Jinsi ya kumtambua/kutofautisha njiwa dume na jike

Alphaking2023

JF-Expert Member
May 20, 2015
2,092
2,122
Kwa wale ambao mmewahi kufuga njiwa tupeane maarifa hapa unawezaje kutofautisha kati ya njiwa dume na jike?
 
kwa upande wa ndege asilimia kubwa madume ni warembo zaid ya majike so chunguza njiwa wako vzr utagundua madume yote ni mazur na wana rangi za kuvutia kuliko majike
Kuna njiwa nilokuwa nao hapa naona kama wote wanaendana endana ukubwa hadi urembo isipokuwa tu mmoja mweupe wengine wa blue sasa nashindwa kutofautisha yupi jike na yupi dume maana wapo watatu
 
Hilo ni kati ya vitu vigumu kidogo,hata waliosema kwamba utawatambua kwa kutizama anaempanda mwenzake ndio dume bado hicho sio kigezo,kwa wasio fahamu kwa njiwa hata jike anaweza kumpanda dume.

lakini chakuwastaajabisha kibisa dume nae anaweza kumpanda dume mwenzake na wakaishi kama wafanyavyo jike na dume na kama wanakiota huingiza majani kwa maandalizi yakutaga lakini kitakachotokea hawawezi kutaga.Hili mara nyingi hutokea kama wakati wakununua umechukua madume yote ukidhani ni jike na dume na mitaa ya jirani hakuna njiwa wengine.

Iko tabia nyingine ambayo mara nyingi hufanywa na madume ambapo dume hubalishia jike kwakuunguruma huku akimzungukazunguka jike.Njia hii nayo sio kigezo cha moja kwa moja kwani wakati mwingine hata jike naye anaweza fanya hivyo.

Njia nyingine ni kutizama tu maumbo yao(shape) na hii ndio mara nyingi nikichanganya hizo tabia nyingine hapo juu mimi huwatambua kwakuwatizama tu ambapo kimsingi inahitaji uzoefu mkubwa.
Asante.
 
Ni kweli kabisa mkuu nimeona hata hawa njiwa wangu wakichukua majani wote kutengenezea kiota lakini changamoto ni kuwa wapo watatu na watu husema kuwa njiwa wanatakiwa kuwa pair ndipo waweze kutaga niliwaza niongeze njiwa mmoja lakini naona kuwatambua imekuwa changamoto hadi nyie wazoefu ndo mwaweza
 
Hukuna namna hapo unatakiwa kufahamu jinsia ya huyo uliyenae ili umtafutie mwenza.

Kwa faida ya wasio fahamu njiwa huwa hawachangii dume kama ilivyo kwa kuku.Hata kama kuna njiwa wengi jirani usitegemee dume litoke huko mtaa wa pili lije kupanda tu kisha lirudi lilipotoka.Hapo lazima eidha jike ama dume lazima mmoja atahama kumfuata mwenzake na mara nyingi dume ndio hua na tabia yakuhama na kufuata jike.

Hivyo kuwa makini inawezekana kabisa huyo njiwa siku akahama na usifahamu amehamia wapi akapotea.
 
Pole sana kwa changamoto hiyo, fanya hivi, mchukue njiwa mning'nize juu kwa kumshika mdomoni , mmoja ukimshika hivyo anapigapiga sana mabawa, mwingie anakua mtulivu, enzi zetu za ufugaji tulifanya hivyo!
So anaekuwa mtulivu ndo jike si ndio
 
Hukuna namna hapo unatakiwa kufahamu jinsia ya huyo uliyenae ili umtafutie mwenza.

Kwa faida ya wasio fahamu njiwa huwa hawachangii dume kama ilivyo kwa kuku.Hata kama kuna njiwa wengi jirani usitegemee dume litoke huko mtaa wa pili lije kupanda tu kisha lirudi lilipotoka.Hapo lazima eidha jike ama dume lazima mmoja atahama kumfuata mwenzake na mara nyingi dume ndio hua na tabia yakuhama na kufuata jike.

Hivyo kuwa makini inawezekana kabisa huyo njiwa siku akahama na usifahamu amehamia wapi akapotea.
Kama nikigundua wote ni madume nikimleta jike mmoja atapandwa?
 
Njiwa ni ndege wa tofauti kidogo,hata kama utaleta dume leo usitegemee kesho tu kuona wanapandana,kwanza wataanza mahusiano ndipo wapandane.

Kumbuka nilikwambia njiwa huwa wanaishi wawiliwawili.Hivyo lazima kwanza kuwe na maafikiano yakuishi pamoja ndipo hayo yakupandana yatafuta.Njiwa sio kama kuku wao wapo tofauti sana.Kwa kiasi kikubwa njiwa wanashabiliana sana na kanga
 
Back
Top Bottom