Jinsi ya kula na kulala bure jijini Dar es Salaam

Jinsi ya kula na kulala bure jijini Dar es Salaam

Likud shida ni nin?? Hahahaha

Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk
 
The guy has a point hasa unapotaka kupanda daladala bure. mtu akimzingua konda uwe upande wa konda au dereva
 
Sasa mkuu mabibi utapataje bure ? maana kuna waqt akili yoote inahamia kwenye zipu.
 
Hongera kwa kutupa hiyo mbinu ya kuishi kimjinimjini. Leo nimeifanya na kufanikiwa kwa kupanda daladala 6 bila ya kulipa nauli. Niliona ni vema ni-test hiyo hypothesis. Nasema big up sana. Endelea kutujuza na mengineyo pia.
 
Bangi mbichi n hatar kwa ubongo


Sent from my iPhone using JamiiForums.🔩🔨
 
Hii mada Bwana Likud ni majanga tu. Haijengi mtu. Inatia uvivu na kutofikiria kufanya kazi.
 
mchangamkie
sana konda na dereva
na uwe unawapagisha
stori za magari magari,
matrafiki, gereji
nakadhalika. Akitokea
mtu akamzingua konda,
ungana na konda
kumzingua huyo jamaa.
Na likitokea tatizo lolote
barabarani kama vile
gari mnalopisha nalo
kutaka kusababisha ajali
etc, ungana na suka na konda.

HAYA NDIO MAWAZO YA GREAT THINKERS WA LEO
 
kwa hapa mwanza, tafuta jezi hasa shati, utapanda kila daladala hapa mwanza, wee sema me ni member.
 


1.asubuhi nenda kwenye hoteli ya hadhi ya kati kama vile pale rombo green view hotel kwa wanaoishi maeneo ya sinza. Asubuhi huwa wanatoa breakfast kwa watu walio lala. Ukifika we jifanye ulilala hapo usiku.


2. Mchana tafuta sehemu ambako kuna msiba, ukifika jifanye muombolezaji, wakati wa maakuli ukifika utakula hapo mchana utapita.

3.usiku nenda kwenye bar zinazo kasha, kama vile kona bar nakadhalika. Nunua soda ya shilingi mia saba, kisha kaa hapo hadi kuche. Kama ukiona hauna hiyo mia saba, tafuta kopo dogo la maji ya uhai, kisha weka maji ya bombani halafu ukifika hapo ujifanye mteja umenunua maji hayo hapo hapo. Utakaa hapo mpaka, asubuhi. Ukiona usingizi umekuzidia sana, sinzia kiaina kwa staili ya kulala kwenye meza.

4. Usafiri : Kusafiri bure kwenye daladala ni rahisi sana. Panda kwenye daladala kisha uchune, konda ikifika zamu yako kulipa, mwambie konda wewe ni staff. Akikuuliza staff wa nani, taja jina lolote unalolijua halafu uwe serious. Unashauriwa kufanya research yako mapema kubaini majina ya madereva na makonda kadhaa wa route tofauti tofauti za dsm.

Ukitaka iwe rahisi zaidi kwako, kupanda daladala bure, ukisha panda, mchangamkie sana konda na dereva na uwe unawapagisha stori za magari magari, matrafiki, gereji nakadhalika. Akitokea mtu akamzingua konda, ungana na konda kumzingua huyo jamaa. Na likitokea tatizo lolote barabarani kama vile gari mnalopisha nalo kutaka kusababisha ajali etc, ungana na dereva kumzingua huyo jamaa wa gari jingine.

Fanya hivi mpaka hapo mambo yako yatakapo kuwa mazuri .


n.b : Kama unataka kuwa na uwezo wa kula bure,kulala bure, kupata hela nyingi bila kufanya kazi yoyote , etc. Mtafute mdudu anaitwa " kibiringisha mavi " halafu unitafute, nikupeleke kwa mtu akutengenezee uchawi wa kufanikisha suala hilo.

janga la kitaifa
 
Back
Top Bottom