Jinsi ya kuandika barua ya Uchumba

gwambali

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
230
Reaction score
76
Salams Wana JF wenzangu!

Kama mnavyo jua changamoto za maisha zimetufanya tuwe mbali na familia zetu, hivyo yanapo kuja mambo muhimu ambayo yanahitaji usaidizi wa kifamilia imekuwa shida sana kwa vijana wengi.... Mimi ni kiwa kama kijana ambaye nahitaji kuwa na mwenza wangu wa maisha nimepitia katika kipindi kigumu sana hasa cha kupata watu wakaribu ambao watanisaidia kufanikisha jambo ili..

Nahitaji kupeleka barua ya posa kwa wazazi wa mchumba wangu, tatizo nililokumbana nalo ni watu wakaribu yangu ambao wanaona ili swala kama vile ni kubwa mna, Kabila langu ni mchaga mila na desturi zetu zinatofautiana na baadhi ya makabila ya hapa Tanzania hasa kwenye swala la kuposa binti.

Mila zetu ni kwamba unatafuta wazee watatu mnawatuma kwenda kwa wazazi wa binti wakiwa na Soda au Mbege, na wakifika kule watajieleza wenyewe kwajinsi wanavyo jua na baada ya hapo watajibiwa na wazazi wa binti na kupangiwa mahari na baada ya hapo wanarudi kukujulisha...


Mchumba wangu ni Mnyaturu, kwa mujibu wa mchumba wangu ameambiwa na wazazi wake natakiwa niandike barua ya posa ikiwa na kishika uchumba, ambapo itapelekwa na watu wazima kama wa 3 hivi.. Hapo ndipo palipo nipa mtihani kidogo, kwamba hiyo barua inaandikwa vipi? nimejaribu kuongea na ndugu zangu wameniambia wao hawakupitia utaratibu wa kuandika barua bali walituma watu tu...

Jamani naombeni mnifungue macho kwa maelekezo wa jinsi ya kuandika hiyo barua..


Kwa mujibu wa thread moja humu JF imenipa mwaga kidogo,


Ng'ongoampoku Amenifungua hapa kwa jinsi ya kuiandika barua ya posa, pia ningependa kujua zaidi ya hapa.


Nimepata Sampuli ya barua ya posa inavyo takiwa kuwa toka kwa ndugu Lighondi


Na imani hii thread itakuwa msaada kwangu na kwa wengine wengi tu, Tafadhalini na wakaribisha kwa michago yenu.
 

Attachments

ngoja nikusaidie kuandike hiyo barua ya posa.

ni mimi..................................nimekuja kumposa binti yenu.........................toka nilipomuona kwa mara ya kwanza binti yenu mapigo ya moyo yalienda mbio,nikawa kula sili,kulala silali,nikinywa maji namuona kwenye glass,nilichompendea binti yenu adi nikaona nilete posa,ni ayo mahaga yake hips,ana hips za ukweli bila kusahau inyegwede,tukija kwenye macho yake akiniangalia ni kama ananiita,yani kutoleta posa kwenu ingekuwa ni jambo ambalo ningejutia sana.
pia chuchu zake ni saa 6 kwa kweli nikaona nilete posa leo,infact mkiniruhusu nimuoe binti yenu mtaenjoy sana,mtakula bata,nampango fungate pia niwashirikishe na nyie wazazi twende sote,mtafurahi sana yani msipoteze hii bahati ivo mniruhusu ni muoe bint yenu.
nina sababu kubwa ya kuwaambia mniruhusu nimuoe binti yenu,mimi niko na pesa sana mtaenjoy for da rest of ur life,
ni wako mme mtarajiwa wa binti yenu mashalah.................
weka sahihi.......................
tarehe.........................

huu ni mtazamo wangu wakuu nimemsaidia ili apewe mke na posa ikubaliwe,mia
 
Mnyaturu uwiiiiiiiiiii
mi sijasikia
 

Dah! hii hataree!! lazima urudishwe na posa yako... Nashukuru hata hivyo mkuu!
 
Nimepitia zoezi hili mimi mwenyewe mwaka juzi na mwakajana nimesimamia hili zoezi kwa rafiki zangu wawili. nipm email yako nikutumie sampuli utachagua unayotaka. taarifa za muhimu ni anuani zote mbili kwenu na kwao, lengo la barua, utambulisho wako wewe baba yako na mama yako, unakotoka hapa mjini na kule mgombani kwenu. Then unataka kumposa nani (ful name pamoja na ya wazazi wake na mahali wanakotoka) Then maliza barua yako kisha weka saini.
 
Shukrani mkuu, Ngoja ni ku-PM
 
mkuu kwaajili ya vijana wengine wa hapa jf hebu wawekee aina ya barua hiyo wajue inafananaje??
 
Ningekua sijaoa, i would have gone for this...lolz!
Umenichekesha sana mpwa!

 

tehe!tehe!tehe!tehe!
Hapa lazima upewe mke bure!
 
Jamani nataka kuchumbia,nimeambiwa nipeleke barua,naomben kwa wazoefu wanisaidie huwa inakuaje? Contents na je ni kama official au?
nisaidieni
 
Jamani nataka kuchumbia,nimeambiwa nipeleke barua,naomben kwa wazoefu wanisaidie huwa inakuaje? Contents na je ni kama official au?
nisaidieni

kama upo serious ni pm namba yako ya simu
 
Jamani nataka kuchumbia,nimeambiwa nipeleke barua,naomben kwa wazoefu wanisaidie huwa inakuaje? Contents na je ni kama official au?
nisaidieni

Mkuu ushi hongera kwanza kutaka kuoa.Tafuta wazee wa hapo mtaani nadhani wanaweza kukusaidia kwenye hilo.
 
Hongera sana!
Nimeoa Mnyaturu,nilianza kwenda ukweni kabla ya kutoa posa coz nilikuwa namega kisela,siku ya ndoa nilipigwa faini ya pesa.Bint ni alikuwa akiishi Dar so mambo ya kutoa ng'ombe 5 hayakunipata coz gharama ya moo m1 si mchezo.
Unataka kujua mila za kinyaturu unapoenda ukweni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…