RRONDO
JF-Expert Member
- Jan 3, 2010
- 54,833
- 119,883
Kumekuwa na malalamiko mengi sana kuhusu watu kuibiwa mafuta kwenye vituo. Sio mbaya kuelimishana nini cha kufanya ili kuepuka wizi huu.
Kabla ya kujua nini cha kufanya ni vizuri tujue njia kuu zinazoweza kutumika kukuibia mafuta.
1.Kukuwekea mafuta bila ku-reset mashine. Yaani anakuja bodaboda au gari anaweka 5000/10,000 ukija wewe mhudumu anaendelea kukuwekea kuanzia 5000/10,000 ile ile.
2.Pump iliochezewa, yaani kwenye lita moja yenyewe inaweka ml 700 etc.
3. Pump inajaza upepo badala ya mafuta hii ni hatari zaidi.
Njia za kuepuka wizi huu ni hizi
1.Hakikisha mashine ime-reset 0000 kabla ya kuwekewa mafuta. Ukifika kituoni acha uboss, ikibidi shuka kwenye gari hakikisha mhudumu kaanzisha 0000
2.Nenda na kidumu cha lita 5 mwambie akujazie mafuta lita tano, angalia kidumu kilivyojaa na geji(kwenye pump) inavyosoma.
Ukifanya hayo mawili hapo huibiwi mafuta hata siku moja. Kingine nashauri uchague kituo kimoja uwe unaweka mafuta hapo hapo. Wakikuzoea hawawezi kukufanyia uhuni,pia lolote likitokea unajua ni wao tu.
Lakini ukiweka mafuta randomly hapa 3000 pale 10000 unaweza ukawa unamlaumu mtu bure kumbe uliibiwa jana ulipoweka 10,000 umekuja kushtukia leo ulipoweka 20,000.
Mimi huwa naweka mafuta weekly,thamani ile ile ya hela kazi yangu ni kuangalia idadi ya lita na mshale umefika wapi, siku zote mshale unakuwa eneo lile lile,hawezi mtu kuniibia.
Hio video hapo chini inaonesha pump inavyojaza upepo badala ya mafuta. Kwa hisani ya Wi-Fi