Jinsi ya kufanya uchapishaji binafsi (self pulbishing)

mapenz matam

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
214
254
Wakuu habari za jioni. Naomba mods msiunganishe uzi huu na nyuzi nyingine kwani huu ni special kabisaa

JINSI YA KUFANYA UCHAPISHAJI BINAFSI (SELF PULBISHING)

UTANGULIZI
Ni ndoto ya watu wengi sana kuchapisha vitabu vyao na kuwafikia hadhira husika. Ila tafiti zinaonesha kuwa ndoto hizi hufutwa na changamoto mbali mbali zinazo wakumba waandishi, ikiwemo ya gharama za uchapishaji pamoja na urasimu uliopo katika makampuni ya uchapishaji. Yaani mchapishaji anafaidi sana kuliko msaani aliyeumiza kichwa chake na kuandika kazi husika. Kama huamini hilo waulize waandishi wengi wakongwe ambao vitabu vyao tumevitumia hadi mashuleni na vingine bado vinaendelea kutumika. Wengi wamekuwa na majina makubwa na wanafahamika sana sana ila hawajafaidi jasho lao. Mfano unakuta publisher analipwa Milioni 200 ila mwandishi anapata milioni mbili. Au laki saba hivi.

Kwa kulitambua hilo makampuni mengi yakaleta njia sahihi kwa kila mwandishi (Haijalishi ni mkubwa au mdogo) ili aweze kuchapisha kitabu chake pasipo kutumia GHARAMA yeyote, na kujiingizia kipato kikubwa sana mara kumi zaidi ya kupeleka kwa Publisher. Njia hii inaitwa uchapishaji binafsi au SELF PUBLISSHING kwa kiingereza.
Uchapishaji binafsi au self Publishing ni ule uchapishaji ambao mwandishi husika wa kitabu anaufanya kwa njia ya mtandao. Hapa mwandishi wa kitabu au andiko Fulani haingii gharama zozote na kitabu chake kinafika kwa watu zaidi ya milioni moja duniani kote. Hapa msanii ndie anafanya kazi zoote za uchapishaji wa kazi yake na haki zoote zinakuwa juu ya msanii na si vinginevyo. Kwa njia hii kitabu au andiko la mwandishi laweza wafikia watu zaidi ya milioni moja duniani katika mataifa tofauti tofauti.

SELF PUBLISHING Imetengeneza mamilionea wengi sana. Kinachotakiwa ni ujuzi wako na uwezo wako wa kuandika kitabu au makala nzuri ikavutia wasomaji. Pamoja na mtandao wa internet na kompyuta ya kawaida tu. Vitabu hivi vinauzwa kwa bei ya dolla. Kwa mfano ukachapisha kitabu kimoja ukawa unauza shilingi dolla 10. Ukauza kopi 1000. Ukizidisha hapo utaona ni kiasi gani cha pesa unaweza ingiza kwa kufanya uchapishaji binafsi wa kazi zako. Sio vitabu tu pia hata nyimbo na filamu. Uzuri wa mitandao hii inakufanya uuze kazi zako kimataifa zaidi na sio ndani tu. Wenzetu nje wana utamaduni sana wa kusoma vitabu. Kwa mfano mimi nilichapisha kitabu changu kinaitwa CHOZI LA SUNDI. Kwa kuwa nilikuwa mgeni kuna mambo mengi sana nilikosea. Ila bado ndani ya miezi 3 niliuza kopi zaidi ya 1500 (licha ya kitabu kuwa na makosa mengi sana). Hivyo nilikifuta mtandaoni nafanya marekebisho nitakirudisha tena hapo baadae kidogo.

Andika chochote kile unachoweza kukiandika, kisha soma hii makala itakuongoza kuingia sokoni hatua kwa hatua, na mimi nitakushika mkono kwa ushauri . Pia waweza kuwa unajua namna gani ya kuchapisha au kuuza kitabu mtandaoni ila suala la namna gani kitabu chako kiuze likawa tatizo kwako. Tatizo kubwa linalo wakumba waandishi wengi ni namna gani awafikie hadhira wake, ukikosea hapo hata uwe mwandishi nguli kama Charles Mloka au Ngugi Wa Thiong’o lazimaa katika soko utafeli. Kwa kupitia makala hii nimeeleza kila kitu humu ndani kitakuongoza. Kama mimi niliweza nikiwa mchanga wewe pia waweza. Tafadhali usiache ndoto na kipaji chako kipotee kitumie ipasavyo na kikuingizie mamilioni leo hii

Katika makala hii tutajifunza namna gani uchapishaji wa vitabu unafanya katika mitandao na namna gani mwandishi anaweza jifunza kuchapisha vitabu vyake na kuwafikia watu zaidi ya milioni moja ulimwenguni na kujiingizia mamilioni ya fedha. Sio tu vitabu pia msaani wa filamu au nyimbo anaweza kuuza kazi zake huko na kuzisambaza. Tutajifunza hatua kwa hatua mwanzo hadi mwisho. Pia tutajifunza namna gani unaweza kukiuza na kukisambaza kitabu chako au kazi yako ya kisanii.

UCHAPISHAJI BINAFS V/S UCHAPISHAJI WA KAWAIDA

Miaka ya nyuma ili uweze kuchapisha kitabu chako ulitakiwa kwenda kwa Agent wa kampuni Fulani ya uchapishaji kisha agent huyu angesoma na kupitia muswada wako (Manuscript). Baada ya kuusoma agent huyu angeupeleka katika kampuni Fulani la uchapishaji nalo lingeupokea na kuupitia kuona kama unafaa au lah. Muswada kupokelewa na kampuni ya uchapishaji haikuwa guarantee ya kitabu chako kuchapishwa na kuuzwa katika maduka ya vitabu na maktaba.
Hivyo pasipo kupitisha muswada wako kwa Agent kampuni ya uchapishaji isingepokea kazi yako mikononi mwako kamwe.

Uchapishaji binafsi umeonekana kuleta tija na mafanikio kwa waandishi wengi na kuinua hali zao za uchumi. Uchapishaji binafsi ndio uchapishaji bora na wa kisasa kwa karne hii
Hapa chini kuna jedwali linallonesha tofauti katika Nyanja zote mbili za uchapishaji wa vitabu.

SIFA HUSIKA UCHAPISHAJI BINAFSI UCHAPISHAJI WA KAWAIDA
Unahitaji kuwa na Agent Hapana Ndio
Utalipia gharama Hapana Ndio
Una haki zote za kazi yako Ndio Hapana
Malipo yako ni uhakika 100% miaka yote Ndio Hapana
Unahtajika kutafuta soko kitabu chako Ndio Ndio
Una uwezo wa kudhibiti wizi wa kazi zako Ndio Hapana
Unaweza chapisha kwa makampuni mengi Ndio Kwa makubbaliano kisheria
Kazi yako kuwafikia mamilioni ya watu kwa wakati mmoja Ndio Hapana
Unauwezo wa kudhibiti malipo Ndio Hapana
Uwazi katika malipo ya kitabu chako Ndio Hapana
Unachukuwa Muda mfupi Ndio Hapana

Kwa kuzingatia hilo leo hii waandishi wengi wa vitabu wamechagua njia hii mpya ya uchapishaji binafsi wa vitabu na kujiongezea kipato cha mamilioni ya fedha.
Kuna njia kuu mbili ambazo mwandishi katika upande wa uchapishaji binafsi anaweza kuchagua. Njia hizi mbili zinamsaidia mwandihsi aweze kuchapisha kitabu chake vizuri na kwa ufasaha kabisa.

Kufanya mwenyewe (Do It Yourself) DIY
Katika njia hii mwandishi wa kitabu anaamua kufanya kila kitu yeye mwenyewe pasipo kumshirikisha mtu mwingine. Hapa tunategemea mwandishi ahariri kazi yake (Editing), abuni kava la kitabu chake (Cover design) na atafute masoko ya kitabu chake (Marketing)
Njia hii sio busara sana kuifanya kwani ni mtu 1 kati ya elf 10 ndio walifanikiwa kwa njia hii.

Kusaidiwa (Assisted
Hii ndio njia salama ambayo mwandishi wa kitabu anashauriwa kuitumia. Katika njia hii mwandishi na machapishaji binafsi anatakiwa kuwasiliana na baadhi ya watalaamu katika tasnia ya uandishi wa vitabu ili wampe muongozo. Katika hili tunategemea mwandishi

MAELEZO YA MSINGI

Kuna kampuni nyingi sana zinazojihusisha na masuala ya self publishing ila leo nitaongelea kampuni kuu tatu tu ambazo nimewahi kufanya nazo kazi na nina uwezo wa kumsaidia mtu akafanya nazo kazi na kujiingizia kipato chake.
Kampuni ya kwanza ni Amazoni (www.amazon.com ) hawa ni wauzaji wakubwa wa vitabu lakini hawa amazon wana kampuni nyingine inaitwa

Kindle Direct Publishing au maarufu kama KDP (Hii ni kampuni ya Amazoni upande wa uchapishaji) ambayo website yao ni www.kdp.amazon.com hawa sio tu kuwa waweza ku publish vitabu bali waweza ku upload kazi nyingine za audio katika mfumo wa CD au DVD. Hata wanamuziki mbali mbali wanaweza pia kuweka kazi zao hapa na wakauza zaid na zaidi. Mwanamuziki naeza weka album yake hapa na akauza sana tu.
Pia sio tu wanamuziki hata wacheza filamu wanaweza kuweka filamu zao hapa na bado zikafanya vizuri na wakauza na kuwafikia watu wengi sana kimataifa.

Kampuni ya pili inaitwa Create Space ila nayo ni kampuni tanzu ya amazon. Ila hivi karibuni hii kampuni imeunganishwa pamoja na KDP. Ila kabla hazijaunganishwa ni kwamba kwa kutumia hii kampuni tulikuwa na uwezo wa ku publish vitabu kwa lugha hata ya Kiswahili ila kwa sasa kwa kuwa imeunganishwa pamoja basi na KDP haikitambui Kiswahili basi uwezekano wa kukipublish. Ila jamani kuna uwezekano wa ku publish kwa Kiswahili huo uwezekano upo na ninaweza kukuonesha na kukusaidia vizuri tu.

NB: hata kama ukipublish kitabu chako kwa kutumia KDP, Lulu au Create space still kitauzwa Amazon tu.

Kampuni nyingine ya uchapishaji inaitwa LULU www.lulu.com hii nayo inatoa huduma kama za kampuni ya azamoni. Na uzuri wake ukipublsih kitabu huku waweza kukiuza Amazoni, Scribd, Kindel, Barnes & Noble pamoja na ibook.

Katika Self publishing kila kitu anachokifanya publisher basi anakifanya mwandishi wa kitabu husika. Kwa mfano kujua template gani utumie (nitaeleza manaa ya template ni nini na unaipata wapi wewe kama mwandishi), una I squeeze namna gani, kuipanga kuanzia table of contents unavifanya mwenyewe.

HATUA YA KWANZA
PANGA KITABU CHAKO
Ili uwe mwandishi mzuri wa vitabu na pia ujiingizie kipato kizuri sana katika kazi yako ni lazima upange au plan kazi yako. Utapangaje kazi yako, sasa hizi hapa ni baadhi ya mbinu zitakazo kusaidia kupanga kazi yako na kufanikiwa kuuza vizuri zaidi.
1. Chagua hadhira yako. Maana yake ni kuwa hapa kama mwandishi lazima ujue unamuandikia nani kazi yako au ni nani ni walengwa wa kazi yako. Pia kama msanii wa filamu au mwanamuziki kazi yako imelenga watu wa aina gani na wa rika gani. Je hawa hadhira wako wapi na ntawapataje hasa.? Nitaelezea kila kitu hapo baadae
2. Angalia uhitaji wa kitabu chako au mada utakayoizungumzia katika kitabu chako. Kisha jiulize je mada hiyo inahitajika kweli? Huwezi andikia hadhira yako mada ambayo haihitajiki hata kidogo. Hapa yakubidi kufanya utafiti Fulani wa mada husika. Kwa hiyo hapo utaangalia masuala ya kitu kimoja muhimu sana kinaitwa key words. NItafafanua vizuri sana hapo baadae maana hapa ndio utajiri na mfanikio yamejificha.
3. Wapi utakiuza na njia gani utatumia ili uuze. Hapa ni muhimu sana kwa mwandishi anayejitengenezea kipato chake kutokana na uandishi wa vitabu. Na je utatumia njia gani kukiuza? Nitaelezea pia namna gani au sehemu gani waweza kukiuza kitabu chako kikakupa hela nzuri. (Ndani ya hii Amazon). Hii Pia nitafafanua kila kitu hapo baadae.
4. Jina la kitabu na Cover la kitabu hivi vina maana kubwa sana katika uuzaji wa vitabu mitandaoni. Pia hata uuzaji wa filamu pia cover linamata sana nitawaambia baadae ni namna gani unatakiwa kufanya. Kumbuka uuzaji wa vitabu mitandaoni kitakachotokea ni picha au cover la kitabu chako na maelezo sas ikitokea kama Cover la kitabu chako halivutii basi hakuna mtu atakaye vutika kukinunua. Kuna aina na namna ya ku design cover la kitabu chako utakachokiuza mtandaoni, sio kila cover linafaa kuuza kitabu mtandaoni hapana. Nitafafanua hapo baadae pia.
5. Muda wa kukiingiza soko. Hapa napo ni muhimu sana kwa mwandishia au msanii anayetaka kufanya hii kazi kibiashara. Provided amechagua mada nzuri basi afikirie mada hiyo kuuza vizuri sana. Baadae nitafafanua mda gani hasa unatakiwa kuingiza kitabu chako sokoni na kwa mada gani.
6. Tafta mhariri wa kitabu chako huyu ni mtu muhimu sana ni mtu atakayekuwa anaksaidia sana kuhariri kitabu chako. Ni vizuri sana kuwa na wahariri zaidi ya wawili watakaokuwa wanakipitia kitabu chako au kazi yako ya kisanii. Pia kuna software nzuri ambayo nayo iko vizur katika masuala mazima ya grammar na punctuation hii itakusaidia kupanga kazi yako vizuri. Hadi zile passive na active voices. Pia nitaeleza ni wapi waweza pata wahariri wazuri wa kazi yako na uta enjoy sana na kunishukur sana.
7. Tafta Template nzuri itakayoendana na kitabu chako. Kumbuka template ni ile sehemu utakayochapia kazi yako (Iko kama page ya Microsoft word). Hii template lazima iendani na size ya cover lako. Nitakueleza ni namna gani waweza pata hii template na ni rahisi sana hata motto wa std 7 anaweza kufanya.

HATUA ZA UCHAPISHAJI
Katika mada hii nimeweka summary ya maelezo ambayo yanatoa angalau mwanga kidogo tu kwa mwandishi au msanii mwenye nia ya kufanya uchapishaji binafsi. Maelezo kamili na hatua za kufanya kazi hizo nitazitoa katika Kijitabu changu chenye ufafanuzi kamili, hatua na mifano kamili ya nini unatakiwa kufanya kama mwandishi. Kijitabu hicho kina muongozo woote, unachotakiwa kufanya kama mwandishi ni kuwa na kompyuta yenye mtandao wa internet na kazi yako iliyokamilika baasi. Waweza kununua kijitabu hiki kwa shilingi 10,000/= tu na ukajiunga na group la Telegram ambapo nitafundisha na kuwasaidia woote muweze kuchapisha kazi zenu.

Pia nitakusaidia na kukushika mkono popote unapokwama. Hasa katika masoko na katika kujisajili na kujaza taarifa za kodi. Na cha muhimu maswala ya kuchagua jina la kitabu liendane na nini hadhira yako inahtaji kwa wakati husika. Pia nitakusaidia namna ya kuandaa template yako na wapi waweza ipate template na kuweka kitabu chako.

Kujiunga nasi utafaidika kwa kupata muongozo wa wapi waweza pata cover nzuri ya kitabu chako na wapi waweza pata wahariri wazuri wa kitabu chako. Pia maelezo ya mitandao mingi na software za bure ambazo zinatumika ku Hariri kazi za wasanii na kuzisambaza. Kwa bei nafuu sana.

HATUA KWA UFUPI
Kitu cha kwanza unachotakiwa kufanya ni ku sign up (Create KDP account) ukishabonyeza hiyo sehemu itakuletea taarifa kibao za kujisajili.

Your Name: Utaweka jina lako
Email: Utaweka Email yako
Password: Utatengeneza password yako
Re-enter password: Utarudia kuweka password yako kasha bonyeza Create your KDP account.
Baada ya hapo utabonyeza agree with these terms, ukimaliza hapo utaona kuna windo mpya ime jitokeza na inakwambia kuwa Your account Information is incomplete ambapo chini yake kuna kitu kimeandikwa Create New title ambapo kun alama ya kujumlisha yenye maneno Kindle ebook na maneno Paper back.
Halafu kuna maneno mengine kama Book content, book cover, description, keywords and category na chini yake kuna ISBN. Taarifa hizi nimezielezea kwa undani kabisa katika kitabu changu. Na nimeelezea hatua kwa hatua na nini unatakiwa kujaza. Hasa upande wa masuala ya kodi maana kumbuka wewew sio raia wa Marekani. Pia nimeeleza aina mbili za vitabu mitandaoni (PAPERBACK & KINDLE EBOOK). So hakikisha unakipata kwani ukikinunua na mimi nitakuunga mkono kukusaidia sehemu yeyote utakayokwama.

KAMA HUWEZI KUANDIKA KITABU NINI UNATAKIWA KUFANYA?
Sio watu wote wana uwezo wa kunadika kitabu wengine wana uwezo wa kusmilulia tu. Hata wewe pia una kipaji ndugu yangu usikate tama kabisa ipo njia ya kisasa ya kukusaidia kuuza masimulizi yako na kuwafikia watu wengi na kujiingizia kipato.
wa kitabu chako.
UCHAPISHAJI

Nenda katika website yako ya KDP kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa bookshelf. Window itafunguka na itakuwa na vitu vifuatavyo.
Kuna sehemu imeandikwa Create New Title Hii maana yake ni kuwa unaenda kuanza kazi mpya ya uchapishaji. Na chini ya hii neno kuna maneno mamwili yaliyo katika viboksi na alama ya kujumlisha
Kindle ebook
Paper back

Maana ya haya maneno ni kuwa mwandishi anauchaguzi wa either kuchapisha ebook (Nitaelezea maana yake na faida zake)
Au kuchapisha kitabu cha Paper back. (Pia nitaelezea ni nini na faida zake)
Pia kuna maneno kama

Book content: Ambapo inakuruhusu wewe mwandishi kuweka muswada wako wa kitabu au. Ukatumia format ya bure toka KDP.
Book Cover: Hapa unaweza weka cover ya kitabu chako au kama huna kava basi utatumia online cover creator ya KDP. Japo sikushauri kabisa kutumia hiyo kitu
Description, Keywords and Categories: Hapa ni namna gani hadhira yako utaijulisha kuhusu kitabu chako na namna gani wanaweza kukipata Amazon.

Hivyo basi unapoanza kuchapisha kitabu chako chagua ni Paper back au ebook kisha bonyeza chaguo husika. Kwa ushauri wangu mimi nakushauri uufanye paperback kwani inalipa sana kwa mwandishi pia unaweza ijumuisha na ebook (Utaona huko mbeleni)

Ukishabonyeza paperback itafunguka page yenye sehemu 3 ambazo Unatakiwa kuzijaza kwa undani na kwa makini sana.
1. Paperback Details
2. Paperback Contents
3. Paperback Pricing and Rights

Hizi zote nimezielezea kwa undani sana katika kijitabu changu.
Naweza nisiwe mwandishi nguli au mwenye kipaji kama wewe ila niamnini mimi hii njia ni mkombozi kwako nimeifanya na nimechukuwa muda mwingi sana kuwa mentored na wauzaji wa vitabu maarufu. Nimeiona hii kama fursa hasa kwetu sisi watanzania. Jamani karibuni tusaidiane naamini tutatoka.
 
Aiseee vyema sana mkuu nimependa sana idea yako
utasaidia sana wanaohitaji kuandika vitabu
 
Swali la msingi...kwa mfano nimeandika kutabu changu, mteja akitaka kukinunua anakipata kama soft copy au hard copy?
Na kama ni hard copy, amazon ndiyo wanaprint kwa ajiki ya mteja au ni mimi naprint copy kibao na kuzituma huko amazon?
 
Mkuu unasemeaje amazon kindle unlimited na faida zake,
ni platform gani kwa sasa wanapublish vitabu vya kiswahili?
 
Swali la msingi...kwa mfano nimeandika kutabu changu, mteja akitaka kukinunua anakipata kama soft copy au hard copy?
Na kama ni hard copy, amazon ndiyo wanaprint kwa ajiki ya mteja au ni mimi naprint copy kibao na kuzituma huko amazon?

Mkuu hapo hilo ni chaguo lako unataka mteja akipate katika namna gani kati ya hizo ulizozitakja hapo juu. Amazon ndio wataprint na kumtumia mteja wewe ushaandika na kuchapisha baasi.

Kwa maelezo zaidi kaka njoo katika channel hii
JIFUNZE "SELF PUBLISHING" YA VITABU AMAZON
 
Hiki kitabu chako kinapatikana wapi? maana topic hii nimekuwa nikitafuta maelezo yake mda
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom