Jambo kwenu wanaJF.
Niende moja kwa moja kwenye maada,ifahamike ya kwamba huu mwezi tunauona unang'ara angani haupo peke yake kuna miezi mingi mingi tu (nimesahau idadi kamili),ila ni zaidi ya sita.
Ukitaka kuona mwezi/miezi (moons) fata hatua zifuatazo na zoezi hili lifanyike wakati wa jua kali;
1.Tafuta vipande saba vya vioo vyenye ukubwa ambao unashikika kwa mikono yako (hata kama ni 4cmx6cm).
NB:Vioo hivyo viwe vile ambavyo unaona upande wa pili (non-silvered) na visiwe vya plastic.
2.Tafuta vipande kumi na nne vya miti vyenye unene sawa na kidole chako cha kati na kila kimoja kiwe na urefu wa 8cm.
3.Weka kioo cha kwanza chini kisha weka vipande viwili vya miti juu ya kioo (vijiti viachiane nasafi na visigusane).
4.Weka kioo cha pili juu ya vipande vya miti (vile vya juu ya kioo cha kwanza).
5.Endelea kupanga vioo katika utaratibu huu hadi vioo vyote saba viishe.
6.Ukimaliza sasa vinyanyue na uvishike vioo vyote pamoja na miti yake kwa mikono miwili (Kuwa makini usiharibu huu mpangilio wa vioo na vijiti).
7.Vielekeze vioo pale katikati ya jua pale panapowaka sanaaa.
8.Chungulia katikati ya vioo mithiri ya kama unalenga shabaha katikati ya jua,chungulia kama kwa dakika 3,4,5...
9.Ukichungulia kwa makini sana hapo ndio utaona mwezi/miezi na unaweza ukaona hata miezi kumi na kuendelea na pia unawwza ukaona michache pia,hii ni kulingana na hali ya hewa na mwanga uliopo kutoka kwenye jua pia na wakati husika.
NB: Usitumie viooo vyenye lenzi sababu ni hatari kwa afya ya macho yako.
Ahsante wakuu,nawasilisha hii mungu akijalia tutaleta na zingine.