GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 4,893
- 6,647
Mwanaharakati maarufu wa Marekani, Dr. Martin Luther King Jr. alishawahi kusema, "An idle mind is the workshop of the devil!". Mtu mmoja anisaidie kutafsiri kwa Kiswahili, tafadhali!π
Namna pekee ya kuiepusha akili kuwa "idle" ni kwa kuifanyisha kazi nzuri, na ili akili iweze kufanya kazi nzuri ni lazima uilishe taarifa nzuri kila siku.
Njia gani bora ya kuilisha akili ya mwanao taarifa nzuri zaidi ya vitabu vizuri?
Unaweza kumzoesha kuwa msomaji kwa kutumia njia zifuatazo:
1. Msomee kitabu kila siku mpaka atakapoweza kujisomea mwenyewe
Hili linaweza likafanyika tokea mtoto akiwa tumboni mwa mama yake. Tafuta vitabu vizuri na uanze kumsomea kwa sauti. Usifikiri kwamba haelewi. Utakachokuwa unakifanya kitakuwa kinarekodiwa kwenye akili yake, na kuchochea aina ya tabia atakayokuwa nayo maishani mwake.
Atakapozaliwa, uendelee kufanya hivyo. Mnaweza mkapeana zamu na mwenzi wako kumsomea kitabu Usiku wakati wa kulala, kwa kumsomea kwa sauti hadi asinzie.
2. Hakikisha kuna vitabu vya kutosha vya aina mbalimbali nyumbani kwako. Muhimu, vitabu hivyo viwe ni vitabu vizuri. Jihadhari na vitabu vinavyoweza kuwa hatari kwa afya ya akili ya mtoto.
3. Jijengee tabia ya kujisomea vitabu kila siku ukiwa naye. Wanasema, "like the father, like the son". Watoto wana tabia ya kuwaiga wazazi wao.
4. Mnunulie zawadi ya kitabu kila baada ya muda fulani, au wakati wa tukio fulani zuri. Kama una kawaida ya kumfanyia "birthday", usiishie tu kumlisha ngano na kuku, mpatie zawadi ya kitabu kizuri.
Ni gharama na usumbufu kufanya hivyo? Vyo vyote vile, lakini kama hiyo itamsaidia mwanao, kwa nini usifanye? Isitoshe, hautawafanyia hivyo milele. Wakishajua kusoma na kuandika, watakuwa wakijisomea wenyewe. Na itakuwa rahisi zaidi wao kufanya hivyo ikiwa ulishawazoesha tokea wakiwa watoto wachanga.
Ukiona vyaelea, ujue vimeundwa!
Unafikiri ni mbinu gani tena itakayomsaidia mtoto kuwa msomaji wa vitabu?
Hongera mkuu, ila usiache kuwa na TV. Watoto wanaweza kutorokea kwa jirani kuangalia tv. Muhimu ni kuthibiti matumizi yake huku ukiendelea kumjengea tabia ya usomaji.Mfano Mimi Napenda Sana kusoma kuliko kutazama Tv hivyo Mimi nyumbani kulikuwa hamna Tv hiyo ilinijenga kupenda kusoma Sana Hadi leo
Ila ukiwa bookworm unafikia malengo yako haraka Sana na kuishi kwa uhuru ,upendo na Amani Sana . Binafsi mtoto wangu lazima nimjenge Apende kusoma VITABU njia mojawapo sinunui Tv nanunua Vitabu na radio na laptop Basi tu namuwekea Movie zakumjenga na soft copy books basi
Kumbe! Nilifikiri ni wa Dr. Martin.Siyo msemo wa Luther, ni Msemo wa wazungumzaji wa Kingereza (English Saying) akiwemo Dr. Martin.
Ni kweli! Pesa ni kihamasishi kisichobagua umri. ShukranπRahisi tu mbona,hakuna MTU asiependa Fedha,kwa watoto Zawadi..Nunua Kila kitabu atakachomaliza kusoma kwa makubaliano ya pesa fulani or kumpatia Zawadi ambayo unamuahidi kuwa endapo atamaliza kusoma basi utampatia..
Hiyo ni baada ya kukueleza NN alichosoma na ameelewa NN Ktk hicho kitabu,n'a kwa vile ww mzazi pia ni msomaji WA vitabu inakuwa rahisi Kujua kama anachosema ni Kweli ama Laa..
Utaingia gharama kwa kipindi fulani anapoanza kujisomea Ili apate hizo Fedha or hizo Zawadi Ila utamu WA vitabu ukimnogea Hilo zoezi linakuwa halipo tena..
Nothing comes at easy,kama unavyotongoza tu Mwanamke unavyojikakamua mwanzoni Ili uonekane uko Vizuri kabla hujampata Ila ukishampata unarudi kwenye uhalisia wako,ndivyo hivyo hivyo tu Comrade..tumia approch hiyo.
Sikumbuki kama nilishawahi hata kusikia kuhusu hayo madarasa! Yalikuwaje?Hivi library hakuna yale madarasa ya jumamosi ya watoto. Zamani nilikuwa nampeleka dogo kila jumamosi anaimba na kusoma pale mpaka saa sita. Ile ilimjenga akawa msomqji mzuri wa vitabu.
Mkuu,nunua vyote.Mfano Mimi Napenda Sana kusoma kuliko kutazama Tv hivyo Mimi nyumbani kulikuwa hamna Tv hiyo ilinijenga kupenda kusoma Sana Hadi leo
Ila ukiwa bookworm unafikia malengo yako haraka Sana na kuishi kwa uhuru ,upendo na Amani Sana . Binafsi mtoto wangu lazima nimjenge Apende kusoma VITABU njia mojawapo sinunui Tv nanunua Vitabu na radio na laptop Basi tu namuwekea Movie zakumjenga na soft copy books basi
Mimi mwenyewe nilikuwa member miaka ile nipo shule ya msingi na huyo dogo ni miaka 2006 tuu hapo.Sikumbuki kama nilishawahi hata kusikia kuhusu hayo madarasa! Yalikuwaje?
Vipi dogo, aliweza kuendelea na hiyo tabia ya usomaji?
Very inspiring! CongratulationsππππMimi mwenyewe nilikuwa member miaka ile nipo shule ya msingi na huyo dogo ni miaka 2006 tuu hapo.
Jumamosi watoto wa shule mbali mbali walikutana kuimba na kusoma vitabu asubuhi kuanzia saa tatu mpaka saa sita.
Mimi mwenyewe mpaka leo nasoma vitabu mfano votabi vyooote vya willy gamba nimevinunua na kurudia kuvosoma mara kadhaa. Sababu vilikuwa library enzi zile..
Dogo anasoma vitabi mpaka kesho na kwa sasa ni Engineer huko Afrika magharibi.
βMkuu,nunua vyote.
Ukimzuia mtoto wako kula nyumbani ni kwamba wewe umeamua kumnyima chakula chako (mchoyo) hivyo atapewa chakula na jirani yako.
Vitu vingi pamoja na kwamba tabia hutegemea mazingira (mazoea) ila pia kupenda jambo flani ni asili ya mtu (nature (in born).
Si unajua ukiandika kwa simu pole. Na asante kwa pongezi.Very inspiring! Congratulationsππππ
NB. Kuna typing error kama 2 hivi kwenye comment yako:
1. Votabi
2. Vitabi
Lakini imeeleweka kuwa ulimaanisha VITABU!
πππ
πππSi unajua ukiandika kwa simu pole. Na asante kwa pongezi.
Nilikua msomaji mzuri ila sasa nimepoteza hamu ya kusoma kabisa nmekua mvivu sjui narudi vipMfano Mimi Napenda Sana kusoma kuliko kutazama Tv hivyo Mimi nyumbani kulikuwa hamna Tv hiyo ilinijenga kupenda kusoma Sana Hadi leo
Ila ukiwa bookworm unafikia malengo yako haraka Sana na kuishi kwa uhuru ,upendo na Amani Sana . Binafsi mtoto wangu lazima nimjenge Apende kusoma VITABU njia mojawapo sinunui Tv nanunua Vitabu na radio na laptop Basi tu namuwekea Movie zakumjenga na soft copy books basi
Ni rahisi sana!Nilikua msomaji mzuri ila sasa nimepoteza hamu ya kusoma kabisa nmekua mvivu sjui narudi vip
No siwezi shindwa ngoja nitafanyia kazi ushauri wako mkuuπNi rahisi sana!
1. Kika siku uamkapo, panga ratiba ya siku nzima (andika), na uhakikishe unajumuisha na alau lisaa kimoja la kusoma. Huo muda wa kusoma ukiwadia, tafuta sehemu ya "kujichimbia" na hakikisha hutoki mpaka muda uishe. Katika kipindi cha hilo lisaa kimoja, hakikisha unatumia kusoma na di vinginevyo. Soma hata kama ni kwa kuilazimisha.
2. Kuja utokapo nyumbani kwako, hakikisha una kitabu mkononi. Uzuri mmoja siku hizi kuna vitabu vya soft copy. Upatapo upenyo, uteseme upo kwenye daladala, ndege, su unasuburia kuingia kwenye ofisi fulani, uutumie huo muda kusoma, hata kama utasoma ukurasa mmoja tu.
Utashindwa kufanya hivyo?
πππππͺNo siwezi shindwa ngoja nitafanyia kazi ushauri wako mkuuπ