puto lolote tu na ampe mtu ambaye jina lake limeandikwa kwenye puto hilo. Ndani ya dakika chache kila mmoja akawa ameshapata puto lake.Ndipo msemaji mkuu akasema:

"Hii inatokea kwenye maisha yetu kila siku. Kila mtu anahangaika kutafuta furaha yake huku na kule, bila kujua ilipo. Furaha yako ipo kwenye Furaha za watu wengine. Wape furaha watu wanaokuzunguka;nawe utapata Furaha yako.Usipende kujitenga... Maisha ni watu.... Bila watu hakuna furaha....hakuna Maisha! Sambaza upendo..
Hii nilikua sijajua siku nilipo ijua nimekua na furaha sana kutangamana na watu.
 
Furaha ipo katika kuwapa furaha watu wengine mfano mke akifurahi na familia ikafurahi unapata amani flani😅 ile ndio furaha yenyewe.
 
Nakubaliana na mtoa mada kwa 75% na 25% ni kwamba hata utende wema kiasi gani bado utalipwa maudhi,na kukoseshwa hiyo furaha yenyewe,
Hivyo tujifunze kuwa usichopenda kutendewa na wewe usimtendee mwenzio.
 
Back
Top Bottom