Jinsi ya kubadilisha kisima chenye Maji chumvi kuwa maji baridi

kennyblue

Member
Apr 10, 2014
11
0
Wateja wangu wanataka maji matamu ( baridi) kisima changu kina maji chumvi, nifanyaje wana jf?

Nimeshauriwa niweke dawa ila hizo dawa sizijui.
 
kuwa macho, utaibiwa! maji yanayokuja kisimani mwako yanapita kwenye miamba yenye chumvi, unaambiwa uweke dawa itaenda yanakotoka? desalination ndo njia ya kuondoa chumvi kwenye maji, ni aghali sana ndo maana dar wanachukua maji ruvu na bahari ipo kwao!
 
Unachimbaje kusima bila kufanya survey kwanza kujua aina ya maji kama ya chumvi au baridi na umbali yalipo? Nenda pale DDCA karibu na chuo cha maji. Wanayo hiyo teknolojia.au kama vp wakupimie eneo lingine na wakuchimbie kirefu zaidi mpaka wakute mwamba wa maji mazuri
 
Confidence level ya huo upimaji wa ubora wa maji 'water quality' kabla hujayachimba ni kiasi gani?
 
Wateja wangu wanataka maji matamu ( baridi) kisima changu kina maji chumvi, nifanyaje wana jf?

Nimeshauriwa niweke dawa ila hizo dawa sizijui.
Ahahahahaa,simple.
Chukua mabarafu lori 7,chukua mifuko 100 ya sukari ya KK sukari ya Dewiji,mwaga kwenye likisima lako,baada ya dk 45 yaonje kama yatakua yameshakua matamu na baridi au lah.
Zingatia kipimo cha mabarafu na sukari.
Ahsante kwa kunielewa.
 
hivi wakuu hayo maji ya chini waweza kufanyia kilimo chaumwagiliaji?kwamfano yakawa yachumvi..nifunguen jaman..
 
Habari zenu wanaJF.
Kisima changu (bole hole) kinatoa maji ya chumvi.

Je kunauwezekano wa kuondoa au kupunguza chumvi kwa kiasi kikubwa ili niweze kuyatumiahayo maji kwa ajiri ya kilimo na ufugaji?

Kama zipo, je zina gharimu kiasi gani kwa kila option?

Yes, kuna machine za kuchuja chumvi kutoka kwenye maji. Gharama inategemea na volume ya maji unayotumia kwa siku, hakikisha kwako upo umeme kwani kwa generator unaweza kupata hasara. GOOGLE DESALINATION WATER SYSTEM
 
pima maji yako ujue content za minerals zilizopo kwenye maji yako.. na kujua chumvi ni ya iron, manganese, ph au nini?

kama mgonjwa unaingia maabara kwanza kupimwa then ndio unaenda kwa daktari..

so baada ya majibu kupata nenda nayo merry water au davis shirtif watakupa tiba ya ugonjwa wa maji yako
 
Pata like! Ni lazima kufahamu hiyo ladha imeletwa na madini yapi kabla hujaamua njia ya kuondoa
pima maji yako ujue content za minerals zilizopo kwenye maji yako.. na kujua chumvi ni ya iron, manganese, ph au nini?

kama mgonjwa unaingia maabara kwanza kupimwa then ndio unaenda kwa daktari..

so baada ya majibu kupata nenda nayo merry water au davis shirtif watakupa tiba ya ugonjwa wa maji yako
 
Ahahahahaa,simple.
Chukua mabarafu lori 7,chukua mifuko 100 ya sukari ya KK sukari ya Dewiji,mwaga kwenye likisima lako,baada ya dk 45 yaonje kama yatakua yameshakua matamu na baridi au lah.
Zingatia kipimo cha mabarafu na sukari.
Ahsante kwa kunielewa.

Jamiiforums mara nyingi huwa hunirudishia furaha na kuniondolea feelings flani hivi hata kama nimekwazika kiasi gani basi najikuta nikicheka nitake nisitake kwa kweli.

VIVA JF.

Kuna local technology ambayo nahusisha kuyapump yakishatoka unatengeneza system ambayo itakua na mchanga. Ila haimalizi chumvi yote inapunguza kiasi kikubwa cha chumvi
 
Hakuna kipimo kinacho Pima nakuonyesha kuha chini kuna Maji chumvi au hambayo hayana chumvi vipo vinaonyesha Maji kama yapo nakama yapo ni mitangap kwenda chini

Ni kweli hakuna kipimo kinachoonyesha dhairi kuwa maji yana au hayana chumvi ila kinachofanyika ni analysis ya data zinazopatikana wakati wa kufanya survey, actually wanachofanya ni kitu kinachoita electomagnetism, kuna kuwa na transimitter inayopeleka umeme ardhini na kunakuwa na receiver inayoupokea umeme unaotoka ardhini kwa interval fulani ya muda, wanachopima hapo ni Resistivity/conductivity hivyo kama maji yana chumvi conductivity inakuwa kubwa hivyo baadaya kupata data za kutosha na kuchora graph unaweza kujua haya maji yana au hayana chumvi
 
Back
Top Bottom