Jinsi nilivyotapeliwa kizembe na muuzaji wa ‘Simu used kutoka Dubai’

Jinsi nilivyotapeliwa kizembe na muuzaji wa ‘Simu used kutoka Dubai’

Polisi wetu wangekuwa na watu competent halafu waandilifu huyu wala asingehitisha kwamba katapeliwa!!

Picha liliharibika kuanzia kwenye usajili wa hizo SIM cards ukizingatia wengi hawakuwa hata na hizo namba za NIDA matokea mawakala wakawa wanasajili laini kwa namba ya mtu mwingine na kuziuza zikiwa tayari zimesajiliwa.
Inauma sana kitu ukihangaikie kwa jasho na damu halaf mwisho wa siku mpumbav mmoja aje akichukue kirahisi

Sasa ndo naelewa kwa Nini mwizi Huwa haonewi hurumi
Pole sana Mkuu kwani Huna ndg hapa Dar....ila nikwambie kitu kimoja ktk haya maisha usimuamini mtu kwenye pesa...pesa ni shetani...mimi mwenyewe nilidhurumiwa 40k pale k/koo...ila mimi nilienda lutengeneza simu ilikua issue ya machine...basi bhana lile jamaa lile jitu lenye ukubwa wa mwili kama Kobisi Kikala halafu akili Kisoda likaniambia niliachie 40k kwaajili ya hiyo machine....na likaniaminisha kwamba Duka letu lile pale so Kesho njoo uichukue simu yako itakuwa tayari....ilipofika hiyo siku nikaibuka K/koo kucheki pale lilipokuwa linatengenezea Simu halipo Duka alilonierekeza kuwa laakwao limefungwa...nikajipa moyo ngoja Kesho nitakuja...ilipofika kesho nikaibuka kama kawaida nikakuta hali ni ile ile...nikajua hapa nishapigwa...ile kuulizia wale majirani zake wa pale wananijubu Jeuri...nikaenda polisi Msimbazi....wakati natoa maelezo kuna polisi alicheka saana....kuna Askari akajitokeza akasema simu ni ya bei gani na hela kiasi gani ulimuachia...nikamwambia simu ya 157k kisha akaniambia nitajie namba za huyo Jambazi... nimpigie...wakalipigia likapokea Kisha Askari akalihoji pale kisha likasema halipo Dar limesafiri kwenda Moshi inamaana Hela yangu ilitumika kama Nauli...likamwambia Askari kwamba mwambie huyo Dogo aende pale amuulizie mtu anaitwa Zaholo ampatie hela yake na simu yake kwababu Mashine nilikosa...Askari akanipa Go ahead nienda nikachue ..kumbe wakati naondoka pale polisi lile jamaa lilinyanyua Simu likampigia Zaholo kuwa Jamaa anakuja na Askari Funga Duka upesi...ile nafika pale nulizia Duka la Zaholo naambiwa hilo hapo ila hajafungua Leo ila nikiwaangalia usoni kama kuna ishara wanapeana..ikanibidi nirudi polisi...yule Askari akaniambia kama hajafungua nenda kesho itaendelea......
Daah ndo hivyo mkuu mjinga Mimi niliingizwa mjini na wajanja
 
Wakuu poleni na matatizo yanayoikumba nchi yetu. Poleni kwenu mliopoteza ndugu, jamaa, na marafiki kutokana na yaliyojiri oct29

Bila kuwachosha. Kuna msemo maarufu usemao """Wajinga ndiyo waliwao"""'

Ilikuwa tarehe 20 mwezi wa 11 mwaka 2025 ndo siku ambayo kwa mara ya kwanza nilihisi kuchanganyikiwa na kutembea barabarani nikiongea pekee yangu hii ni baada ya kutapeliwa kiasi Cha laki Moja na elfu kumi.

Mkasa mzima ulikuwa hivi

Siku Moja katika pitapita zangu mtandaon nikakutana na tangazo la mtu anaedai kuwa anauza simu used kutoka dubai

Kwa kuwa nilikuwa na shida na simu wakati huo basi nikachukua namba zake kama inavyoonekana hapo chino.

Nikawasiliana nae vizuri akanipa utaratibu wote unavyokuwa, maskin wa Mungu nikamwamini (kosa kubwa sana)

Akanielekeza kuwa Simu zipo ukifka dukani ni sh laki Moja ila kwa mkoani unalipia nauli elfu kumi akasema kuwa unatuma Hela Kisha ndo mzigo wako unapelekwa kwenye basi tayari kwa kusafirishwa

Basi akanitumia namba yake ya M-pesa Hela nikatuma Jina likaja Jaffari Yusuph

Baada ya muda kidogo akanipigia na kuniambia Hela nimeiona Kisha akaniuliza nikuchagulie ya rangi gani

Mimi nikamwambia nyeusi akaniambia nimtumie taarifa zangu nikamtumia

Hela nilituma saa nne asubuhi kwa makubaliano kuwa muda huo huo anawapelekea hao wanaosafirisha kuja huku mkoani (ilitakiwa ije kahama)
Na alisema kuwa akiwakabidhi atanipigia Ili kunijulisha mzigo umekuja na bus la aina gani ,nikasema sawa

Imefika Saa nane mchana mtu Yuko kimya saa tisa kimya

Ilipofika saa kumi na Moja nikampigia kumuuliza je simu inakuja na kampuni gani . muda huo akili imeshaanza kuvurugika

Akaniambia simu imepelekwa stendi na aloipeleka bado hajarudi, akirudi atanijuza kwa hiyo nivute subira

Saa Moja usiku kimya akili ndo ikanirudi nikajua nishatapeliwa kupiga simu ikawa haipokelewi mwisho akaizima

Nikiri wazi nilitamani kujiua hiyo siku kutokana na kwamba nimeweza kumtumia kiasi chote hicho mtu Ambae simjui

Nilijilaumu mno nilihisi kuchanganyikiwa kiasi kwamba nilijiona Mimi ni mjinga wa mwisho

Hii itabaki kwenye historia ya maisha yangu yote

Tangazo ndo kama lilivyo hapo chini

Jaffari Yusuph, Jaffari Yusuph popote ulipo Mungu anakuona

N.B:Nisamehen kwa uandishi mbovu

View attachment 3523259View attachment 3523260
Pole mkuu biashara za wabongo, ukiitwa pembeni, ukisikia mambo ya free delivery na mikoani tunatuma kaa kitaalamu,..
 
Pole sana Mkuu kwani Huna ndg hapa Dar....ila nikwambie kitu kimoja ktk haya maisha usimuamini mtu kwenye pesa...pesa ni shetani...mimi mwenyewe nilidhurumiwa 40k pale k/koo...ila mimi nilienda lutengeneza simu ilikua issue ya machine...basi bhana lile jamaa lile jitu lenye ukubwa wa mwili kama Kobisi Kikala halafu akili Kisoda likaniambia niliachie 40k kwaajili ya hiyo machine....na likaniaminisha kwamba Duka letu lile pale so Kesho njoo uichukue simu yako itakuwa tayari....ilipofika hiyo siku nikaibuka K/koo kucheki pale lilipokuwa linatengenezea Simu halipo Duka alilonierekeza kuwa laakwao limefungwa...nikajipa moyo ngoja Kesho nitakuja...ilipofika kesho nikaibuka kama kawaida nikakuta hali ni ile ile...nikajua hapa nishapigwa...ile kuulizia wale majirani zake wa pale wananijubu Jeuri...nikaenda polisi Msimbazi....wakati natoa maelezo kuna polisi alicheka saana....kuna Askari akajitokeza akasema simu ni ya bei gani na hela kiasi gani ulimuachia...nikamwambia simu ya 157k kisha akaniambia nitajie namba za huyo Jambazi... nimpigie...wakalipigia likapokea Kisha Askari akalihoji pale kisha likasema halipo Dar limesafiri kwenda Moshi inamaana Hela yangu ilitumika kama Nauli...likamwambia Askari kwamba mwambie huyo Dogo aende pale amuulizie mtu anaitwa Zaholo ampatie hela yake na simu yake kwababu Mashine nilikosa...Askari akanipa Go ahead nienda nikachue ..kumbe wakati naondoka pale polisi lile jamaa lilinyanyua Simu likampigia Zaholo kuwa Jamaa anakuja na Askari Funga Duka upesi...ile nafika pale nulizia Duka la Zaholo naambiwa hilo hapo ila hajafungua Leo ila nikiwaangalia usoni kama kuna ishara wanapeana..ikanibidi nirudi polisi...yule Askari akaniambia kama hajafungua nenda kesho itaendelea......
Jr. Muendelezo vipi? Mbona kimya mkubwa
 
Pole mkuu biashara za wabongo, ukiitwa pembeni, ukisikia mambo ya free delivery na mikoani tunatuma kaa kitaalamu,..
Nimejifunza japokuwa iliniwia ugumu kuukubali ukweli kuwa Hela yangu imeenda kimasihara ukiangalia mazingira niliyopitia mpaka kuipata basi tu
 
Back
Top Bottom