Nasaha zangu kwa watu, kuingia mkataba na mashetani kunawalazimu kufanya matendo ya shirki na madhambi makubwa makubwa. Hivyo nawanasihi watu mjiepushe na mambo haya. Shirki ni dhulma kubwa kabisa. Na ni machukizo mno kwa Allah.
Pili, baadhi ya watu mfano wa mtoa mada wanaokuja na mada hizi huja na sura na dhahiri za Uislam. Nawaambia Uislam uko mbali na haya na mambo haya yako mbali na Uislam.
Dhambi kubwa kuliko zote katika Uislam ni Shirki. Na hauwezi "kufuga" majini au kuyatumikisha ila baada ya kuingia mkataba nao wa kufanya shirki na kukufuru kisha ndio wakutumikie. Utakuwa mshirikina na pia mtumwa wa majini.
Allah atuweke mbali na shirki.
Nimefikisha.