Jinsi ya kuondoa au kupunguza mafuta tumboni kwa wanawake (Vitambi vya kike)

Nimeshamwambia apunguze vyakula vya mafuta. asile chakula kingi sanaaaa. Wanga apunguze...aongeze mboga za majani, matunda na maji mengi.
Nahubiri tu hapa lakn na mimi napigana na kitambi changu hapa...ha ha haaa
That's nice mkuu ukifanikiwa kabla yangu utaniambia
 
Hakuna dawa kwa maana ya dawa ni kubadili mwenendo wa kula kula na mazoezi.

1. Mazoezi ya tumbo siyo lazima uende Gym au ufanye sitting ups, kwa nyie bidada unaweza kufanya mazoezi yenye faida kwenye nyumba kwa kufanya usafi nyumbani kwako kwa kupiga deki na tambala sakafu ya nyumbani kwako na siyo kutumia vifaa vya kisasa kama fagio la kupigia deki huku umesimama "mopping tools"

2. Epuka au punguza sana vyakula vya wanga kama ugali, wali, mikate, vitumbua, maandazi, tumia kidogo sana nafaka ambazo hazijakobolewa kama uzalendo utakushinda siku za mwazo

3. Epuka vyakula vya kukaangiza au vya kukaanga mfano Chips Mayai, Kuku wa kukaanga, mambo ya "mdudu", epuka au punguza sana kula nyama nyekundu, mfano nyama ya mbuzi, kondoo, ng'ombe; Uzalendo ukikushinda basi usile zile za kukaanga au kuungwa na mafuta; kula kidogo zilizochomwa au kuokwa na kuiva vizuri lakini pembeni yake kuwe na saladi nyingi ya nguvu kwa ajili ya kumeng'enywa haraka usisahau na maji ya moto au green tea

4. Pendelea kunywa angalau glasi moja ya maji ya uvugu uvugu ukiamka kabla ya kula chochote au kupiga mswaki; ukae angalau nusu saa kabla ya kupiga mswaki au kutumbukiza chochote tumboni

5. Kula mlo ambao ni "balance diet" asubuhi waweza tupia chai (green tea), silesi mbili za mkate wa brown, na mayai mawili ya kuku wa kienyeji au kama vipi tupia kabakuli kamoja ka "wheat grain", mchana kula mlo uwe na mboga mboga nyingi hasa jamii ya kabichi na nzuri zaidi za kuchemsha, na kama nyama basi upendelee zaidi kuku wa kienyeji au samaki wa kuchemsha au kuokwa , unaweza tupia na ndizi moja au mbili za kuchemsha, ;

6. Jioni kula chakula kabla ya masaa matatu hadi manne kabla ya kulala, ili unapoenda kulala chakula kiwe kimeshasagwa kabisa. Jaribu kuachana kabisa na ugali, wali na vyakula vya wanga usiku. Potezea tu na mboga mboga, matunda, unaweza tupia kipande cha kuku au samaki wa kuchemsha au kuokwa

7. Kunywa maji angalau lita moja na nusu kwa siku. Hayo maji siyo unayanywa kama bomba la mvua "gudugudugudu!" kwa wakati mmoja. Hakikisha unakuwa na chupa yako kubwa ya lita moja na nusu, mbili, mbili na nusu ambayo unajiwekea lengo la kuimaliza kwa siku

8. Lala usingizi angalau masaa saba, nane, kwa siku.

9. Tembea angalau nusu kwa siku haraka haraka na utoke jasho, siyo unatembea saa nzima halafu unatembea kama unasindikiza harusi. Hamna kitu hapo.

10. Kama umeolewa au una mtu wako ambao umpendaye kweli kweli na ni wako nasisitiza tena ni mtu wako siyo wa kuparamia basi usiwe na hiyana toa mzigo angalau mara nne kwa wiki; hii kitu hupunguza msongo wa mawazo ambao ukizidi husababisha mwili kunenepeana, vile vile ni mazoezi tosha ya viungo; ukipiga mzigo kisawasawa raundi moja ni sawa sawa na kupandisha ngazi kumi za ghorofa; sasa fikiria unaweza kuunguza calories ngapi kwa mwili wako kwa siku tena kwa njia ya raha na mustarehe?

11. Usiwe mtu wa stress, punguza stress ni sumu mbaya ndani ya mwili ambayo husababisha mwili kushindwa kufanya kazi yake vizuri. Weka furaha, amani, upendo pamoja na mambo yote yatuzungukayo.

12. Achana na mambo ya vinywaji vyenye sukari kama soda, juisi za viwandani, kula matunda tena matunda yasiyo na sukari nyingi labda kama uwe na matatizo mengine ambayo itakulazimu kula matunda hayo. Tunda liliwe dakika kumi mpaka kumi na tano kabla ya mlo.

13. Achana na mambo ya monde au pombe, kama unakamata kamata mara moja moja kama wikiendi pata mbili au tatu zinatosha na ziwe zile ambazo siyo makombora zenye sukari na wanga wingi (zenye carbs chache),Sitaki kuingia ndani huko maana ni biashara za watu! kama kuna muziki jiachie ni mazoezi tosha ya mwili na muziki husimumua akili na mambo mengine mwilini.
Mkuu umeongea yote ila vingine vingumu hapo but nitajitahidi
 
Mazoezi ni mengi sana, na si lazima kwenda GYM.

Utakaporudi nyumbani kutoka kazini, muda tosha wa kufanya mazoezi unapatikana. Ni wewe mwenyewe kujiwekea ratiba.

Chumbani panatosha, na Mazoezi ya tumbo ni mengi sana, ngoja nikupe haya mepesi kwanza.

Unachotakiwa kufanya ukiwa chumbani au hata sebuleni ni wewe tu na maamuzi yako, muombe mtu wa kukuzuia miguu yako huku wewe ukiwa umekaa kitako, kisha anza kulala kinyume nyume kidogo, ukishafika chini jinyanyue tena.

Na hii si lazima uwe na mtu hata peke ako, tafuta sehemu ambayo utapenyeza miguu yako ili uweze kujinyanyua na kujirudisha taratibu, na vilevile ukishazoea uwe unajinyanyua kiubavubavu kisha ukijirudisha unajirudisha kwa kanuni ile ile ulioanza nayo, yaani unajirudisha kwa kujiweka sawa, na ukijinyanyua tena unaendelea kiubavubavu ukijirudisha kama nilivyoelezea hapo.

Sasa kwa vile wewe itakuwa ni mara ya kwanza inabidi usiende raundi nyingi, fanya hata kumi kumi kisha unapumzika japo dakika mbili au tatu kisha unaendelea.

Na kwa mtu kama wewe ambae hufanyi mazoezi siku ya pili utajisikia sana maumivu ya tumbo, usiogope inabidi uendelee kila siku mpaka utakapozoea hutohisi maumivu tena, na pia kuwa na utaratibu wa kujiwekea mapumziko japo kwa wiki mara moja, unajiwekea siku moja ambayo unapumzika/hufanyi mazoezi.

Na pia uwe unakunywa sana maji.

Na cha nyongeza, siri ya mazoezi ya tumbo mwanzoni tegemea kuharisha, na wala usiogope kama hali hiyo itakutokea, wewe endelea na mazoezi. Inategemea na tumbo la mtu waweza kuharisha au kutoharisha ila maumivu ya tumbo lazima, usiogope jiandae.

Ruka sana kamba, inasaidia sana kukufanya uwe mwepesi na kupunguza mafuta ya mwili kwa kiasi kikubwa.

Haya maelezo ninayoyatoa naona kama hayatoshi vile, ungekuwa karibu na mimi ningekupa mazoezi ya kutosha na nakuahidi baada ya wiki mbili tu ungeanza kuona mabadiliko
Raha sana kuwa na mtu kama were mkuu maana hili zoezi ngumu sana kwangu
 
Hakuna dawa kanuni ni ile ile ukila bata sana iwe chakula na madiko madiko, uvivu uvivu na matokeo yake kibilikitambi, basi kukiondoa kanuni zake zile zile lakini unafanya kinyume chake! Ndiyo kanuni ya msingi.

Sasa ni kujua madiko madiko gani uyaepuke, na mazoezi gani ufanye.
 
Nimeshamwambia apunguze vyakula vya mafuta. asile chakula kingi sanaaaa. Wanga apunguze...aongeze mboga za majani, matunda na maji mengi.
Nahubiri tu hapa lakn na mimi napigana na kitambi changu hapa...ha ha haaa
itabidi nije nikupeleke gym.... manake inaelekea wewe ni mvivu... lol
 
Kutokuwa na kitambi ndio ndoto ya watu wengi kwa sasa wanaojali afya zao. Kutokana na kufumka kwa maradhi mbalimbali baadhi ya watu wamekuwa wakihangaika kutafuta njia rahisi za kupunguza ama kuondoa vitambi hivyo na uzito uliopitiliza.

Wapo waliamua kukaa na njaa na wengine kutumia dawa kali wakilenga kufikia malengo yao ambayo ni kupunguza uzito. Lakini kuwa na kitambi ama ongezeko la uzito linaweza kuondolewa kwa njia rahisi sana tofauti na unavyodhani. Tena njia isiyohusisha hata chembe ya dawa itakayoweza kukuletea madhara baadaye.

Licha ya wataalamu wengi kusisitiza kuwa kitambi au ongezeko la uzito ni matokeo ya ulaji mbovu, lakini ukweli utabaki kuwa mazoezi kwa sehemu kubwa yana nafasi kubwa ya kupunguza uzito na kuondoa kitambi.

Profesa Christine Rosenbloom, mtaalamu wa lishe kutoka Chuo Kikuu cha Georgia, Marekani anasema kupunguza mafuta mwilini kunaendana na ulaji wa chakula bora pamoja na mazoezi ya kila siku.

“Unatakiwa kufanya mazoezi kwa muda usiopungua dakika 60. Kwa kufanya hivi utaweza kuondokana na matatizo ya unene ama mafuta tumbo,” anasisitiza.

Naye Profesa Michael Jensen wa Kliniki ya Mayo anasema, mazoezi ya viungo yana nafasi kubwa sana ya kuutengeneza mwili wako katika hali nzuri zaidi na pia kuufanya uwe mwepesi pia.

Ni muhimu kuelewa kuwa unapoushughulisha mwili wako, unauweka katika nafasi ya kuunguza mafuta na hivyo kujiweka kwenye nafasi ya kuondokana na unene. Ikiwa utafanya mfululizo ni wazi mwili hautakuwa na mlundikano wa mafuta.

Umuhimu wa mazoezi
Wataalamu wanasema watu wengi huamini kuwa unene ni matokeo ya kula vyakula vyenye kalori nyingi. Hivyo kwa kupunguza kalori wanaamini kuwa itakuwa ni njia rahisi ya kupunguza uzito wa mwili.

Licha ya kuamini hivyo lakini wataalamu wanasisitiza kufanywa kwa mazoezi kwani ndiyo njia pekee itakayoufanya mwili wako kukubaliana na mpango mzima wa kupunguza hizo kalori huku ukiipa nafasi misuli yako kuurudisha mwili katika hali inayotakiwa.

Wanasema kupunguza kalori kwa njia isiyokuwa na mazoezi huwaweka wahusika katika hali ya kunenepa zaidi endapo ataamua kurudi katika ulaji wake wa kawaida.

Kujenga misuli
Jambo la muhimu unalopaswa kufahamu unapoamua kuanza mpango wa kupunguza uzito na mafuta mwilini ni kujua ni nini hasa unatakiwa kufanya. Kuwa na malengo ndiyo jambo la msingi litakalokusaidia kukutia nguvu na hata kufanikiwa.

Watafiti kutoka maabara ya Chuo Kikuu cha San Diego Marekani, waliunganisha mazoezi mbalimbali ya tumbo. Matokeo yake waligundua kuwa mazoezi ya tumbo yana nafasi kubwa sana ya kuikaza misuli inayozunguka tumbo na hivyo kurahisisha zoezi la kupunguza kitambi na kulifanya tumbo kuwa bapa.

Yafuatayo ni mazoezi matano muhimu katika kupunguza mafuta tumboni:
Zoezi la baiskeli – Hili husaidia kukata tumbo sehemu ya chini na ya juu. Unachotakiwa kufanya ni kulala chali. Kisha chukua mikono shika kichwani kwa nyuma upande wa kisogoni. Wakati umelala kunja miguu yako na kisha jinyanyue hadi kujikunja mfano wa ‘C’ iliyolalia mgongo. Fanya hivyo mara 12 hadi 16.

Zoezi la “Sit ups’
Ukiwa umelala chini. Nyoosha miguu yako. Kisha nyoosha juu mikono yako. Jinyanyue na kugusa miguu yako. Fanya hivyo mara 20 hadi 30 Zoezi la kunyoosha tumbo. Kaa chini na nyoosha miguu yako huku ukiitanua hadi kufikia uwezo wako wa mwisho. Geuza kifua chako hadi uweze kuona upande wa nyuma yako kwa uzuri zaidi bila kugeuka mwili mzima. Fanya hivyo huku ukibadilisha upande.

Hakikisha unafanya mara 10 kwa kila upande, mkono wako wa kulia uweze kuzunguka.

Zoezi kunyonga miguu
Hili ni maalumu kwa ajili ya tumbo la chini. Lala chali na kisha nyanyua miguu yako. Anza kuinyonga kama unavyofanya unapoendesha baiskeli. Fanya hivyo mara 20. Utasikia maumivu katika tumbo lako la chini.
Zoezi la kuzungusha kiuno
Simama na kisha shika mikono yako kiunoni. Tanua miguu yako ili kusimama imara. Zungusha mwili wako kuanzia kwenye kiuno kuja juu huku ukiwa umesimama bila kugeuka. Fanya hivyo mara 20. Ukihusisha mara kumi kwa kila upande.
 
Habari zenu wakuu,
Mimi jina tatizo la kua na kitambi kikubwa sana naombeni msaada wenu,hali hii inanipa hofu sana wakati mi bado sijazaa
 
Nani amekwambia Kukimbia ni zoezi la wanawake? Hivi unajua(jogging) kuwa kukimbia ni zoezi bora kuliko yote. Chuma kina hypertrophy muscle kwa wingi zaidi. Kuna watu wengi nawajua wanabeba vyuma na wanavitambi. Zungumza kiv ulicho na uhakika nacho! aceroty

Hajielewi huyo jamaa achana nae..halafu uzi za kupotosha kama hizi zinatakiwa kufutwa haraka sijui kwa nn zinaendelea kubaki
.
 
Hajielewi huyo jamaa achana nae..halafu uzi za kupotosha kama hizi zinatakiwa kufutwa haraka sijui kwa nn zinaendelea kubaki
.
Hakuna upotoshaji Bali kuna ukweli ambao unawaudhi wale waliosomea kulea magonjwa ya binadam
Carbohydrate na sukari ndio maadui namba moja kwenye kuendeleza mafuta kuhifadhiwa kwa kuwa yanahusika moja kwa moja na kimengenyo cha Insulin
Kunenepeana ni matokeo yaparanganyiko wa utendaji wa Insulin na njia pekee ya kurekebisha ni kupunguza ulaji wa vitu vinavyozindua uzalishaji wa insulin na vitu hivyo ni Wanga na Sukari
Hivyo MTU mwenye dhamira ya kuunguza mafuta yaliyohifadhiwa anawajibika kutafiyta namna ya kuufanya mwili ukose wanga na sukari kwa ajili ya kutengeneza nishati
Mwili ukikosa wanga na sukari hutafuta namna mbadala ya kutengeneza nishati hitajika kwa kutumia akiba ya mafuta iliyohifadhiwa mwilini akiba hiyo ndiyo vitambi na minyama zembe sehemu mbalimbali za miili yetu.
Kwa hiyo ni kweli njia ya kuufanya mwili uanze kuyaunguza mafuta ya akiba ili kujitengenrzea nishati ni kuongsza ulaji wa mafuta mazuri na protein na kujizuia ulaji wa wanga na sukari katika mifumo yake halisi.
Hivyo mubimu ni kula mafuta kwa kiasi kikubwa ikifuatiya na protein na vitamini mihimu.
Hivyo wanga kwa kiasi kidogo utaupata kwenye mboga mboga.
Unywaji wa maji mengi ni muhimu sana.

Madaktari wanasomea muda mrefu sana hadi kufudhu na moja ya janga la binadam tena la kudumu ni ukweli kuwa madaktari wapo ili kupooza magonjwa na sio kuyakomesha kwa kuwa wakiyakomesha watafanya nini ?
Sio ajabu madaktari wakipinga hili pia.
Mwenye kitambi na uzito mkubwa tiba ni chakula wala sio mazoezi. Maxoezi ni muhimu kwa afya lakini sio tiba ya kitambi wala uzito mkubwa
 
Hakuna upotoshaji Bali kuna ukweli ambao unawaudhi wale waliosomea kulea magonjwa ya binadam
Carbohydrate na sukari ndio maadui namba moja kwenye kuendeleza mafuta kuhifadhiwa kwa kuwa yanahusika moja kwa moja na kimengenyo cha Insulin
Kunenepeana ni matokeo yaparanganyiko wa utendaji wa Insulin na njia pekee ya kurekebisha ni kupunguza ulaji wa vitu vinavyozindua uzalishaji wa insulin na vitu hivyo ni Wanga na Sukari
Hivyo MTU mwenye dhamira ya kuunguza mafuta yaliyohifadhiwa anawajibika kutafiyta namna ya kuufanya mwili ukose wanga na sukari kwa ajili ya kutengeneza nishati
Mwili ukikosa wanga na sukari hutafuta namna mbadala ya kutengeneza nishati hitajika kwa kutumia akiba ya mafuta iliyohifadhiwa mwilini akiba hiyo ndiyo vitambi na minyama zembe sehemu mbalimbali za miili yetu.
Kwa hiyo ni kweli njia ya kuufanya mwili uanze kuyaunguza mafuta ya akiba ili kujitengenrzea nishati ni kuongsza ulaji wa mafuta mazuri na protein na kujizuia ulaji wa wanga na sukari katika mifumo yake halisi.
Hivyo mubimu ni kula mafuta kwa kiasi kikubwa ikifuatiya na protein na vitamini mihimu.
Hivyo wanga kwa kiasi kidogo utaupata kwenye mboga mboga.
Unywaji wa maji mengi ni muhimu sana.

Madaktari wanasomea muda mrefu sana hadi kufudhu na moja ya janga la binadam tena la kudumu ni ukweli kuwa madaktari wapo ili kupooza magonjwa na sio kuyakomesha kwa kuwa wakiyakomesha watafanya nini ?
Sio ajabu madaktari wakipinga hili pia.
Mwenye kitambi na uzito mkubwa tiba ni chakula wala sio mazoezi. Maxoezi ni muhimu kwa afya lakini sio tiba ya kitambi wala uzito mkubwa


Mazoezi sio tiba ya kitambi labda kwako na mtoa mada sisi wengine tumeshapoteza na kuteketeza kba vitambi kwa mazoezi.. so hizo porojo zenu bakini nazo wenyewe na vilazza wengine
 
kuruka kamba zoez zur sana huwa nalitumia nkiwa nahisi uviv kwenda kiwanjani...tafuta stop watch ruka kwa sek 20..pumzika sec 10 rudia hivyo mara tano
 
Wanawake wengi miaka ya karibuni wanakabiliwa na tatizo linalofanana na kitambi kwa upande wa wanaume. Hivyo ingekuwa ni wanaume tungesema ni kitambi ambalo nalo ni tatizo kubwa miongoni mwa wanaume wengi nyakati za sasa.

Kinachowasumbuwa wanawake siyo kitambi tunasema ni mlundikano wa mafuta sehemu ya chini ya tumbo na tumbo kwa ujumla kufikia hali kuonekana kama ana tumbo kubwa au kuhisi labda ni ujauzito kumbe ni mafuta tu mengi.

Kwa ujumla ni vigumu sana kupunguza tumbo la namna hii, hivyo kwenye post hii pamoja na mengine tutaona pia visababishi vya tatizo lenyewe, dawa za asili zinazoweza kuondoa tatizo hilo na aina ya maisha unayotakiwa kuishi ili ufanikiwe kirahisi zaidi bila kukuachia madhara mengine yoyote.

Nini kinasababisha tumbo kwa kina mama:
  • *Vyakula feki (Junk food)
  • *Kutumia vyakula vya wanga kupita kiasi
  • *Kutokunywa maji ya kutosha kila siku
  • *Kula chakula kizito muda mchache kabla ya kwenda kulala
  • *Kukaa masaa mengi kwenye kiti
  • *Kutokujishughulisha na mazoezi
  • *Mfadhaiko (stress)
  • *Kula wali kila siku
  • *Ugali wa sembe
  • *Kula vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi (chipsi, maandazi, nk)

Vyakula 25 vinavyoondoa mafuta kwenye tumbo kwa wanawake

1. ASALI NA LIMAU
Chukua asali kijiko kikubwa kimoja cha chakula na majimaji ya limau vijiko vikubwa viwili, changanya hivi viwili ndani ya glasi moja (robo lita) ya maji ya uvuguvugu na unywe yote mara tu ukiamka asubuhi.
Tumia kwa wiki 3 hivi mpaka mwezi mmoja na hutachelewa kuona tofauti.

2. MAJI YA UVUGUVUGU
Kunywa maji ya uvuguvugu kama lita 1 hivi wakati tumbo likiwa tupu hasa asubuhi ukiamka tu. Hii inasaidia kusafisha mwili na kuondoa mafuta yasiyohitajika.

3. NYANYA
Kula nyanya ambazo hazijapikwa pia inasaidia kupunguza tumbo kwa kina mama, hivyo kula kachumbali ya kutosha kila siku ya nyanya peke yake na utaona mabadiliko.

4. TANGAWIZI
Chemsha chai ya tangawizi, ipua na usubiri ipowe kidogo, ongeza asali mbichi kidogo na pilipili manga kidogo ya unga. Pata kikombe kimoja cha chai hii kila siku asubuhi mapema ukiamka tu. Asali inasaidia kuyeyusha mafuta wakati pilipili itauongezea nguvu mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.

5. SIKI YA TUFAA
Siki ya tufaa (apple cider vinegar) inasaidia kupunguza njaa na kukufanya ujisikie umeshiba kwa kipindi kirefu. Kunywa kijiko kikubwa kimoja cha siki ya tufaa mara 1 kwa siku kila siku wakati unakula chakula cha usiku. Kazi nyingine ya hii siki ni kuweka sawa damu sukari mwilini hivyo ni nzuri pia kwa wenye kisukari.

6. MAJANI YA BIZARI
Majani ya bizari husaidia kuondoa sumu na takatka nyingine mwilini kitu ambacho moja kwa moja hupelekea mlundikano mdogo wa mafuta katika tumbo. Kunywa chai ya majani ya bizari kila siku asubuhi, ukikosa majani unaweza kutumia hata unga wake.

8. ILIKI
Iliki hufanya kazi ya kuongeza nguvu katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula na ni dawa nzuri sana ya kuondoa sumu na takataka nyingine mwilini. Iliki pia hutumika katika kupunguza uzito. Tengeneza chai yenye iliki kila siku ndani yake, pia ni kiungo karibu kwa vyakula vingi hivyo hakikisha unaiweka katika kila chakula unachopika kwa matokeo mazuri zaidi.

9. MDALASINI
Mdalasini hufanya kazi ya kuchoma mafuta mwilini. Chukua kijiko kidogo kimoja cha mdalasini ya unga na uweke ndani ya glasi 1 ya maji ya moto na uache kwa dakika 5 hivi. Ongeza kijiko kidogo kimoja cha asali mbichi ndani yake na ukoroge vizuri, kisha unywe huo mchanganyiko wote asubuhi ukiamka tu.

10. JUISI YA LIMAU
Kunywa maji ya limau au juisi ya limau kila mara kutakusaidia kuondoa mafuta tumboni kwa haraka sana. Ongeza majimaji ya limau vijiko vikubwa viwili ndani ya glasi 1 ya maji na uongeze punje 1 ya chumvi ya mawe, koroga vizuri na unywe asubuhi ukiamka tu kila siku.

11. KITUNGUU SWAUMU
Ili kupunguza mafuta tumboni katakata vipande vidogo vidogo (chop) punje 3 mpaka 4 za kitunguu swaumu na unywe na maji vikombe viwili asubuhi tu na kisha shushia na glasi moja ya maji yenye limau kidogo kwa mbali. Hii ndiyo njia nzuri kabisa ya asili ya kuondoa mafuta tumboni kwa haraka zaidi.

12. TIKITI MAJI
Tikiti maji lina asilimia 82 za maji kitu kinachofanya tumbo lako kutokuwa na njaa ya kuhitaji chakula. Tikiti maji lina vitamini C ambayo ni mhimu kwa afya bora. Kula tikiti kila siku.

13. MAHARAGE
Kula maharage kila mara kunasaidia kupunguza mafuta katika tumbo. Maharage yana kiasi kingi cha nyuzinyuzi (faiba) kitu kinachosaidia tumbo lako kutojisikia njaa na hivyo itakuwezesha kula chakula kiasi kidogo. Kadri unavyokula chakula kichache ndivyo unavyokuwa mbali na uwezekano wa kuzalisha mafuta mengi tumboni.
Basi kula maharage kila siku.

14. TANGO
Tango lina asilimia 96 za maji na asilimia zinazobaki ni nishati. Tumia kachumbali yenye tango ndani yake kila siku au kula tu tango moja kila siku ili kupunguza mafuta tumboni kwa haraka.

15. PARACHICHI
Parachichi ni tunda lingine zuri sana kwa ajili ya kuchoma mafuta yaliyozidi mwilini. Parachichi ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi (faiba). Parachichi huikimbiza mbali njaa na wewe. Parachichi lina mafuta lakini ni mafuta mazuri (monounsaturated fatty acids) ambayo yenyewe husaidia kuchoma mafuta na hivyo kuondoa mafuta mabaya tumboni kirahisi zaidi.
Kula parachichi 1 kila siku.

16. TUFAA
Kula tufaa maarufu sana kama 'apple' (epo) kunaweza kusaidia kupigana na magonjwa mengi sana mwilini na inaweza pia kusaidia kuondoa mafuta kwenye tumbo lako. Tufaa hukufanya ujisikie umeshiba sana kwa masaa mengi sababu lina potasiamu na vitamini nyingi sana ndani yake.
Hivyo kula tunda hili 1 kila siku asubuhi kupunguza shauku yako ya kutaka kula zaidi ndani ya hiyo siku nzima.

17. MAFUTA YA SAMAKI
Mafuta ya samaki ni mbadala mzuri kabisa katika kuchoma mafuta ya tumboni. Mafuta ya samaki yenyewe hulenga kuyachoma moja kwa moja mafuta yanayozidi tumboni. Ukiweza unaweza kuamua yawe ndiyo mafuta yako ya kupikia, pia unaweza kunywa mafuta haya kijiko kikubwa kimoja kila siku unapoenda kulala.

18. SIAGI YA KARANGA
Siagi ya karanga hupunguza njaa na kuongeza nguvu katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Siagi ya karanga ina kiinilishe kijulikanacho kama 'niacin' ambacho chenyewe huzuia mafuta kujilundika tumboni. Hivyo kwenye mkate wako asubuhi ningekushauri utumie hii siagi ya karanga badala ya mafuta mengine ambayo si salama, pia unaweza kutumia hii siagi ya karanga kama mafuta yako ya kuunga katika mboga nyingi unazopika hata katika wali unaweza kutumia kama mafuta yako mbadala.

19. MAYAI
Mayai yana vitamini nyingi sana ndani yake (mayai ya kienyeji lakini) na yana madini pia kama kalsiamu, zinki, chuma, omega -3 nk. Viinilishe vyote hivyo katika mayai husaidia kuchoma mafuta yanayozidi tumboni. Hivyo kula mayai asubuhi kila siku ili kuondoa na kupunguza mafuta mwilini. Mayai pia ni moja ya vyakula vinavyomfanya mtu ajisikie kushiba kwa muda mrefu bila kuhitaji kula kula tena.

20. CHAI YA KIJANI
Chai ya kijani maarufu kama 'Green tea' hufanya kazi ya kuondoa sumu mwilini jambo linalosaidia pia kuchoma mafuta yaliyozidi mwilini. Kunywa chai hii ya kijani kila siku kutafanya ngozi yako kukua vivyo hivyo kufanya tumbo lako kukaa sawa bila kuwa na mafuta mengi.

21. MTINDI
Ingawa mtindi unaweza kupelekea kuongeza uzito zaidi, hata hivyo mtindi mtupu kabisa ule ambao haujaongezwa kingine chochote ndani yake unaweza kukusaidia kupunguza mafuta tumboni. Matumizi yake kwa siku yasizidi kikombe kimoja (robo lita). Pia mtindi ni moja ya vyakula vinavyoweza kukufanya ujisikie umeshiba na hivyo kukuondolea njaa ya kutaka kula.

22. JUISI YA KOTIMIRI
Juisi ya kotimiri (Parsley juice) huondoa sumu na takataka nyingine zozote mwilini, pia huchoma mafuta na nishati. Kotimiri ni dawa nzuri kwa matatizo mbalimbali ya figo pia kwa kuchoma mafuta mwilini.
Pata kikombe kimoja cha juisi hii kila siku unapoenda kulala.

23. NDIZI
Kama lilivyo tufaa, ndizi pia zina kiasi kingi cha potasiamu na vitamini za aina mbalimbali ndani yake. Ukipenda kula ndizi kila mara zinachofanya mwilini mwako ni kuondoa ile hamu ya kutaka kula vyakula feki (fast food). Zaidi sana ndizi huuongezea nguvu mfumo wa mmeng'enyo wa chakula na hivyo kupelekea mafuta ya tumboni kuyeyuka kirahisi zaidi. Kula ndizi kila siku ukiweza ukiamka tu kula ndizi zilizoiva 3 mpaka 5 kila siku.

24. MAJI YA KUNYWA
Kunywa maji ya kutosha kila siku kunasaidia pia kupunguza uzito. Kunywa maji lita 2 mpaka 3 kila siku iendayo kwa Mungu. Kunywa maji kidogo kidogo kutwa nzima. Hili halitafanya kazi ya kusafisha mwili tu bali pia litafanya ngozi yako kung'aa na kukuwa. Nywele zako pia zitaonekana ni zenye afya na mwili mzima utakuwa ni wenye kuvutia.

Kitu cha kwanza ukiamka tu ni kunywa maji glasi 2 na uendelee hivyo hivyo glasi moja moja kila baada ya lisaa limoja au mawili kutwa nzima. Maji ni uhai, bila kunywa maji kila siku ni sawa na kwenda dukani bila hela mfukoni.

Asilimia 94 ya damu yako ni maji, asilimia 85 ya ubongo wako ni maji, asilimia 27 ya mifupa yako ni maji, asilimia 75 ya mwili wako ni maji. Sehemu kubwa ya dunia hii imefunikwa na maji na sehemu yenye ardhi ni kipande kidogo sana. Haijalishi unaishi kwenye baridi au kwenye joto hakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku, huhitaji kusikia kiu au hamu ndipo unywe maji, hapana maji ni lazima uyanywe tu hata iweje.

25. MAZOEZI YA KUTEMBEA
Shida kubwa kwa kina mama wengi wa kiTanzania ni kuwa hawajishughulishi na mazoezi. Hapa Tanzania mazoezi inaonekana ni jambo la wanaume tu. Mazoezi ni jambo la lazima kwa mtu yeyote iwe unaumwa au huumwi.

Ili kuchoma mafuta mwilini kwa haraka zaidi tembea kwa miguu mwendo kasi kidogo lisaa limoja kila siku. Kumbuka nimesema lisaa limoja yaani dakika 60 bila kupumzika (none stop) kila siku. Kutembea kwa miguu lisaa limoja huamsha mwilini kimeng'enya kijulikanacho kama 'lipase' ambacho chenyewe huamka tu ikiwa utatembea bila kusimama kwa dakika 60 na kikishaamshwa (when it is activated) huendelea kuchoma mafuta mwilini kwa masaa 12 mfulululizo.

Usiseme nikitoka sehemu fulani kwenda sehemu fulani nitakuwa nimetembea vya kutosha, hapana, unahitaji uwe na saa mkononi kuhakikisha kweli dakika 60 zimeisha ukiendelea kutembea bila kusimama. Kama utaweza kukimbia kidogo kidogo (jogging) basi utachoma mafuta ya tumbo kwa haraka zaidi.
Ufanye zoezi hili kila siku kwa mwezi mmoja mpaka miwili mfululizo na mafuta kwenye tumbo lako yatapotea yenyewe bila kupenda.


Kwa hisani ya Deusdedit Mahunda blog
 
Sijaona adui rafiki mwingine wa vitambi vya kike hapa, Beer. Ila maendeleo ya siku hizi mtu ashindwe mwenyewe maana kuna calorie-free ama less kabisa.
All in all, mapunguzo yakiendana na mazoezi ya tumbo matokeo huonekana haraka zaidi.
 
na kweli, asante kwa somo maana wanawake wenye vitambi wanakera sana , yani hawana mvuto kabisa
 
Back
Top Bottom