jinsi ya kudhibitiana kwenye mapenzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

jinsi ya kudhibitiana kwenye mapenzi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by figganigga, Jan 31, 2012.

 1. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,975
  Likes Received: 6,612
  Trophy Points: 280
  Habari jf.
  Unapoanza uhusiano na mwanamke na mambo yakawa yanakwenda vizuri, yaani akakukubalia ombi lako, utaiona dunia kuwa mahali pazuri sana pa kuishi.

  Mara nyingi katika hatua za awali kila mmoja huwa na tabia njema na kila mmoja anajitahidi kwa kila awezavyo kumfurahisha mwenzake, ili hatimaye kuufanya uhusiano kujenga mizizi na kisha kutimiza malengo.

  Lakini baada ya muda, kila mmoja huanza kujiona amefika kwa mwenzake na kumwona
  mwenzake kama mwenye bahati kwa kumpata yeye. Yakishakuja mawazo haya, mtu huanza
  kumchukulia mwenzake huyo katika hali ya kawaida sana.

  Muda si muda, kila mmoja huanza kubaini kasoro katika tabia za mwenzake, ambazo awali hazikuwa dhahiri. Kasoro hizi ni mwanzo wa kuvua ngozi ya kondoo ambayo ni muhimu katika kumtafuta mwenza, na kuanza kudhihirisha undani wa hulka yake.

  Japo hakuna mtu aliye mkamilifu, inashangaza na kukatisha tamaa kuona mtu uliyempenda kwa dhati anaanza kubadilika taratibu, si kwa wema, bali kwa ubaya.

  Kwa upande wa mwanamke, zipo tabia mbalimbali ambazo zinaweza kujitokeza, ambazo
  mwanaume anaweza akashindwa kukabiliana nazo. Makala hii inajadili baadhi ya tabia hizo mpya na jinsi ya kukabiliana nazo.

  ANAPENDA KUKULAUMU
  Kila mara anapofungua kinywa chake kusema, utamsikia akilaumu, akianza na maneno
  kama "Nilikwambia …", "Kwa nini usifanye hivi…", "Kwa nini kila mara unafanya hivi…"
  na kadhalika.

  Ukitafakari utabaini kuwa hakuna lolote unalolifanya akaliona la maana tena, ila kila ulifanyalo anaona unakosea. Hukulaumu na kukulalamikia kwa matatizo yote na wakati mwingine anaweza kukulaumu kwa kushindwa kusoma mawazo yake na kumwelewa katika jambo fulani.

  Tatizo ni kwamba wanawake wana matatizo katika suala zima la mawasiliano, kwa hiyo
  badala ya kusema moja kwa moja hutumia njia za lawama na malalamiko.

  Wanaume ni watu wasiopenda kulaumiwa, kwa hiyo ni vema mwanamke asitarajie faida kwa
  kumlaumu mwanaume maana hakika badala ya kumsaidia atakuwa anampoteza.

  Wanaume hupokea lawama kwa njia mbili tofauti: ama anaweza kusema tu kirahisi “Sawa
  mpenzi," au anaweza kumpuuza mpenzi wake na kuanza kumwepuka maana anamkera. Katika njia hizi mbili, hakuna iliyo suluhisho la tatizo.

  Kukubali lawama zake na kuomba radhi hata bila kosa kutakufanya ujishushie hadhi na kujiweka katika hadhi ya ‘mbwa popi’; lakini pia kukwepa tatizo ni sawa na kukiwekea bandeji kidonda cha kansa na kudhani kimepona.

  Kwa hiyo, njia nzuri zaidi ni kukabiliana naye na kama una neno la kujibu na kujitetea, usinyamaze na kuondoka kwa kuogopa kumuudhi.

  Mwambie kwa uwazi na ukweli kabisa kuwa lawama zake zinakukera na kwamba hutaendelea kuzivumilia. Mtake naye awe wazi na kama ana shida aeleze kwa uwazi, maana wewe si
  mtabiri wa nyota uweze kufahamu ana tatizo gani.

  ANA WIVU WA KUTISHA
  Wanawake wengi hawajisikii salama. Hii ni kwa sababu ya kutokujiamini. Wanawake
  wengi huwaogopa wanawake wenzao kuwa watawapokonya wapenzi au waume zao.

  Mwanamke hufahamu kwa hakika jinsi ilivyo rahisi kwa mwanaume kuingia katika mitego ya mwanamke, maana hata yeye mwenyewe alitumia mitego fulani fulani kukupata.

  Mathalani, anafahamu jinsi wanaume wengi walivyo wadhaifu waonapo maziwa ya saizi wazipendazo vifuani mwa wanawake, na jinsi wanavyopagawa waonapo sehemu za juu za miguu ya mwanamke, au kitovu chake, hivyo wanafahamu jinsi walivyo na kazi kubwa ya kuwalinda wapenzi wao katika zama hizi za vimini na vitopu.

  Mwanamke mwenye wivu huchukulia kirahisi kuwa mpenzi wake anawatamani wanawake
  wengine, hata kama si kweli. Kwa hiyo atatumia nguvu nyingi na muda wa kutosha kukujaribu.

  Unapotoka na marafiki zako kwa ajili ya kinywaji kwenye kibanda cha karibu, atajiwa na mawazo kuwa huko uko na mwanamke na anaweza kujipitisha pale ‘kwa bahati mbaya’ ili kuhakikisha kuwa uko na wanaume wenzako au mwanamke.

  Kwa mwanamke huyu, kama utachelewa kurejea nyumbani, basi ni kwa sababu ulikuwa
  katika mapenzi na mwanamke mwingine na kama utabainika kuwa na marafiki wa kawaida
  wa kike, basi mawazo yake ni kwamba ni mahawara wako.

  Mwanamke mwenye wivu anaweza kuyafanya maisha yako kuwa mabaya, kwa hiyo unapaswa kuchukua hatua haraka iwezekanavyo. Ukimwona mpenzi wako ana wasiwasi na uaminifu wako, mweleze kuwa anapaswa kukua na kujiamini katika uhusiano wenu.

  Muulize kama wapo wanaume anaowadhania kuwa wanavutia na iwapo anafikiria kufanya
  nao mapenzi. Mweleze kuwa kama hayo ndiyo mawazo yake, basi asilazimishe na wewe uwe
  na mawazo kama hayo.

  Njia nyingine ya kupunguza na kisha kuondoa wivu wake juu yako ni kumwalika atoke
  nawe unapotoka na marafiki zako wa kike na wa kiume na mkiwa huko, mpe nafasi azungumze nao na ajipatie marafiki miongoni mwao. Kama hutafanikiwa kuondoa wivu wake, basi mwambie kuwa kama hawezi kukuamini basi amtafute mwanaume anayeweza
  kumwamini.

  ANA MILIPUKO YA HISIA
  Mara nyingi wanawake hawatabiriki. Dakika moja anaweza kuwa anakubusu na kukwambia jinsi anavyojisikia vema kuwa nawe, dakika moja baadaye analia kwa sababu amekumbuka neno baya ulilowahi kumwambia mwaka mmoja uliopita.

  Ubongo wa mwanamke hutawaliwa na mihemko na kwa sababu hii wanaume hupata wakati mgumu kuwaelewa wanawake. Hata hivyo, hali hii ya kimaumbile si sababu ya kuyafanya maisha ya mwanaume kuwa magumu.

  Japo ni wazi kabisa kuwa huwezi kubadilisha jambo la asili, ni vema kumtaka mwanamke
  uliye naye kutambua tabia zake mbaya na kuzichunga – anaweza akawa hajui kuwa anakukera, kwa hiyo mweleze kwa hekima.

  Wakati mwingine ukibaini kuwa laazizi wako ana matatizo ya kihisia, nenda zako matembezini. Kama anayo matatizo dhahiri, msikilize. Usijitolee kutoa ushauri kama hajautaka kwako, wala usijaribu kutafuta suluhisho la tatizo lake kama hakukujia kwa
  ustaarabu.

  Kwa upande mwingine, hupaswi kuvumilia manyanyaso yoyote yatokanayo na mabadiliko ya
  kihisia ya mwanamke.

  ANAPENDA WANAUME WAMWONE
  Wakati mwingine unaweza kukuta msichana uliyempenda, ni mchangamfu kwa kila kijana
  wa kiume na kila anapotoka, huvaa nguo fupi au zile zinazoonesha vema maungo yake.
  Zaidi ya hapo, anapopokea simu hawi muwazi, bali hupenda kuzungumzia pembeni ambako
  hutamsikia.

  Mwanamke huyu anaweza akawa hana mpango wa kutembea na mwanaume mwingine yeyote,
  lakini kila mara hujiweka katika mkao wa kuwatega wanaume. Huyu anaweza kuwa na
  tatizo la kisaikolojia, pengine hajiamini sana na angependa aendelee kujihakikishia
  kuwa wanaume wanateseka kwa ajili yake.

  Ukiwa naye huyu njiani halafu akaonekana kutaka kuamsha hisia za vijana wa kiume, ni
  wazi kuwa atakuaibisha na utajiona kama mjinga. Unapaswa kukabiliana na tabia hii
  haraka iwezekanavyo.

  Mwambie mrembo wako kuwa kama anataka kuwa na wewe, basi akuangalie wewe na si kila
  mwanaume. Mwambie kuwa hakuna lelemama katika jambo hilo na kama ataonekana kutoweza kubadilika, mpe ruhusa ya moja kwa moja kwenda kwa wanaume awatakao.

  HAPENDI KUKUACHIA NAFASI
  Yupo mwanamke mwingine ambaye bila wivu wala nini, atataka aendelee kuwa pamoja
  nawe. Atakupigia simu mara 20 kwa siku, atakuja ofisini au nyumbani mara kwa mara,
  atakutumia kadi za ‘nakupenda’ na ‘nakumisi’ mara kwa mara, atakuuliza mara kwa mara
  una mawazo gani kuhusiana na uhusiano wenu, na kadhalika. Mwanamke huyu kwa hakika
  amekukalia kooni na anakunyima nafasi ya kupumua.

  Katika hali hii, ni wazi kuwa utawapoteza hata baadhi ya marafiki zako wa kiume,
  maana umedhibitiwa na mbaya zaidi anakuingiza katika utaratibu wa kufanya mambo ya kike na kukuweka katika mkao wa kuwa na furaha kuwa naye kila mara, eti kwa sababu mnapendana.

  Hakuna mwanaume yeyote mwenye akili timamu anayeweza kukubaliana na hali hii.
  Mwanaume anapaswa kuachiwa uhuru wake wa kuendelea kuwa mwanaume. Kijana wa kiume
  huhitaji nafasi na kujisikia, ama akiwa peke yake, au na wanaume wenzake.

  Ukijihisi kuwa kuna dalili za kukaliwa kooni, mwambie mpenzi wako kuwa mahusiano yenye mafanikio hayahitaji wenza wawe pamoja kila wakati. Mwambie kuwa unapokuwa mbali na mpenzi wako ndipo unapokuwa na hamu kubwa zaidi ya kuwa naye baadaye.

  Mwezeshe kukutana na watu na kujitengenezea marafiki kadhaa. Mtambulishe kwa ma-girlfriend (au wake) wa marafiki zako ili siku nyingine ajisikie kuwa nao.
  Mhimize kupanga mambo yake binafsi na kuwa na kitu anachokipendelea.

  HAPENDI KUFANYA MAPENZI
  Mwanzoni mwa uhusiano baina ya watu wa jinsia mbili, mwanamke huwa au hupenda kuwa karibu na mpenzi wake na kwa kuzingatia makubaliano yao, watu hawa wanaweza kuwa
  wanafanya mapenzi bila tatizo lolote, lakini muda si muda, mwanamke anaweza kuanza
  kuutumia mwili wake kwa manufaa binafsi, mathalani kukomoa, au kushinikiza matakwa yake.

  Kwa asili, wanawake hawana msisimko wa kimapenzi kama walio nao wanaume na wanao
  uwezo wa kujizuia kuhemka kimapenzi kila watakapo na ndiyo maana wanaweza kutumia
  ngono kama fimbo.

  Hata hivyo, ngono ni sehemu isiyoepukika katika uhusiano wa kimapenzi baina ya mwanaume na mwanamke, hususan kwa upande wa mwanaume, kwa sababu hiyo, kama unajidhania kuwa na haki na mwili wake, hupaswi kuvumilia tabia hii.
  Wapo wachumba ambao hukubaliana kuwa hawatafanya mapenzi hadi watakapooana. Kama anakukatalia katika muktadha huu na anataka mpime afya zenu kisha kupewa baraka za
  wazazi na viongozi wa dini, hilo ni jambo jema zaidi, kwani ndiyo maadili mema, lakini jambo hili lisikubalike katika hali ambayo una uhakika kuwa una haki na mwili wake.

  KUWA MAKINI
  Njia pekee ya kujenga mahusiano imara, ni kukubaliana na kuelewana. Lakini kama
  unajikuta katika matatizo ya upande mmoja kama yaliyobainishwa hapo juu, basi
  pengine unawajibika kuutathmini uhusiano wako na mwenzako.

  Kama mpenzi wako yu radhi kubadilika, ni vema, maana ni kwa mustakabali mwema wa
  uhusiano wenu – lakini kama hataki, basi ujue kuwa una mtihani mkubwa mbele yako.

  Ni hayo tu. mia
   
 2. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Uuuhshuuu... Nahsi nahtaji wiki nzima kusoma hyo post.
   
 3. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Watu wanapo kutana kwa mara ya kwanza, huwa hawatambuani hulka bali panatokea mvuto tu. Na bahati mbaya huo mvuto hautambui hulka. Baada ya kuwa pamoja kwa kipindi fulani ndiyo unakuja kuzi fahamu hulka. Sababu mvuto bado unakuwepo basi wote mna anza kuji adjust na mwnzio. Tatizo lina anza pale wakati mmoja hataki kuji adjust. Na hapo ndiyo mwanzo wa kuchujuka huo mvuto.
  MTU HACHUNGWI BALI ANAJICHUNGA MWENYEWE
  na
  UKIMCHUNGUZA KUKU UTASHINDWA KUMLA
   
 4. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  shit mimi wangu anajiona mzuri sana.kila saa story zake ni flani kanitamani,flani kanitongoza n.k
   
 5. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Nimesoma nusu ntarejea tena kumaliza oooooiiii
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  "Anajiona"??!Ina maana sio mzuri sana?
   
 7. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #7
  Jan 31, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hahaaaa kweli amekukuta na wewe umetulia tuli wamsikiliza.
   
 8. The dirt paka

  The dirt paka JF-Expert Member

  #8
  Jan 31, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Actually ndefu sana hiyo sijaisom yote, ila wanawake mjifunze kuheshimu wapenzi wenu nasi wanaume tuwapende bakika tutadumu katika mahusiano yetu.
   
 9. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #9
  Feb 1, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,975
  Likes Received: 6,612
  Trophy Points: 280
  mtu inabidi uongee kwa ulefu ili ueleweke. mapenzi yana uwanja mpana, huwezi yaongelea yote. hayo ni mache tu. Mia
   
 10. mkudeson

  mkudeson Senior Member

  #10
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  binafsi imenisaidia sana. Thanx a lot!!
   
 11. mkudeson

  mkudeson Senior Member

  #11
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hili ni tatizo la watanzania. Hatupendi kabisa kusoma na ukitaka kumficha kitu mtanzania, andika hicho kitu kwenye maandishi.
  kwa ujumla mnatakiwa mbadilike. PENDENI KUSOMA!!
   
 12. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #12
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  figganigga a.k.a mia..thanks kwa huu uzi, yani nimereflect sana mahusiano yangu!
   
 13. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #13
  Feb 1, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Asante kwa hii kitu mzee wa mia,
  Ni usefull kwangu na nimeondoka na mafunzo ya kutosha,
  Ubarikiwe sana,100.
   
 14. s

  sawabho JF-Expert Member

  #14
  Feb 1, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Kama wewe leo ungekuwa Kiongozi mwenye dhamana na nchi, halafu hii thread ni mkataba wa uwekezaji, tayari tungeanza kuibiwa, maana ungesaini bila kusoma vipengele vyote. Afadhali Chief Mangungo wa kule Msovero, Usagara alisaini mikataba na Dr. Carl Peters bila kujua kusoma, sisi tunajua kusoma lakini ni wavivu wa kusoma na kufikiri.
   
 15. MWAMUNU

  MWAMUNU JF-Expert Member

  #15
  Feb 1, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 661
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mi kiukweli huu uzi umenishika sana !!
  endelea kutufundisha baba asan sana !!!
   
 16. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #16
  Feb 1, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  ni kweli....just give me a break then i will be back kuisoma zaidi
   
 17. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #17
  Feb 1, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,072
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  dah!...kweli mkuu. asante sana.
   
 18. G

  Green Apple Member

  #18
  Feb 2, 2012
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mhh imenigusa,i have s0me characterz ntabadilika kmya kmya
   
 19. 3squere

  3squere JF-Expert Member

  #19
  Feb 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 928
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mape..... Mi kizunguzungu baba angu
   
Loading...