Jinsi ya kuongea na majini ili wakusaidie

Jinsi ya kuongea na majini ili wakusaidie

Hakushirikiana na mashetani kufanya hivyo. Bali yeye alikuwa ni katika mawalii wa Allah na ile ilikuwa ni katika Karama. Hakuwa walii wa shetani/kuhani/mchawi.

Na kuna tofauti kati ya Walii wa Allah na Kuhani/rafiki wa Shaitwani.

je 'Asif alikuwa kuhani?

Kisai adriz
Kuomba na kutaka msaada kwa kutumia majini hizo njia Mtume Muhammad (Upon him be peace and blessing of Allah) amewahi kufundisha au kufanya ? hata maswahaba zake (Mwenyezi Mungu awaridhie ) wame2ahi kuomba kupitia hivyo ? maana hili hakuna kisingizio kuwa kipindi hiko kulikuwa hakuna shida wala majini na Mtume Muhammad (Upon him be peace and blessing of Allah) asingeweza kuacha jambo kubwa kama maombi yaliyo mazuri ila angefundisha ..
 
kuna mahala nimeweka element ya kitu chochote cha udini? chuki binafsi ulionayo juu ya dini nyingine itakugharimu na itakutafuna sana
Kutaka msaada wa majini ndio maana halisi ya shirk. Waislamu ni maarufu sana kwa haya machukizo!
 
Hizi nyuzi za namna ya kuongea na majini zipo nyingi sana humu, afike pahala walio wahi kujaribu hizo mambo baada ya kupewa mbwinu humu watuletee mirejesho.
Bora ufe kapuku kuliko kujaribu mambo ya kishenzi kama hayo..
 
je nabii suleiman hakufanya kazi na majini?
Nabii wa Allah Sulayman ('Alayhis Salaam) alipewa ufalme ambao hakupewa mwengine baada yake. Haku"fuga" majini, bali Allah katika ufalme aliompa ni kumdhalilishia mashetani watii amri yake. Hakuwa anaingia mkataba nao (kwamba akufuru au afanye dhambi kubwa kisha wamtumikie).

Hakuna aliyepewa ufalme huo katika sisi. Hivyo anayedai kuwa eti majini wanavyomtumikia ni kama ilivyokuwa kwa Nabii Sulayman ni muongo. Sababu ili majini wafanye unachokitaka ni sharti ufuate masharti yake ambayo huwa ni kufanya matendo ya shirki na madhambi kisha ndio akutumikie. Unaingia naye mkataba, unakuwa mshirikina, na hilo halikuwa kwa Nabii Sulayman. Nabii Sulayman hakuwa kuhani/mchawi, hakukufuru;



102. Na wakafuata yale waliyo zua mashet'ani kuuzulia ufalme wa Su leiman. Na wala Suleiman hakukufuru, bali mashet'ani ndio walio kufuru, wakiwafundisha watu uchawi, na yaliyo teremshwa kwa Malaika wawili, Haaruta na Maaruta katika Baabil. Wala hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni mtihani; basi usikufuru. Wakajifunza kwa hao wawili yale ya kumfarikisha mtu na mkewe. Wala hawawezi kumdhuru mtu ila kwa kutaka Mwenyezi Mungu. Na wanajifunza yatayo wadhuru wala hayawanufaishi. Na hakika wanajua kwamba aliye khiari haya hatakuwa na fungu lolote katika Akhera. Na hakika ni kiovu mno walicho jiuzia nafsi zao laiti wangelijua.

(Qur'aan 2:102)
 
Mamboo 😝 majini sio mazuri yameadhiri maisha ya watu wengi sana , acheni kuona kila kitu ni sawa uwe dini gani majini ni mabaya
 
Back
Top Bottom