Jinsi wasomi wanavyodhalilishwa Bungeni

Haya ndio madhara ya wataalamu na wasomi wetu kukimbilia siasa na kuacha taaluma zao. Ona sasa wanavyozodoana na wanasiasa wasio wasomi. Wangebaki kwenye taaluma zao vyuoni na kwengineko na kuwaacha wanasiasa katika siasa yasingewakuta haya
 
Wao walifuata nini huko Bungeni.?
Inabidi wazoee tu kwa kuwa kuna mahala inabidi watumie elimu yao kujifanya wajinga.
Msomi anayelalamika Bungeni huyo si msomi anayeitumia elimu yake vizuri.
 
Kwahiyo msukuma anafaa kuwa Mwl.wako? Watanzania tumekuwa tukisombwa na mihemko sana.Alichokiongea Prof.Mhongo ni kwa mujibu wa tafiti mbalimbali duniani kote kwamba umeme wa maji si wa kutegemea kwa karne hii ya sasa kutokana na mabadiliko ya mara kwa mara ya hali ya hewa. Bahati mbaya mzee Magu alikuwa hashauriki,na hatuwezi kuzuia mradi kwa sasa kwani tayari ujenzi unaendelea.

Na Kilichosababisha Magufuli kuachana na gesi ya Mtwala ni ubovu wa mkataba uliopo kwenye bomba la gesi ya Mtwala. "Charges" zake ziko juu mno na Magufuli siku zote alijipambanua kuwa mtetezi wa wanyonge. Isingekuwa hivyo hivi tunavyoongea pesa yote hiyo angetumia kwenye kuwekeza kwenye gesi.
 
Msomi anayesema tuachane na mradi ambao umeshakula trilioni 2 ni mpumbavu kama wapumbavu wengine
 
..Tatizo hawa wasomi wamechagua kutumikia taifa kule ambako elimu zao hazistahili....wangebaki tu vyuoni...huku kwenye siasa kunawafanya washindwe kufikiri kwa level zao....
Tupe evidence kuwa msomi ni mahususi kufanya kazi vyuoni tu?
Wasomi hawafungwi na usomi wao, wanaweza kufanya kazi popote bila kuvunja sheria.
Hivi wasomi wote Tanzania wakafanye kazi vyuoni, hivyo vyuo vinazo hizo nafasi?
 
Mkuu inatupasa kufanya analytical study kati ya gesi na maji, wapi kwenye nafuu, tusiufuate mihemko ya kina kibajaji ambao hawajui uchambuzi wa mambo mazito unavyofanywa.
 
Wakipewa uwaziri wanajitoa ufahamu,hawana uwezo waa kutambua koleo nini, badala yake husema kijiko kikubwa 'they call a spade a big soon'
 
Lakini kwa ujumla chambuzi wa Muhongo na wa Assad, ni kisomi sana, tatizo kule bungeni kuna mashindano ya kumponda au kumsifu mwendazake!
Lakini ni kweli kwamba kuna wasomi wanaokana taaluma zao kwa ajili ya matumbo yao, kama walivyo viongozi wa dini wanaokana imani zao kwa sababu hizo hizo!
 
Hivi wewe na akili zako unakubali upuuzi wa Prof wa Geology Muhongo na pesa za kuhongwa za gesi yeye na JK watudanganye? Ingawa sikubaliani na hoja ya la saba, ila Prof yeyote anatakiwa kuwa makini akiwa anatoa hoja. Aliboa siku ile wakati tunajua alivyopata mrungula
 
Alichosema Muhongo, tusitegemee maji tu, ambayo mabwawa yanaweza kukauka, ni muhimu kuwekeza kotekote! Sema tatizo pale mjengoni kuna wale wanaondelea na zile ibada zao kwa mwendazake, hao kina kibajaji!
Let us be realistic, umeme wa maji ni onetime investment na rehabilitation. Unajua umeme wa gesi wewe! Acha mchezo. Sasa jazia na ule ufisadi, ndo maana JPM aliona bora kuanza upya, tatizo ulikuwa ni ufisadi ambao usingeshusha bei ya unit ya umeme
 
Tatizo maprofessor wote wawili walioongea juzi kati wote walikuwa very subjective! Kitu ambacho kimepelekea wao wenyewe kujivunjia heshima.
 
Wasomi wanajiangusha wenyewe kwa kutokujiamini na kuwa na misimamo ya Kisomi kama wa kenya, wao akili na usomi unaishia kwenye tumbo
 
Tatizo hapa sio lasaba wala phd,hapa ni ccm kukikana na mabadiliko,swala LA ajira bila elimu limepitwa na wakati.INAUMA sana
 
Hayo masalia ya Magu ndio yalikuwa yamewaaminisha watu kwamba Kazi ya serikali ni Kazi ya mtu binafsi huku yakiiba pesa

Bora Mungu kaondoa jitu lilioanza kujigeuza Mungu mtu na kuabudiwa na wajinga walio wengi
Alikumbatia majinga akayapa kauli na fursa ili atoboe kiulainiii.
 
Unamueleza zaidi Musukuma kwa sababu hata wewe upeo wako ni mdogo tu kama Musukuma!
Unamuelewa kirahisi kwasababu anaeleza lugha rahisi unayoielewa kama vile kumuomba Rais Magufuli wakasafishe kiroba cha mchanga wakapata milioni 16!
Nilidhani hiyo ndio KAZI ya msomi kuchanganua Mambo magumu na kuyaeleza Kwa lugha nyepesi inayoeleweka Kwa Umma especially huu wa Tanzania ambao asilimia kubwa elimu yetu ni ya kawaida.
 
Msukuma alifanya uchunguzi akajua kwamba mchanga ulikuwa na madini , professor hakujua akamdharau ! Akaona hawezi kushauriwa na darasa la saba . Baadae ikajulikana ni kweli ikawa aibu kwa professor ! Mimi siungi mkono darasa la saba kuwa bungeni ila katiba yetu inaruhusu . Tuwaacha wachape kazi mpaka katiba itakapobadilishwa . Kawali kadogo ! Alikotokea msukuma hakuna wasomi ? Ni kwa nini wakamuacha akapita ! Aliwashinda na hoja !

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
Kama Prof mwenyewe nu Muhongo ngoja ayapate anayostahili...!! Mzee unamuambia ule mchanga unaoenda Ulaya mle kuna mali wanatupiga anakujibu fyongo..!! Muhongo anawaona watu wasio na PHD kama wehu wala hana time yakuwasikiliza ata kidogo..!! Linadharau sana lile jibu. Si alimuambia Mengi hela yake akawekeze kwenye juice yule..!!
 
Mimi binafsi namuelewa sana Musukuma kwa sababu anajua kujenga hoja yake in a simple way ikaeleweka. Ila sasa hao wanaojikuta maprofesa au madokta wakati mwingine speech zao huwa zinaniacha na mshangao sana. Na mara nyingi huwa najiuliza ni kwamba hawaelewi kweli au ni kwamba wana mtu wanayemtumikia hadi wanakuwa wanautweza weledi wao kiasi hicho?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…