Jinsi ya kudumisha uhusiano wa mbali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi ya kudumisha uhusiano wa mbali

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jpinduzi, Nov 15, 2011.

 1. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #1
  Nov 15, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  ​[​IMG]

  Siku zote mapenzi huyapa maisha thamani lakini wapo ambao hujikuta kwa namna moja ama nyingine wanatengana na wapenzi wao kwa sababu tu ya mihangaiko ya kila siku yakujitafutia ridhiki, masomo na wakati mwingine utengano huwa ni matokeo ya wapendanao kuishi sehumu tofauti hii huwakumba sana wanafunzi wa vyuo na shule za bwen

  Umbali hulifanya penzi baina ya wapendanao kuteteleka kama wapendanao hawatafanya kazi za ziada kuhakikisha wanaziba mianya yote itakayosababisha usaliti kama sio kuachana kabisa.i.Hata hivyo, mapenzi ya mbali huna ni vigumu kuteteleka endapo tu wapendanao wanamapenzi ya dhati na kutamani kuwa pamoja kila wakati na mmoja wapo kuamua kujitoa muhanga kwa kuamia anakoishi ama kufanyia kazi la azizi wake. Hata hivyo, mnaweza kudumisha mapenzi yenu ya mbali endapo utafanya haya:-
  Mawasiliano ya mara kwa mara
  Mawasiliano ni nguzo muhimu sana baina ya wapendanao, humfanya kila mtu kuhisi uwepo wa mwenzi wake hata kama atakuwa mbali naye. Hivyo, kama una mpenzi wako aliye mbali nawe hakikisha unakuwa naye karibu kwa kumtumia ama sms, email, kadi au simu.
  Aidha, pindi mnapowasiliana hakikisha humkwazi mwenzako kwa namna yoyote ile, kwani kuna watu wengi wanatabia ya kudharau baadhi ya mambo kutokana na kutingwa na shughuli kadha wa kadha, naomba nikuweke wazi kuwa hata kama umebanwa vipi pindi mpenzi wako aliyembali anapokutumia ujumbe kwenye simu yako basi usisite kumjibu katika muda muafaka na siyo kuuchuna hadi ulalamikiwe!

  Heshimu hisia zako
  Mapenzi ya kweli yametawaliwa na hisia kali ambazo ndizo huwafanya wapendanao kufikishana kwenye mambo fulani kwani pasipo hisia hata uwe na ujuzi au utundu wakutosha hutapata raha ya mapenzi.
  Kama kweli unampenda kwa dhati mwenza wako na mmetengana kutokana na sababu za kimasomo ama kazi kwa hakika utakuwa tayari kumtunzia penzi lake hadi mtakapokutana tena.
  Uaminifu pekee ndio utakaokufanya uwasiliane mara kwa mara na mwenza wako na kwenye uaminifu mapenzi hushamiri huku kila mmoja akimuonea wivu wa hapa na pale mwenzi wake, lakini sio ule wakubomoa! Hivyo heshimu hisia zako kama kweli unampenda mwenzi wako kwa kumuonyeshe unampenda.
  Umbali si kigezo cha kunyimana
  Mpe mwandani wako raha kamili kama ilivyokuwa awali mlipokuwa pamoja! Bila shaka unajiuliza inawezekanaje? Hili linawezekana kwa kutumia njia yoyote ya mawasiliano. Mfano kama nyote mna simu jiandaye vyakutosha nikiwa na maana uhakikishe upo sehemu ambayo utakuwa huru kuongea ama kufanya chochote kitakachokufanya uhisi raha isiyo na kifani na kukufikisha kwenye kilele cha mlima kilimanjaro bila kutarajia.

  Bila shaka kila mtu anamfahamu vema mpenzi wake na hasa nini hupenda kufanyiwa ili aweze kufika safari yake na kama ndivyo basi hakikisha unafanya mambo yote ambayo ukimfanyia mwenzi wako pindi mnapokuwa kwenye mambo furani hupagawa.
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  uongo mtupi
  asiyekuwepo na lake halipo,fimbo ya mbali haiuwi nyoka.

  Tunadanganyana ila ukweli tunazungukana
   
 3. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #3
  Nov 15, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Marrytina ukweli ndo huo!Ukifuata tu wala nadhani hakuna tatizo lolote!
   
 4. M

  Marytina JF-Expert Member

  #4
  Nov 15, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  hayo ni maneno ya kujifariji na kujihesabia huibiwi ila ..................
   
 5. PROF. ENG

  PROF. ENG Senior Member

  #5
  Nov 15, 2011
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante shem!!
   
 6. JS

  JS JF-Expert Member

  #6
  Nov 15, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nikuulize: mbona umeamua kutumia picha hii?? ina linkage yoyote na thread hii??
   
 7. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #7
  Nov 15, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Sama hani kama nimetumia picha yako ila unaweza kuipata tangazo -
   
 8. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #8
  Nov 15, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Js samahani kama ndo wewe ila unaweza kuipata picha hii kwenye tangazo -
   
 9. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #9
  Nov 15, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kuna ukweli kidogo, japo ni vizuri ku Assume kwamba hauibiwi mali yako hata kama wajanja wanakula kisera.
   
 10. e

  ejogo JF-Expert Member

  #10
  Nov 15, 2011
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  I don't believe in long distant relationships!
   
 11. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #11
  Nov 15, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,500
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Asante Jpinduzi!
   
 12. Jatelo

  Jatelo Member

  #12
  Nov 16, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mi nlishafanya yote hayo unayosema ila niliambulia kusalitiwa mpaka sasa cpendi na cdhani kama ntapenda tena, chako ulichoshika kikiwa kwingine cha wengine. Tena hao wa vyuo ndo nyoko kabisa bola anaefanya kazi,
  nawasilisha
   
 13. Tulizo

  Tulizo JF-Expert Member

  #13
  Nov 16, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 849
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Long distant relationships = delayed Regrets + delayed Pain
   
Loading...