Jinsi ya kugandisha maziwa ya mgando ili yasitengane na maji

NOTREGISTERED

Member
Oct 14, 2015
20
5
Waungwana habari za leo.

Kwa wale wafugaji wa ng'ombe na wajuzi wa maziwa, naomba kujulishwa njia nzuri ya kugandisha maziwa ambayo hayatajitenga na maji.

Kwa sasa nagandisha maziwa kwa kuyachemsha afu yakipowa nayaweka kwenye ndoo safi nachanganya na maziwa mgando kwa ratio kama ya lita 5 fresh kwa 0.25 lita mgando alafu nayaacha kwa siku moja au mbili.
Sasa shida ni kuwa yakiganda yanajitenga na maji, na maji kuwa mengi kuliko maziwa. Naomba kujua nakosea wapi katika ugandishaji huu.
 
ninachojua maziwa yana 85% ya maji,na yanapoganda lazima maji yajitenge kwamba yatakuwa chini na maziwa juu.Ukilazimisha kuyachanganya basi hayatakuwa mazito na ladha yake haitakuwa nzuri na kuharibika ni mapema sana.
 
Back
Top Bottom