Jinsi ya kupata ajira & connection kwa kijana yeyote mpambanaji

kityentyee

Member
Mar 9, 2021
72
338
Habari zenu wakuu,
Leo napenda kushare jambo hili adhiim kwenu vijana wote watafutaji mliokata tamaa ya kupata michongo, ajira, au connection.

Kulingana na soko la ajira kwa sasa kuwa gumu, kiasi kwamba imekua nadra sana mtoto wa msaka tonge anayemaliza chuo, taaluma au fani fulani kujikuta anaishia kuwa Jobless pasipokuwa hata na matumaini ya kutoboa.

KAZI YA ULINZI
Nadhani kila mmoja wenu atakua si mgeni wa hizi kazi, ila ni miongoni mwa kazi ambazo kijana yoyote msomi anaweza kuzitumia kama starting point itakayo muwezesha kupata exposure, connection na hata Ajira. Kibongo bongo makampuni makubwa yanayoaminika kutoa walinzi mahiri ni pamoja na G4s, GARDA WORLD na SUMA JKT, SOYUZ n.k

Mara nyingi kwa kijana ambaye hana connection, hizi kazi za ulinzi huweza kumexpose kijana au kumuweka kwenye platforms flani ambazo ni rahisi yeye kuonekana / kuonana na watu wengi wazito ambao ni ngumu kuonana nao in a normal way.

Mfano akishaajiriwa, anaweza kuwekwa kwenye malindo nyeti kama Mahoteli makubwa (SERENA, HYYAT ,SLIP WAY, CORAL BEACH, n.k) au ofisi za BALOZI mbalimbali mfano Us embassy, EUROPEAN UNION, TURKEY EMBASSY, n.k, au pia anaweza akapangiwa lindo la mtu binafsi mwenye pesa zake, au makampuni mbali mbali ambapo kiuhalisia yatampa EXPOSURE nzuri sana. Maeneo haya ni rahisi sana Mlinzi mwenye sifa za kitaaluma kupata kazi endapo zikitangazwa, kwanza ni rahisi kuaminika na kupewa kipaumbele kuliko mtu mwingine wa nje.

Kazi ya ulinzi ni kazi nzuri sana kwa kijana anayetaka kutafuta exposure na connection huku akiendelea kusubiri na kupambania ajira ya ndoto yake aliyosomea japo sometimes anaweza pia akajikuta amepata michongo mingine mikubwa out of profession yake.

NOTE
Mungu humsaidia anayejisaidia, usitegemee miujiza ikukute huku ukiwa unashinda ndani tu unafungua mahotpot ya vyakula na kulala kama mjamzito. Ulinzi ni kazi ngumu , akubali kudharaulika, kufubaa,,kukosa usingizi,,kurisk maisha yake (kuuza roho) na mengine mengi.
 
Tatizo binamu yangu ni mfupi futi nne vp ye afanyeje
Ofcourse suala la kimo huwa linazingatiwa sana hasa GARDA WORLD,,ila kama ana cheti cha JKT cha mujibu wa sheria pia kinaweza kumbeba,,halafu siyo kampuni zote zinazozingatia kimo mkuu, kikubwa yeye ajichanganye tu hawezi akakosa kambi
 
Sawa ahsante mkuu vp unaconnect labda apo gurd a world
 
Habar mkuu ujege na connection za fani ya undreva ...maana nifani ambayo watu husotea mno
 
Unaweza kueleza japo kwa ufupi tujifunze mkuu.
Baada ya ku graduate, niliona nisipoteze muda wa kuanza kutafuta ajira , mimi nilichukua cheti changu cha jkt , nikaenda kwenye kampuni moja hivi, ya ulinzi..

Nikajichanga changa, japokuwa mshahara wa kawaida, nikafanikiwa kununua boda boda kwa mtu, so nikawa naingia lindoni jioni , means asubuhi na mchana, nipo road napiga boda..

Bahati nzuri lindo nilipo kuwa, kulikuwa na mishe mishe zingine za kupiga, na unapata hela..

Baadae nikaenda kupanga room, nilihama om, nikawa na jitegemea, sikuwa tena chini ya wazazi.

Nilikomaa sana, japokuwa kulikuwa na changamoto, sometimes unachelewa kuingia lindoni, mnaishia kugombana na walinzi wenzako, na superviser, sometimes unakuwa umechoka , unaishia kulala tu lindoni..

Ila nikafanikiwa

kufungua duka

nikanunua kiwanja

nikaongeza boda boda, nikawapa vijana mkataba

Nikafungua duka la mayai, na kuuza gas..

Baadae nikatemana na kaz ulinzi, nikawa nasimamia biashara zangu, mpaka sasa..

Sijawahi kufikiria kuajiriwa.. bado nakomaa na biashara zangu, i wish one day niwe mbali zaidi ya hapa..

hapo nime summarize tu...
 
Tatizo wabongo wengi, tumejaa na dharau , au nitaonekanaje nikiwa nafanya kaz fulani, kama za ulinz au boda boda.

Kwenye lindo , ambalo mm nilikuwepo, kuna walinzi walibahatika kuingia kwenye vyombo vya usalama, haswa usalama taifa.. Connection zinapatikana hapo hapo ofisini, the way unavyo ishi na watu vizuri, the most thing is good customer care
 
Ushauri wako ni mzuri sana ila asilimia kubwa wakiambiwa huu ushui watapata Sonoma na kuanza kuangaliwa madhara ya kazi ya ulinzi.
 
Baada ya ku graduate, niliona nisipoteze muda wa kuanza kutafuta ajira , mimi nilichukua cheti changu cha jkt , nikaenda kwenye kampuni moja hivi, ya ulinzi..

Nikajichanga changa, japokuwa mshahara wa kawaida, nikafanikiwa kununua boda boda kwa mtu, so nikawa naingia lindoni jioni , means asubuhi na mchana, nipo road napiga boda..

Bahati nzuri lindo nilipo kuwa, kulikuwa na mishe mishe zingine za kupiga, na unapata hela..

Baadae nikaenda kupanga room, nilihama om, nikawa na jitegemea, sikuwa tena chini ya wazazi.

Nilikomaa sana, japokuwa kulikuwa na changamoto, sometimes unachelewa kuingia lindoni, mnaishia kugombana na walinzi wenzako, na superviser, sometimes unakuwa umechoka , unaishia kulala tu lindoni..

Ila nikafanikiwa

kufungua duka

nikanunua kiwanja

nikaongeza boda boda, nikawapa vijana mkataba

Nikafungua duka la mayai, na kuuza gas..

Baadae nikatemana na kaz ulinzi, nikawa nasimamia biashara zangu, mpaka sasa..

Sijawahi kufikiria kuajiriwa.. bado nakomaa na biashara zangu, i wish one day niwe mbali zaidi ya hapa..

hapo nime summarize tu...
Motivation speaker
 
Back
Top Bottom