Jinsi ya Kuibadili Tanzania kuwa ulimwengu wa pili

Nathan Jr

JF-Expert Member
Sep 14, 2017
1,437
1,875
Ndugu zangu wana intelligence Nina wazo muhimu ambalo linaweza kubadili Tanzania kuwa katika ulimwengu wa pili au wa kwanza kabisa,

Hii anatakiwa kuwa mwendelezo kabisa siyo suala la kukurupuka Mara moja,

Suala ili lilitiwa timing iwe wakati wa Jakaya Mrisho Kikwete,

Pale suala muhimu ilipaswa liwe viwanda kila sehem, na viwanda havitatokea kwa kutamka tu majukwaani ni mbinu thabiti ambazo haziingiliani na kupendwa kisiasa, bali ukweli,

ELIMU INAYOENDANA NA WAKATI

shule zetu za primary zingeendelea kama kawaida na mitaala tuliyonayo ila wakati wa kwenda secondary wangefanya yafuatayo katika kuwachagua wanafunzi kuendelea na masomo

Yangetengwa madaraja yafuatayo

Daraja A ni wale waliopata 120 out of 150 hapa nimebase kwa wale waliokuwa wanaofanya masomo matatu, hesabu, lugha na maarifa ya jamii, (kipindi elimu bado ni elimu)
Hawa wangeenda direct secondary kwenye shule zile zetu za zamani za kufaulu kama kawaida, hawa baadae wawe viongozi na wanaoratibu shughuli za Maendeleo katika managerial level watakapofika vyuo vikuu

DARAJA B 100 hadi 120

Hawa waende shule za kufaulu lakin za kawaida Ambazo wengi wao wanaweza kufika juu wanaweza wasifike degree au elimu ya juu zaid, ila elimu wanayopewa iwe semi tertiary education, ( elimu ya vitendo 50% na ya darasani 50%)
Hawa watakuja baadae kushika nafasi za middle managerial posts au supervisors,

Sasa daraja C 50 hadi 100

Hawa waende shule za ufundi wote nchi nzima, wajifunze jinsi ya kutengeneza vitu mbali mbali kuliko kukalili Archimedes principals Ambazo haisaidii chochote,

Sasa basi zile shule za kata nchi nzima walikosea waliozianzisha , wangejikita zaid katika uanzishaji wa vyuo vya ufundi nchi mzima na kupata msaada wa vifaa kutoka China na kwingine duniani, wangeleta wachina wengi kuwafundisha vijana kazi na ufundi, hii ingesaidia sana vijana kwanza kupunguza uzembe wa kifikiria kuajiriwa, na kupunguza ushindani usio wa maana kwenye soko la ajira, maana unakua. Mtu ambaye hata hafai kabisa ila kwa kuchechemea alifika chuo kikuu hakuna analojua, naye anapeleka CV kwa tangazo la kazi ,kuongeza ushindani usio wa maana,

Hapa zile shule 4000 ningekuwa vyuo vya ufundi na katika kila tarafa kukawepo na shule ya secondary moja tu, isiwe kila kata,

Kupitia mpango huu Tanzania tutazalisha vitu vyetu wenyewe na kuvitumia,

SIASA ISICHANGANYWE NA UHALISIA WA MAISHA

kwanza elimu kipindi cha nyuma hasa kwa kikwete alifanya elimu kama ngazi ya kudanganya wananchi kuwa tumeongeza vyuo vikuu, kumbe havikukidhi malengo au sifa, ila anataka tu idadi ionekane yeye ameacha vyuo vikuu vingi zaid, suala ambalo limeua elimu yetu,
Jingine viongozi wakubwa kulazimisha ndugu na jamaa zao kudahiliwa katika vyuo mbali mbali bila sita stahiki, nayo ilileta shida mnoo,

Suala au Jambo kingine ni kuogopa kuwa sema wazembe kwa kuogopa kuchukiwa kisiasa au kukosa Kura kwa awamu ya pili,
Hapa watu wengi wameharibu nchi sana,

SHERIA ZA UWEKEZAJI NA MADINI

hapa uwekezaji apewe masharit kwamba kama ni muwekezaji sawa unataka Tupate 10% tu ya faida yote OK hatuna shida ila kila.muwekezaji eneo alipo ajenge au kurekebisha miundombinu mbali mbali kama mabweni, kama madarasa, kama hospital na huduma za jamii,

Sheria Kali ya kuwanyonga wote watakao onekana kuwa wabadhirifu wa Mali za umma,

KUPIGWA MARUFUKU BIDHAA ZA NJE, kuna baadhi ya bidhaa si muhimu kuingiza nchini hivyo ili kulinda soko la ndani tunabidi kupiga marufuku bidhaa hizo,

KUKARIBISHA UWEKEZAJI KATIKA MIRADI MIKUBWA

ujenzi wa viwanda vya kuunganisha magari ,kuunda pikipiki, kuunda vyerehani, nashangaa wakati wa Nyerere tulikuwa na kiwanda cha redio NATIONAL , baiskeli swala, kuunganisha vichwa vya scania lakin muda huu tunaangaika na viwanda vidogo vidogo vya matofari,

Njia zipo Nyingi tuungane
 
kuhusu kuzuia bidhaa za nje ni lzm uwe na uhakika kuwa hizo bidhaa unazozuia lzm ziwe zimeanza kuzalishwa nchini kwako na kwa ubora stahiki,alasivyo yatakuwa ya sukari 5000 kilo:D tunakuza uchumi wa nchi:D
Kwenye swala la uongozi ni lzm kuangalia weledi,hekima,utimamu na uzalendo si uniambie ati waliopata 150-120 ndo wanatakiwa wawe viongozi hapana,watu tunatofautiana vipaji,kuna watu hawakusoma sana lkn wameibadili dunia kiasi kikubwa sana.
Kwenye suala la vyuo nipo nawe 100%..
Nafikiri kwa nchi yetu hata tukiegemea kilimo kiudhatiti hatuitwi maskini tena,sera mipango na utekelezaji ndio nyezo ukijitambua.
 
Kabisa ni mawazo mazuri mno
 
Ipo vizuri, sema hii mifumo yetu ya elimu ni agenda za wazungu ndo maana haibadilishwi..
 
Kuhusu siasa kutochanganywa na maisha Nadhani ni gumu kuliko yote hayo.......kwa maana siasa ni maisha...
 
Siasa iwe siasa. Ila mwanasiasa asiwe ndie mchumi wa kupanga mipango, asiwe mwanasheria wa kujivunjia mikataba hovyo, asiwe igp wa kutaka nani awekwe ndani na kunyanyaswa. Abaki na siasa yake ila akae na wote wenye taaluma zao na kuangalia masualaa ya nchi yanaenda aje na kushauriana nao juu ya kuyaboresha.
Msisitizo wa elimu ya ufundi iwe ni kipaumbele. Kuliko kuwaleta wachina wengi, tungepeleka WaTz wengi nje kupata ujuzi, wataalamu wachache kutoka nje waletwe pale kwenye mambo mkubwa kama kufunga mitambo na washirikiane/ kuwaelekeza wa kwetu jinsi ya utunzaji na kufanyia matengenezo.
Mambo yanayosikitisha ni kwamba nchi haina dira ya muda mrefu, leo viwanda vinashadidiwa majukwaani, lakini ukweli ni kuwa 1985 kulikuwa na viwanda vya kumwaga si vya vibiriti, batteries, magurudumu, makaratasi/daftari, kalamu, radio, majiko, taa za chemli, baiskeli, nguo/vitambaa, viatu/ngozi, plastic(ndoo/vyombo vya ndani n.k) mbao, vyuma, chokaa na cement, uzalishaji, sabuni zote, mafuta ya kujipaka, ya kupikia, vya maziwa, pembejeo za kilimo, mbolea, yaani karibu kila idara ilikuwa na kiwanda kinachozalisha vifaa husika. Vimeachwa na kufia mbali so wananchi wala viongozi walioona kuwa tunaelekea siko , leo tunakurupuka ili tuanze upya. Ipitiwe historia na kuangalia viwanda vile vilianzishwa kwa muda gani na nini kilipelekea hadi kupotea kwake. Ili makosa yasirudiwe tena kama kuna nia ya dhati. La sivyo siasa ikiendekezwa, kama ilivyo kwa umasikini na ujinga kuwa mtaji wa wasiasa wa nchi hii, basi na suala la viwanda litaongezwa katika hiyo orodha, mwanasiasa wakipata uhakika wake wa kuwa madarakani kwa kutumia kauli mbiu hiyo, anaondoka, hakuna lolote lililotekelezwa, akija mwingine, anakuja na uzushi wake, itabakia Tz ya kuchezewa na wanasiasa na wananchi hawajitambui.
 
Elimu tunayofundishwa iliandaliwa kwa mpango na maono yao binafsi ili tutumwe kutokana na mahitaji yao swala la muhimu ni kujua kusoma na kuandika alafu turudi kwenye uhalisia mtoto ajifunze mambo yaliopo nchini mwake na si kuandaa kutumwa
 
SIASA ISICHANGANYWE NA UHALISIA WA MAISHA

kwanza elimu kipindi cha nyuma hasa kwa kikwete alifanya elimu kama ngazi ya kudanganya wananchi kuwa tumeongeza vyuo vikuu, kumbe havikukidhi malengo au sifa, ila anataka tu idadi ionekane yeye ameacha vyuo vikuu vingi zaid, suala ambalo limeua elimu yetu,
Jingine viongozi wakubwa kulazimisha ndugu na jamaa zao kudahiliwa katika vyuo mbali mbali bila sita stahiki, nayo ilileta shida mnoo,

Suala au Jambo kingine ni kuogopa kuwa sema wazembe kwa kuogopa kuchukiwa kisiasa au kukosa Kura kwa awamu ya pili,
Hapa watu wengi wameharibu nchi sana,

Njia zipo Nyingi tuungane

Hapo kwenye siasa kwa nchi zetu Africa inakua tabu kidogo, kwa kuwa sisi wenyewe tumewakabidhi uaminifu mkubwa wanasiasa na wao kutufanya wanavyotaka.
Vile vile wanasiasa ni watu ambao siku zote mtaji wao ktk mafanikio ni watu ambao Lazima wahakikishe wanafanywa kuwa Wateja wao ktk sanduku la kura. Kwa hiyo ndo hao ambao husema maisha bila siasa haiwezekani.
Lakini maisha ukichanganya na siasa ni sawa na kuchanganya "sukari na chumvi".
 
Ni kweli. Mkuu
Hapo kwenye siasa kwa nchi zetu Africa inakua tabu kidogo, kwa kuwa sisi wenyewe tumewakabidhi uaminifu mkubwa wanasiasa na wao kutufanya wanavyotaka.
Vile vile wanasiasa ni watu ambao siku zote mtaji wao ktk mafanikio ni watu ambao Lazima wahakikishe wanafanywa kuwa Wateja wao ktk sanduku la kura. Kwa hiyo ndo hao ambao husema maisha bila siasa haiwezekani.
Lakini maisha ukichanganya na siasa ni sawa na kuchanganya "sukari na chumvi".
 
Siasa iwe siasa. Ila mwanasiasa asiwe ndie mchumi wa kupanga mipango, asiwe mwanasheria wa kujivunjia mikataba hovyo, asiwe igp wa kutaka nani awekwe ndani na kunyanyaswa. Abaki na siasa yake ila akae na wote wenye taaluma zao na kuangalia masualaa ya nchi yanaenda aje na kushauriana nao juu ya kuyaboresha.
Msisitizo wa elimu ya ufundi iwe ni kipaumbele. Kuliko kuwaleta wachina wengi, tungepeleka WaTz wengi nje kupata ujuzi, wataalamu wachache kutoka nje waletwe pale kwenye mambo mkubwa kama kufunga mitambo na washirikiane/ kuwaelekeza wa kwetu jinsi ya utunzaji na kufanyia matengenezo.
Mambo yanayosikitisha ni kwamba nchi haina dira ya muda mrefu, leo viwanda vinashadidiwa majukwaani, lakini ukweli ni kuwa 1985 kulikuwa na viwanda vya kumwaga si vya vibiriti, batteries, magurudumu, makaratasi/daftari, kalamu, radio, majiko, taa za chemli, baiskeli, nguo/vitambaa, viatu/ngozi, plastic(ndoo/vyombo vya ndani n.k) mbao, vyuma, chokaa na cement, uzalishaji, sabuni zote, mafuta ya kujipaka, ya kupikia, vya maziwa, pembejeo za kilimo, mbolea, yaani karibu kila idara ilikuwa na kiwanda kinachozalisha vifaa husika. Vimeachwa na kufia mbali so wananchi wala viongozi walioona kuwa tunaelekea siko , leo tunakurupuka ili tuanze upya. Ipitiwe historia na kuangalia viwanda vile vilianzishwa kwa muda gani na nini kilipelekea hadi kupotea kwake. Ili makosa yasirudiwe tena kama kuna nia ya dhati. La sivyo siasa ikiendekezwa, kama ilivyo kwa umasikini na ujinga kuwa mtaji wa wasiasa wa nchi hii, basi na suala la viwanda litaongezwa katika hiyo orodha, mwanasiasa wakipata uhakika wake wa kuwa madarakani kwa kutumia kauli mbiu hiyo, anaondoka, hakuna lolote lililotekelezwa, akija mwingine, anakuja na uzushi wake, itabakia Tz ya kuchezewa na wanasiasa na wananchi hawajitambui.
Ni hakika Nyerere alituachia viwanda vingi nadhani vimekufa 1995
 
Viwanda:
1. Naona matajiri wanakimbia sera hii kutokana na kuogopa kuingia hasara kwa kuwapo na gharama kubwa za uanzishwaji na uendeshwaji kiwanda, wasiwasi wa upatikanajinwa rasilimali ya kutosha na soko la kuridhisha. Mtu anaweza kudiriki kuagiza mzigo mkubwa kutoka nje na akauza hapa kwa bei nafuu kuliko kuanzisha kiwanda hapa.
-Ili kushawishi sera za viwanda kufanikiwa serikali itabidi kuweka sera rafiki za viwanda vidogo, vya kati na vikubwa.
-Kuweka mpango mkakati, kuhimiza na kusmamia wa kila mkoa au kanda kuwa na uzalishaji wa rasilimali za viwandani vya kutosha mfano mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi, chuma, madini zingine, pamba, katani, rubber n.k.
-gharama za uanzishwaji na uendeshwaji upungue kama kuvuta umeme sehemu husika, umeme wa uhakika na bei nafuu zaidi, huduma ya maji, kupunguza kodi za mashine za viwandani, unafuu wa cement.
-kuondoa urasimu mbovu wa kiserikali na kupunguza kodi za uendeshaji. Na zaidi ya hapo kuwepo na ofisi moja ya kulipia kodi na tozo zote hizo na mfumo uliokuwa rahisi mf. bank, mobile banking.
-serikali za mitaa(manispaa, wilaya) au wizara zingine na wizara ya viwanda na biashara ziwe na mfumo mmoja wa mawasiliano na usimamizi kwa wenye viwanda. sio kila mmoja anakurupuka na sheria zake na kumbana mwenye kiwanda.
-Veta na vyuo vya ufundi na technolojia, na vyuo vya Tanzania vinatakiwa viende na wakati na hasa katika sera mpya hii ya viwanda. Kutangaza kozi za maabara za viwandani, civil and mechanical engineering, ufundi, information technology, occupational safety, industrial pharmacy, chemical engineering, computer engineering, n.k. na kozi hizi ziwe katika ngazi zote yaani certificate, diploma na degree ili ijenge Wafanyakazi wenye ujuzi.
- kuhusu masoko ni serikali kusimamia ubora wa bidhaa ambayo tayari inayo taasisi ya kusinamia hilo
-kuongeza ushindani kwa kufunguliwa kampuni zaidi ya moja
-Miundombinu ya mawasiliano naona imeendelea nchini
-barabara zote za nchini kuingia East, central na southern africa ziboreshwe kwa njia ya lami ambayo nimeona serikali imejitahidi kuboresha hapo.
-miundombinu ya usafiri wa majini hasa ziwa victoria bado( kuonganisha kenya na uganda); ziwa tanganyika(DRC,Burundi,Zambia) na Nyasa(Malawi). Ila hasa Reli ndio muhimu zaidi kusafirisha mizigo mingi kwa bei nafuu. Reli kwenda Rwanda-Burundi-Mozambique,Uganda.
-Kuboresha viwanja vya ndege vyenye hadhi ya kupokea ndege za mizigo katika mikoa yenye viwanda vikubwa vingi.
- sera ya afrika mashariki ya fair competion of goods.

Kwa kifupi, Sera ya viwanda ni nzuri ambayo inahitaji kuingiliana kwa wizara karibia zote ikiisaidia wizara ya viwanda kutengeneza mikakati, sheria, kanuni na utaratibu wa namna ya kuitekeleza ili iwaridhishe wadau.

Elimu ntachangia siku nyingine.
 
Mfumo wako wa elimu ni wa kibaguzi, sio mzuri kwa afya ya akili ya mwanafunzi
 
Back
Top Bottom