Jinsi ya kula na kulala bure jijini Dar es Salaam

Jinsi ya kula na kulala bure jijini Dar es Salaam

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
19,943
Reaction score
37,825


1.Asubuhi nenda kwenye hoteli ya hadhi ya kati kama vile pale Rombo Green View Hotel kwa wanaoishi maeneo ya Sinza. Asubuhi huwa wanatoa breakfast kwa watu walio lala. Ukifika we jifanye ulilala hapo usiku.


2. Mchana tafuta sehemu ambako kuna msiba, ukifika jifanye muombolezaji, wakati wa maakuli ukifika utakula hapo mchana utapita.

3.Usiku nenda kwenye bar zinazo kasha, kama vile kona bar nakadhalika. Nunua soda ya shilingi Mia Saba, kisha kaa hapo hadi kuche. Kama ukiona hauna hiyo mia saba, tafuta kopo dogo la maji ya uhai, kisha weka maji ya bombani halafu ukifika hapo ujifanye mteja umenunua maji hayo hapo hapo. Utakaa hapo mpaka, asubuhi. Ukiona usingizi umekuzidia sana, sinzia kiaina kwa staili ya kulala kwenye meza.

4. USAFIRI : Kusafiri bure kwenye daladala ni rahisi sana. Panda kwenye daladala kisha uchune, konda ikifika zamu yako kulipa, mwambie konda wewe ni staff. Akikuuliza staff wa nani, taja jina lolote unalolijua halafu uwe serious. Unashauriwa kufanya research yako mapema kubaini majina ya madereva na makonda kadhaa wa route tofauti tofauti za Dsm.

Ukitaka iwe rahisi zaidi kwako, kupanda daladala bure, ukisha panda, mchangamkie sana konda na dereva na uwe unawapagisha stori za magari magari, matrafiki, gereji nakadhalika. Akitokea mtu akamzingua konda, ungana na konda kumzingua huyo jamaa. Na likitokea tatizo lolote barabarani kama vile gari mnalopisha nalo kutaka kusababisha ajali etc, ungana na dereva kumzingua huyo jamaa wa gari jingine.

FANYA HIVI MPAKA HAPO MAMBO YAKO YATAKAPO KUWA MAZURI .


N.B : KAMA UNATAKA KUWA NA UWEZO WA KULA BURE,KULALA BURE, KUPATA HELA NYINGI BILA KUFANYA KAZI YOYOTE , ETC. MTAFUTE MDUDU ANAITWA " KIBIRINGISHA MAVI " HALAFU UNITAFUTE, NIKUPELEKE KWA MTU AKUTENGENEZEE UCHAWI WA KUFANIKISHA SUALA HILO.
 
duh!ila hii haimjengi mtu mkuu,kuna viwanda kadhaa vya biscuit mwenge,sabuni buguruni au TOT unaweza kuwa japo kibarua!
 
Yakulala hotelini ni ngumu mkuu kwani wanauliza number ya chumba ulicholala
 
Hiyo ya kuzuga umelala hoteli ili upate breakfast imekaa poa sana hiyo(In Joti's voice)
ila ya kupanda daladala unaweza kuchezea manundu!


Hata hiyo waweza kujikuta unaosha masufuria ya hoteli siku nzima, watakustukia tu. Njia ya mkato mara nyingi huwa ina gharama zake mkuu.
 
Hahahaaa huyo mdudu vilingisha mavi naweza kumpata niambie jinsi ya kutengeneza dawa

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Wewe. Mbona utawafanya vijana wengi kuja Dsm waishie kulala chini ya madaraja?
 
ukitaka kusafiri bure fanya hivi. tufanye unatoka mwenge manyanya. ukifika manyanya mwambie konda umebanwa na haja ukachimbe dawa na nauli unayakuendea tu.
 
tabia za ki..sho..ga hizo. ule bure ulale bure ili iweje sasa.? siku ukigundulika tabia yako ukaombwa mini kabang utakataa.?
 
Back
Top Bottom