Jinsi ya kuchemsha maji ya kunywa

Squidward

JF-Expert Member
Jul 21, 2014
6,925
7,936
Wadau,

Ni muhimu unapoandaa maji ya kunywa kuzingatia usafi katika zoezi hilo. Usafi wa mazingira, chombo utakachochemshia na chombo utakacho hifadhia.


BOILING_WATER_POT_GENERIC.jpg



1. Hakikisha jiko unalochemshia lina moto wa kutosha. Kwa wale wanaotumia mkaa wahakikishe mkaa umewaka vizuri na hakuna moshi unatoka kwenye makaa (Moshi unaweza kubadilisha ladha ya maji hayo).

2. Hakikisha chombo (sufuria) unayochemshia ni safi na haina shombo ya harufu yoyote ile, ili kuhakikisha maji hayawi na harufu au ladha ya kitu kingine zaidi ya maji.

3. Mara nyingi ni vyema ukihakikisha maji hayo unapoyatenga jikoni yanafunikiwa vyema.

4. Hakikisha umeandaa chombo kisafi kwa ajili ya kuhifadhi maji yakishachemka. Usipende kuyaacha kwenye chombo ulichotumia kuchemeshia.

5. Kwenye maeneo ambayo maji yao huwa ni machafu, unahakikisha maji yametulia kisha taratibu weka katika chombo kingine huku ukihakikisha huyatingishi, ili kuepusha kuweka na ile rangi chafu iliyotwama chini. Pia kuna chujio yenye tundu ndogo sana (inakuwa kama chuma hivi) ambayo inafaa kuchujia maji hayo. Wengine hutumia kitambaa cheupe.

5. Kwa wale wenyewe wanaonamiliki majokofu, hakikisha maji yamepoa kabisa kabla ya kuyahifadhi kwenye Fridge au kabla huyajaweka barafu ya kupozea.


Nimewasilisha.
 
pamoja sana.. unashauriwa kutumia chungu badala ya sufuria, kiafya kuna materials si mazuri yanaweza ku affect maji
 
Kwa wapenzi wa karafuu, mkichemsha maji wekeni karafuu kama chembe 1 au 2 kwa kiasi chupa ya lita 1 na nusu.

Unapata harufu nzuri na ni dawa ya tumbo pia.

Nawasilisha...
 
Kumbe ndio hivi! Mimi huwa nanywa tu ila nilikuwa sijui ni jinsi gani yanaandaliwa.
Nalog off
 
Back
Top Bottom