Jinsi ya kuondoa au kupunguza mafuta tumboni kwa wanawake (Vitambi vya kike)

FANYA MAZOEZI,
USIPENDE SHORTCUT...

unawezaje kupunguza JITUMBO Kwa kupungiza kula?
huko ni kuudhoofisha mwili mzima..
AM DONE.
Hatakiwi kuacha kula. inaonekana anakula sana kuliko kiasi cha kawaida pia anapenda mapochopocho. Mimi pia nina tatizo hilo lakini nikila ipasavyo kwa wiki tu tumbo linapungua tena bila mazoezi. Ulaji mbovu unachangia sana kwenye hivi vitambi vya siku hizi
 
Hii siyo picha sahihi.
Hebu weka full picha huku umesimama, vaa nguo ya kubana mwili kisha upigwe kutokea pembeni.
Ili niweze kujua tatizo lako ni kubwa kiasi gani, na nitaweza kukupa tiba sahihi zaidi.
Kama ukishindwa kuweka hapa basi nitumie PM pamoja na mawasiliano yako.
Poa
 
Anza na hilo lililo ndani ya uwezo wako. Kunywa maji lita1 au hata nusu lita unapoamka kabla hujaweka kitu mdomoni. Mchana kula kiasi, usiku kula chakula mapema ikibidi kula matunda au chakula kidogo sana, kabla ya kulala kunywa maji tena hata glass moja.
Asante
 
Hatakiwi kuacha kula. inaonekana anakula sana kuliko kiasi cha kawaida pia anapenda mapochopocho. Mimi pia nina tatizo hilo lakini nikila ipasavyo kwa wiki tu tumbo linapungua tena bila mazoezi. Ulaji mbovu unachangia sana kwenye hivi vitambi vya siku hizi
Jamani mi nikila tumbo linakua kubwa i hope ungeniona nikiwa nimeshiba
 
Jamani mi nikila tumbo linakua kubwa i hope ungeniona nikiwa nimeshiba
Nakuelewa sana. ikibidi achana na soda, chips na vyakula vyenye mafuta mengi. usiache kula lkn punguza kiasi ulichokiwa unakula. Maji mengi...ukisikia njaa kama muda wa kula bado kuka matunda au maji. Usiku kula chakula chepesi na pia ukisha kula usiende kulala hapo hapo. Tenga kama masaa mawili ndio ulale. Ukifanya hivyo ndani ya mwezi utaona mabadiliko. Kama unaweza mazoezi fanya pia.
 
Nakuelewa sana. ikibidi achana na soda, chips na vyakula vyenye mafuta mengi. usiache kula lkn punguza kiasi ulichokiwa unakula. Maji mengi...ukisikia njaa kama muda wa kula bado kuka matunda au maji. Usiku kula chakula chepesi na pia ukisha kula usiende kulala hapo hapo. Tenga kama masaa mawili ndio ulale. Ukifanya hivyo ndani ya mwezi utaona mabadiliko. Kama unaweza mazoezi fanya pia.
Asante sana good point
 
Hatakiwi kuacha kula. inaonekana anakula sana kuliko kiasi cha kawaida pia anapenda mapochopocho. Mimi pia nina tatizo hilo lakini nikila ipasavyo kwa wiki tu tumbo linapungua tena bila mazoezi. Ulaji mbovu unachangia sana kwenye hivi vitambi vya siku hizi
Kwahiyo unamshaurije kwenye hiko kipengele cha ulaji?
 
Kwahiyo unamshaurije kwenye hiko kipengele cha ulaji?
Nimeshamwambia apunguze vyakula vya mafuta. asile chakula kingi sanaaaa. Wanga apunguze...aongeze mboga za majani, matunda na maji mengi.
Nahubiri tu hapa lakn na mimi napigana na kitambi changu hapa...ha ha haaa
 
Hakuna dawa kwa maana ya dawa ni kubadili mwenendo wa kula kula na mazoezi.

1. Mazoezi ya tumbo siyo lazima uende Gym au ufanye sitting ups, kwa nyie bidada unaweza kufanya mazoezi yenye faida kwenye nyumba kwa kufanya usafi nyumbani kwako kwa kupiga deki na tambala sakafu ya nyumbani kwako na siyo kutumia vifaa vya kisasa kama fagio la kupigia deki huku umesimama "mopping tools"

2. Epuka au punguza sana vyakula vya wanga kama ugali, wali, mikate, vitumbua, maandazi, tumia kidogo sana nafaka ambazo hazijakobolewa kama uzalendo utakushinda siku za mwazo

3. Epuka vyakula vya kukaangiza au vya kukaanga mfano Chips Mayai, Kuku wa kukaanga, mambo ya "mdudu", epuka au punguza sana kula nyama nyekundu, mfano nyama ya mbuzi, kondoo, ng'ombe; Uzalendo ukikushinda basi usile zile za kukaanga au kuungwa na mafuta; kula kidogo zilizochomwa au kuokwa na kuiva vizuri lakini pembeni yake kuwe na saladi nyingi ya nguvu kwa ajili ya kumeng'enywa haraka usisahau na maji ya moto au green tea

4. Pendelea kunywa angalau glasi moja ya maji ya uvugu uvugu ukiamka kabla ya kula chochote au kupiga mswaki; ukae angalau nusu saa kabla ya kupiga mswaki au kutumbukiza chochote tumboni

5. Kula mlo ambao ni "balance diet" asubuhi waweza tupia chai (green tea), silesi mbili za mkate wa brown, na mayai mawili ya kuku wa kienyeji au kama vipi tupia kabakuli kamoja ka "wheat grain", mchana kula mlo uwe na mboga mboga nyingi hasa jamii ya kabichi na nzuri zaidi za kuchemsha, na kama nyama basi upendelee zaidi kuku wa kienyeji au samaki wa kuchemsha au kuokwa , unaweza tupia na ndizi moja au mbili za kuchemsha, ;

6. Jioni kula chakula kabla ya masaa matatu hadi manne kabla ya kulala, ili unapoenda kulala chakula kiwe kimeshasagwa kabisa. Jaribu kuachana kabisa na ugali, wali na vyakula vya wanga usiku. Potezea tu na mboga mboga, matunda, unaweza tupia kipande cha kuku au samaki wa kuchemsha au kuokwa

7. Kunywa maji angalau lita moja na nusu kwa siku. Hayo maji siyo unayanywa kama bomba la mvua "gudugudugudu!" kwa wakati mmoja. Hakikisha unakuwa na chupa yako kubwa ya lita moja na nusu, mbili, mbili na nusu ambayo unajiwekea lengo la kuimaliza kwa siku

8. Lala usingizi angalau masaa saba, nane, kwa siku.

9. Tembea angalau nusu kwa siku haraka haraka na utoke jasho, siyo unatembea saa nzima halafu unatembea kama unasindikiza harusi. Hamna kitu hapo.

10. Kama umeolewa au una mtu wako ambao umpendaye kweli kweli na ni wako nasisitiza tena ni mtu wako siyo wa kuparamia basi usiwe na hiyana toa mzigo angalau mara nne kwa wiki; hii kitu hupunguza msongo wa mawazo ambao ukizidi husababisha mwili kunenepeana, vile vile ni mazoezi tosha ya viungo; ukipiga mzigo kisawasawa raundi moja ni sawa sawa na kupandisha ngazi kumi za ghorofa; sasa fikiria unaweza kuunguza calories ngapi kwa mwili wako kwa siku tena kwa njia ya raha na mustarehe?

11. Usiwe mtu wa stress, punguza stress ni sumu mbaya ndani ya mwili ambayo husababisha mwili kushindwa kufanya kazi yake vizuri. Weka furaha, amani, upendo pamoja na mambo yote yatuzungukayo.

12. Achana na mambo ya vinywaji vyenye sukari kama soda, juisi za viwandani, kula matunda tena matunda yasiyo na sukari nyingi labda kama uwe na matatizo mengine ambayo itakulazimu kula matunda hayo. Tunda liliwe dakika kumi mpaka kumi na tano kabla ya mlo.

13. Achana na mambo ya monde au pombe, kama unakamata kamata mara moja moja kama wikiendi pata mbili au tatu zinatosha na ziwe zile ambazo siyo makombora zenye sukari na wanga wingi (zenye carbs chache),Sitaki kuingia ndani huko maana ni biashara za watu! kama kuna muziki jiachie ni mazoezi tosha ya mwili na muziki husimumua akili na mambo mengine mwilini.
 
Mazoezi gani mkuu muda wote nipo job vyakula vya mafuta kuacha hilo lipo ndani ya uwezo wangu tuendelee wangu
Mazoezi ni mengi sana, na si lazima kwenda GYM.

Utakaporudi nyumbani kutoka kazini, muda tosha wa kufanya mazoezi unapatikana. Ni wewe mwenyewe kujiwekea ratiba.

Chumbani panatosha, na Mazoezi ya tumbo ni mengi sana, ngoja nikupe haya mepesi kwanza.

Unachotakiwa kufanya ukiwa chumbani au hata sebuleni ni wewe tu na maamuzi yako, muombe mtu wa kukuzuia miguu yako huku wewe ukiwa umekaa kitako, kisha anza kulala kinyume nyume kidogo, ukishafika chini jinyanyue tena.

Na hii si lazima uwe na mtu hata peke ako, tafuta sehemu ambayo utapenyeza miguu yako ili uweze kujinyanyua na kujirudisha taratibu, na vilevile ukishazoea uwe unajinyanyua kiubavubavu kisha ukijirudisha unajirudisha kwa kanuni ile ile ulioanza nayo, yaani unajirudisha kwa kujiweka sawa, na ukijinyanyua tena unaendelea kiubavubavu ukijirudisha kama nilivyoelezea hapo.

Sasa kwa vile wewe itakuwa ni mara ya kwanza inabidi usiende raundi nyingi, fanya hata kumi kumi kisha unapumzika japo dakika mbili au tatu kisha unaendelea.

Na kwa mtu kama wewe ambae hufanyi mazoezi siku ya pili utajisikia sana maumivu ya tumbo, usiogope inabidi uendelee kila siku mpaka utakapozoea hutohisi maumivu tena, na pia kuwa na utaratibu wa kujiwekea mapumziko japo kwa wiki mara moja, unajiwekea siku moja ambayo unapumzika/hufanyi mazoezi.

Na pia uwe unakunywa sana maji.

Na cha nyongeza, siri ya mazoezi ya tumbo mwanzoni tegemea kuharisha, na wala usiogope kama hali hiyo itakutokea, wewe endelea na mazoezi. Inategemea na tumbo la mtu waweza kuharisha au kutoharisha ila maumivu ya tumbo lazima, usiogope jiandae.

Ruka sana kamba, inasaidia sana kukufanya uwe mwepesi na kupunguza mafuta ya mwili kwa kiasi kikubwa.

Haya maelezo ninayoyatoa naona kama hayatoshi vile, ungekuwa karibu na mimi ningekupa mazoezi ya kutosha na nakuahidi baada ya wiki mbili tu ungeanza kuona mabadiliko
 
Back
Top Bottom