Urban86
JF-Expert Member
- Jan 26, 2014
- 276
- 127
MWAMINI NI #KIUMBE_KIPYA
Je unajua nini kilitokea katika kuokolewa kwako?
Je! Unafahamu umekuwa nini mara baada ya kuwa na imani katika kufa kuzikwa na kufufuka kwa Kristo ili wewe uhesabiwe haki?
Wewe umekuwa #Kiumbe #kipya!
2Wakorintho 5:17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
Wagalatia 6:15 Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya.
Neno “kiumbe kipya” limetafsiriwa kutoka neno la Kigiriki “kainos ktisis” ambalo lina maana ya mtu mpya, kiumbe kipya (new specie, a new person,), yote pamoja katika Kristo.
Upya huu siyo habari ya kitu cha zamani au kikuukuu kilichofanyiwa marekebisho, hapana! Ni upya ambao haukuwapo, kitu ambacho hakina historia, hakikuwahi kuwepo (A real brand new thing). Ndiyo sababu mahali pengine jambo hili linaitwa uzao mpya, a new birth.
Upya huu ni kwa sababu upo ndani ya Kristo, kwa Imani katika Kristo; imani katika Injili. Upya huu sio badiliko la tabia, upya huu ni habari ya asili yako mpya katika Kristo.
Mwamini, kwa utambulisho pamoja na Kristo (identification with Christ) alizikwa pamoja na Kristo, alifufuka pamoja naye na ana maisha mapya.
Warumi 6:4 Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.[5] Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake; [6] mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena; [7] kwa kuwa yeye aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi. [8] Lakini tukiwa tulikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye;
Wakolosai 3:1 Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu.
Kwa hio katika mind ya Mungu, Kristo alipokufa, ulikufa naye (utu wako wa kale/dhambi, au asili yako ya dhambi) ilikufa pamoja naye. Na Kristo alipofufuka ulifufuka pamoja naye, ukawa na utu mpya, ukawa umezaliwa kiumbe kipya. Huku ndiko kubatizwa katika Kristo, kuzamishwa kabisa ndani ya utu wa Kristo na kutambulishwa pamoja na huo kiasi unakua kitu kimoja (roho moja) na YEYE! (to be totally immersed and identified with Christ)
Kwa hiyo mwamini ndani ya Kristo hana historia ya nyuma, ndani ya Kristo hapana hata kumbukumbu ya dhambi na makosa kabla hajaamini. Ni kama mtoto mchanga aliyezaliwa- hana historia ya nyuma, ni mpya!
Ni makosa mwamini kusimama mbele ya kusanyiko akishuhudia maisha yake ya nyuma, jinsi alivyokua mchawi, mzinzi, mlevi, mwizi, muuaji… hayo ni mambo ya mtu aliyekufa, unaletaje habari za wafu katikati ya walio hai? Ushuhuda wa mwamini siyo huo, ushuhuda wake ni juu ya kazi ya Kristo na matokeo au impact yake kwake. Ndiyo sababu mwandishi wa Waebrania anasema tuyashike sana maungamo yetu, haya maungamo si juu ya tabia zetu kabla hatujaamini bali ni juu ya kazi aliyoimaliza Kristo kwa ajili yetu na matokeo yake.
Tunakiri na kushuhudia vile tulivyo ndani ya Kristo;
uzao mteule, taifa takatifu, haki, hekima, utakatifu, ukombozi, ukuhani wa kifalme, wenye masamaha ya milele, walio keti naye, wenyeji wa mbinguni, kanisa la wazaliwa wa kwanza, watu wa milki ya Mungu, wenye baraka zote katika ulimwengu wa roho, wenye kukaliwa na Roho wa Mungu, wenye maisha na uzima wa Mungu ndani yetu, wenye mamlaka dhidi ya falme zote na mamlaka, wamoja na Kristo, nuru, hekalu la Mungu, chumvi ya ulimwengu, utukufu wa Mungu, washindi, wateule, wenye pendo la Mungu, walioshirikishwa tabia ya kiungu, na kadhalika.. (hivyo ndivyo tulivyo katika Kristo, hayo ndiyo maungamo yetu)
Yes! Ndivyo ilivyo, Mwamini ni kazi ya Mungu:
Waefeso 2:10 Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.
Neno ni kazi yake ina maana ya kuwa mwamini ni kazi ya mikono yake (kito -masterpiece). Hii inaelezea ukamilifu wa mwamini, yeye ni uumbaji wa Mungu mwenyewe.
Si uumbaji wake, siyo jitihada zake, ni kazi ya Mungu, ametokana na Mungu, mtu mkamilifu, mtu kutoka/aliyezaliwa juu. Si wa udongo, si wa ulimwengu, amezaliwa mbinguni.
Usikubali mtu kukwambia kuwa utakuja kuwa kiumbe kipya siku ukiwa na tabia bora, wewe ni kiumbe kipya leo! Maandiko yanasema “umekuwa” siyo “utakuwa”
Hivyo ishi katika ufahamu wa kweli hii, huku ukibadili ufahamu na nia yako kwa neno la Mungu ili uchukue sura ya mtu wako wa ndani aliye mpya na mkamilifu. Kadri unavyokua katika kweli ya wewe ni nani katika Kristo, utakuwa ukibadilika katika mwenendo wako wa nje siku hadi siku.
Ndiyo sababu Paulo anasema; “bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia (ufahamu) zenu..”
Baada ya kuokolewa, umekwisha kuwa kiumbe kipya, kazi iliyopo ni kugeuzwa kwa ufahamu wako ili ufanane na mfano wa ule utu mpya ulio umbwa na matokeo yake ni ukuaji wako kiroho, ni tunda la roho, ni maisha yenye kuidhihirisha haki uliyo nayo tayari. Hivyo, Jifunze Kristo, Jifunze Neno la Mungu.
Usionewe!
Wewe ni Kiumbe kipya! Mwana wa Mungu kabisa!
Unajua nakupenda.
Felician Makarios
30 July 2019
Kainos Creation