Jinsi ya kuendesha Biashara ya canter

Harry Barry

Member
May 12, 2016
14
16
Habari wana jf
Kama kichwa kinavyojieleza mimi ni kijana mjasiliamali nimekua nikifanya biashara tofauti tofauti kwa muda sasa na kila siku nawaza kufanya kitu kipya

Nipo hapa kwaajili ya msaada wenu wana jf kuhakikisha nafikia malengo yangu kama mjasiriamali

Hivyo basi nimefanikiwa kununua magari aina ya CANTER ton 3.5 pamoja na CANTER ton 2.5 tipa kwaajili ya biashara kwasababu ni biashara ambayo niliiona inalipa kupitia kwa rafiki yangu ambaye kwasasa tumepotezana baada ya kwenda nje ya nchi

Hivyo basi nahitaji usaidizi jinsi ya kupata madereva waaminifu na pia kujua hesabu ya wiki ni kiasi gani kwa kila gari moja.

Natanguliza shukrani
 
Umenunuwa gari bila kuwa na basic knowledge ya vitu vidogo kama hivi? Utaiweza vipi hiyo biashara?
 
Habari wana jf
Kama kichwa kinavyojieleza mimi ni kijana mjasiliamali nimekua nikifanya biashara tofauti tofauti kwa muda sasa na kila siku nawaza kufanya kitu kipya

Nipo hapa kwaajili ya msaada wenu wana jf kuhakikisha nafikia malengo yangu kama mjasiriamali

Hivyo basi nimefanikiwa kununua magari aina ya CANTER ton 3.5 pamoja na CANTER ton 2.5 tipa kwaajili ya biashara kwasababu ni biashara ambayo niliiona inalipa kupitia kwa rafiki yangu ambaye kwasasa tumepotezana baada ya kwenda nje ya nchi

Hivyo basi nahitaji usaidizi jinsi ya kupata madereva waaminifu na pia kujua hesabu ya wiki ni kiasi gani kwa kila gari moja.

Natanguliza shukrani
Unapatikana Mkoa gani kwanza
 
Sababu ushanunua tayari na hauna ABCs basi tukushauri hivyo hivyo. Mimi nakushauri usichukue ela kwa kipande chukua ela kwa kila trip.

Paki gari zako hapo kila zikipata kazi ujue ni kiasi gani na inapeleka wapi, ujue dereva unamuachia kiasi gani na mafuta inatumia kiasi gani kwa umbali.

Mwache dereva atafute kazi akipata akufate kuomba chombo na kukupa briefing ya kazi. Ukimuachia dereva gari afanye biashara akuletee kipande utarudi hapa kutafuta mteja wa kununua screpa. Maana wale wanaunga route juu kwa juu halafu hata akipata 800k kwa siku atakuletea ela yako kama ni 200k kila siku itabaki hapo hapo.

Ni hayo tu.
 
Back
Top Bottom